Kwa Kamanda wa Polisi (RPC) - Tabora: Hali ya ulinzi na Usalama mali na raia manispaa ya Tabora ni mbaya!

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Sielewi polisi wa mkoa wa Tabora na hususani Manispaa ya Tabora chini ya RPC wenu mnakwama wapi.

Tabora manispaa ya hatari ya miaka ya 1990s na kidogo 2000s iliyokuwa imejaa uhalifu na ujambazi ni kama inarudi taratibu.

Miaka hiyo majambazi hawakuwa na urafiki na taa za barabarani. Kila serikali ilipoweka taa za barabarani walikuwa wanazipiga kwa manati na kuzivunja vunja ili kuwe na giza kuwapa fursa ya kufanya uhalifu wao nyakati za usiku.

Hali ya usalama wetu raia na mali zetu uko mashakani sana ni kana kwamba hakuna jeshi la polisi hapa.

Kuna ongezeko la wimbi la vibaka na ujambazi wakifanya matukio ya uhalifu waziwazi kana kwamba mna ushirika nao.

Nitawapa mfano wa tukio moja.

Linawahusu walimu watatu wa kike na bodaboda wa pikipiki.

Hawa usiku wa kuamukia kuanza mitihani ya taifa drs la VII mwaka huu walioponea chupuchupu kutekwa na kunyang'anywa kila walichokuwa nacho usiku wa saa 8.

Tukio hili lilitokea barabara ya kutoka Uyui gerezani jirani na Shule ya Sekondari Isevya.

Ilikuwa ni wakati wa mitihani ya darasa la saba. Walimu hawa walitoka nyumbani kwao wakielekea ofisi za manispaa ili kupanda magari kusambazwa kwenye shule mbalimbali kwa zoezi la usimamizi mitihani hiyo ya drs la VII - 2020.

Kila mmoja alipanda bodaboda ya pikipiki kutoka eneo la Ipuli kwa Nyembo.

Walipofika eneo la Isevya Sekondari kwenye makutano ya barabara ya Uyui gerezani na Ipuli walikuta gari na pikipiki kama tatu na kundi la vijana kama 7 hivi wenye mapanga wamevaa black masks kufunika nyuso zao wakiwa wamezuia barabara kwa yeyote anayepita hapo.

Waliwapiga mkono. Bahati njema mita kama 150 hivi, bodaboda alitambua kuwa hao ni majambazi. Aligeuza pikipiki yake kwa kasi na kurudi alikotoka na kubadilisha njia.

Cha kushangaza majambazi haya yalianza kumfukuza mpaka karibu na ofisi za manispaa. Walipoona wameingia ndani getini yakaachana nao.

Sasa hii ni hatari sana. Ni kana kwamba polisi mko likizo na mmeshindwa kufanya kazi yenu.

Hili ni moja ya tukio la ujambazi lililofanyika kwa ujasiri sana kana kwamba hawa majambazi wana ushirika nanyi polisi.

Tunawaomba jeshi la polisi fanyeni kazi yenu.

Kuna wimbi kubwa sana la majambazi kuwatumia watoto wadogo wa miaka 10 hadi 15 kutenda ujambazi wao. Chunguzeni hili na mlifanyie kazi.

Sisi tunachotaka ni Tabora iliyo salama usiku na mchana.
 
NGOJA RPC ni Nani? Yaani Majambazi Yanaamua Lolote

RPC wa Tabora ni mwanamama mmoja hivi (nimemsahau jina lake)..

Dada yangu mwalimu aliponea chupuchupu na bodaboda wake usiku ule kuporwa kila kitu na target kubwa ilikuwa kumnyang'anya yule dogo pikipiki yake...
 
Saa nane usiku mtoto wa kike anafanya nin road? Mi nilifikiri ukibaka wa mchana mchana hapo tungemlaumu RPC, sa usiku saa nane Jamani?

Mtoto wa kike unaranda randa tu na boda boda, mida ya wanga kabisa, kama ni hivyo bas polisi wana kazi kuigeuza hii Dunia kuwa paradiso
 
Sana nane usku mtoto wa kike anafanya nin road ? Mi nilifkr ukibaka wa mchana mchana hapo tungemlaumu RPC , sa usku sa nane Jaman , mtoto wa kike unaranda Randa Tu na boda boda, mida ya wanga kabisa , ... Kama ni hivyo bas polisi wana kazi kuigeuza hii Dunia kuwa paradiso
hujaelewa kwamba alikuwa anawahi manisapaa kwa ajili ya kwennda kusimamia mitihani ya darasa la saba,kuwahi usafiri kwenda wilayani..HALAFU TANGU LINI WANAWAKE HAWANA RUHUSA KUTEMBEA USIKU?ITANGAZWE TU kama ni hivyo
 
