Polisi, kuajiri vijana wa umri huu ni hatari kwa usalama wa raia.

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Ninavyoamini mimi ni kuwa, vitu mfano wa silaha za moto zinapaswa zibebwe na watu wenye akili timamu. Jioni ya leo nikiwa katika mitaa ya uhindini mjini Dodoma nimeshuhudia tukio ambalo limenifedhehesha sana. Nimekutana na askari mwenye umri mdogo, naweza kusema ni mtoto kwani kwa jinsi alivyo sidhani kama umri wake unafikia japo miaka 18. Katinga sare za kifidifosi, na bunduki yake begani. Kibaya zaidi mikononi kashika pakiti ya pombe maarufu aina ya kiroba huku akiendelea kunyonya taratibu. Tangu wakati huo mpaka sasa nahisi moyo wangu ukiwa na hofu. Hakuna asiyejua madhara ya pombe, kwa mtoto kama yule kulewa huku akiwa na SMG Begani ni hatari sana kwa usalama wa raia. Wanaohusika walitizame hili mapema kabla madhara hayajatokea siku moja..
 
kakomaaa tu unaweza kukuta anamiaka zaidi ya 33 alafu kama amepiga depo moshi viroba vimeshamkolea hanashida.Utumiaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako na si utumiaji wa pombe ni hatari kwa afya yako.
 
siku hizi nafasi wanapeana kwa hiyo haijalishi mwili wa mtu hii inatisha. Nashut down
 
askari aliyejiua juzi ni ndugu yangu....alikuwa ni mtoto mdogo sana tu ..sijui huko kwenye mafunzo wanafundishwaga ninim..sijui kabisa
nina mpango wa kwenda mahalamani
 
Wengi ni vijana wadogo,na hata ukikaa nao wengi unaona upeo wao pia mdogo!
Ila pia ukiangalia vigezo wanavyotumia kuwapata hao wanaoingia kwenye mafunzo unapata picha ya kwa nini wako hivyo walivyo! kiukweli wengi huenda huko baada ya michakato mingine kuonekana imekaa ndivyo sivyo! so tunaweza kutegemea lolote kama hakuna usimamizi mzuri wa sheria zinazowaongoza.
 
kuna madogo niliwaona ilala wamebeba mashine hawazidi 18yrs, wala hawaelewi wanalofanya wapo wapo tu wanashangaa magari. kuna jamaa nawafahamu waliingia polisi na less than 17yrs
 
mkuu kwa mishahara yao, viroba havikwepeki...
ishu ya SMG, unashauri begani wabebe upinde au?
 
mkuu kwa mishahara yao, viroba havikwepeki...
ishu ya SMG, unashauri begani wabebe upinde au?

Wabebe lkn wawe na akili timamu. Si unajua kazi ya viroba ni nini! Au unafikiri viroba vya unga.
 
Hiyo ni tabia haizuiwi na umri. Kuna wazee kibao ila kila saa wamelewa.
 
MyTz this is very serious matter, ni ukweli usiopingika kwamba polisi wengi wanaoajiriwa sasa ni wadogo sana (jamani hivi huwezi kujua polisi mdogo na aliyekomaa?? hii si kweli hata kidogo!) tena form four failure, hasa wanaopelekwa CPP Moshi. Hii ina implications nyingi kwenye utendaji wa kila siku wa jeshi la polisi kwa sababu hawa ndiyo wanaotumwa kazi mbalimbali kama kuzuia maandamano (angalia walivyomng'ang'ania yule dada mwanachuo wa mlimani, kulinda mabenki etc). Mimi huwa najiuliza nini kimetokea kwenye jeshi hili kwa sababu vijana wengi ninawafahamu huwa naona kama ni kawaida kabisa kwao kupata kinywaji (viroba coz is cheap, but also beer) wakati wa kazi na sidhani kama huwa wanakaguliwa kuona kama hawajalewa. Hivyo umri mdogo plus ugumu wa maisha (huku wakijua wakubwa zao wakitanua) tutegemee nn? Hili jeshi jamani linahitaji total reform!!

Mkuu naweka nchi mbele na kukubaliana na wewe, uswahilini madogo wengi wanakuwa recruited kutokea matawi ya CCM, huanza na kazi za kusaidia kampeni na uahidiwa kazi ya upolisi na magereza. Wengine hupelekwa kunduchi, sehemu nzuri za kuwa recruit ni vijiwe vya tae kwan do ambavyo vimeshamiri huku uswahilini. Ni ajira kwa vijana ila wengi ni madogo ambao home yaani noma, south hakuendeki wala kukalika na kuchukua mapipa kwenda Greece siku hizi sio dili.
Matokeo yake wazee wa chama ndio sehemu ya kupata future.... This really scares me!! halafu kama kuna utemi fulani hivi wakiwa wanasita!, serious hii imeenea sana siku hizi.
 
Back
Top Bottom