Sana nane usku mtoto wa kike anafanya nin road ? Mi nilifkr ukibaka wa mchana mchana hapo tungemlaumu RPC , sa usku sa nane Jaman , mtoto wa kike unaranda Randa Tu na boda boda, mida ya wanga kabisa , ... Kama ni hivyo bas polisi wana kazi kuigeuza hii Dunia kuwa paradiso
Acha uzwazwa hujui kusoma au

Kwahiyo majukumu aliyopangiwa kusimamia mitihani ya watoto wetu wa darasa la saba alale mpaka saa5 asubuhi halafu atafikishwa kituoni saa ngapi
 
Nimetoka huko juzi, sasa nipo Dom city.

Ila kutoka huko isevya secondary hadi manispaa kuna umbali na kama kweli walikimbizwa na kwa nature ya barabara basi hao bodaboda walikuwa wazembe, maana wangeweza kuwahi central police kuliko huko manispaa walipokimbilia.

Pia, Ofisi za manispaa tabora hakuna geti na halijawshi kuwepo, ni sijui kama litawahi kuwepo.
Hapo ofisi za manispaa ni karibu sana/mkabala na kwa mkuu wa mkoa na huko ndio kuna ukuta na geti kubwa sana ambalo hata dar kwa kunenge halipo.
 
Hao polisi wa Tabora ni mapimbi kweli kazi yao kuu ni kukamata pikipiki kutwa kucha , ulinzi na usalama wa raia hawana habari , waambie kukamata bodaboda hawalali , mitaa haipititika kwa sababu ya vitoto vidodovidogo , Kanyenye , Ng'ambo hakupitiki usiku , Kona ya Tabora boys hakupitiki I was there few days ago .
 
Sana nane usku mtoto wa kike anafanya nin road ? Mi nilifkr ukibaka wa mchana mchana hapo tungemlaumu RPC , sa usku sa nane Jaman , mtoto wa kike unaranda Randa Tu na boda boda, mida ya wanga kabisa , ... Kama ni hivyo bas polisi wana kazi kuigeuza hii Dunia kuwa paradiso
Mbona usomi story ukaimaliza.
Maswali utjijibu mwenyewe.
 
Mkuu soma vizuri kabla ya kuleta hoja yako
Sana nane usku mtoto wa kike anafanya nin road ? Mi nilifkr ukibaka wa mchana mchana hapo tungemlaumu RPC , sa usku sa nane Jaman , mtoto wa kike unaranda Randa Tu na boda boda, mida ya wanga kabisa , ... Kama ni hivyo bas polisi wana kazi kuigeuza hii Dunia kuwa paradiso
 
Tabora hasa wilaya ya Sikonge inabidi wajitathmini sana, pia matukio ya kinyama bado yanaendelea kuongezeka kwa kasi Sana, kuna kijana na mke wake waliuwawa na majambazi usiku kisa wanahitaji pesa na hawakuwa na pesa, wakajaribu kuwapa funguo wakafungue dukani na ndio kulikuwa na pesa, jamaa mwingine mtaa huohuo kakatwa na mapanga hasa sehemu ya bega, tunawasihi sana vyombo vya ulinzi viongeze bidii hasa ufuatiliaji wa matukio ya kutisha
 
Wiki iliyopita yaani j2 ya tarehe 13 nilikuwa wilaya ya Sikonge nikaambiwa ndani ya mwezi mmoja wameuwawa watu 4 na hakuna taarifa yoyote ya kukamatwa hao wahalifu
 
Sielewi polisi wa mkoa wa Tabora na hususani manispaa ya Tabora chini ya RPC wenu mnakwama wapi...

Tabora manispaa ya hatari ya miaka ya 1990s na kidogo 2000s iliyokuwa imejaa uhalifu na ujambazi ni kama inarudi taratibu...
Au Nasema uongo ndugu zangu?
 
Sana nane usku mtoto wa kike anafanya nin road ? Mi nilifkr ukibaka wa mchana mchana hapo tungemlaumu RPC , sa usku sa nane Jaman , mtoto wa kike unaranda Randa Tu na boda boda, mida ya wanga kabisa , ... Kama ni hivyo bas polisi wana kazi kuigeuza hii Dunia kuwa paradiso
Kwa nini usisome kwanza uelewe kabla ya ku comment?
 
Back
Top Bottom