Polisi jijini Dar wamjeruhi mtuhumiwa, yupo mahututi ICU

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Polisi Goba, Dar, wajeruhi kwa kipigo, majeruhi yuko ICU, anapumlia mashine, madaktari wasema, kupona kwake utakuwa muujiza wa Mungu....

Jumatano, November 10, 2021, Polisi Goba walimkamata Issa Kassim (20), nyumbani kwao huko Goba kwa madai kwamba ameuziwa TV ya wizi, tukio ambalo mtuhumiwa alikana kulitenda.

Baada ya kumkamata waliondoka naye wakidai wanampeleka kituo cha polisi Goba, lakini kabla ya kufika huko kituoni walimuomba awapigie simu ndugu zake waweze kumuokoa.

Mtuhumiwa alipiga simu kwa mama yake akazungumza na mmoja wa polisi hao aliyefahamika kwa jina moja la Majuto.

Askari huyo wa jeshi la polisi kituo cha Goba, katika mazungumzo na mama wa mtuhumiwa huyo alimuomba atume Sh 800,000 ili kijana wake waliyemshikiria kwa tuhuma ya kununua TV ya wizi waweze kumuachia.

Mama wa mtuhumiwa aliomba apunguziwe dau hilo, badala ya sh 800, 000 atume 500, 000 , ombi lake lilikubaliwa akatakiwa atume hiyo laki tano.

Wakati biashara hiyo ikiwa kwenye mazungumzo, mtuhumiwa alikuwa akisikia, alimzuia mama yake kuwatumia polisi hao fedha yoyote kwani hajatenda kosa lolote, anasingiziwa tu.

Baada ya mtuhumiwa huyo kuzuia fedha kutumwa kwa polisi hao, polisi hao wakiongozwa na Majuto, na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Paul walimpiga sana, hasa maeneo ya kichwa kwa kutumia nyaya ngumu wakidai ni jeuri anazuia wao wasitumiwe fedha ili aachiwe.

Baadaye tena, akiwa tayari amepokea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa polisi hao, alitakiwa kumpigia simu ndugu yake mwingine mwenye uwezo kifedha ili atume fedha hiyo aweze kuachiwa.

Alipigiwa simu binamu wa mtuhumiwa huyo aitwaye Tusekile Shadrack, ambaye alielezwa tukio hilo, na kutakiwa na afande Majuto, wa jeshi la polisi Goba atume fedha sh 800, 000 ili ndugu yake aweze kuachiwa na kufutiwa kesi inayo mkabili.

Ndugu huyo wa mtuhumiwa alimuomba polisi Majuto ampe namba yake ya simu amtumie fedha hiyo, aligoma kutoa namba yake, akamtaka atume kwenye simu ya mtuhumiwa au apewe namba ya wakala atoe kupitia huko, ilishindikana, fedha haikutumwa, mtuhumiwa alimzuia asitume chochote maana anasingiziwa tu, hajatenda kosa hilo.

Kipigo kwa mtuhumiwa kiliendelea, akiambiwa atakufa kwa sababu ya jeuri yake.

Alhamisi, November 11, 2021, asubuhi, Afande Majuto alimpigia simu Mama wa mtuhumiwa akimtaka afike Hospitali ya Mwananyamala haraka, hali ya mwanaye ni mbaya.

Mama huyo wa mtuhumiwa aliongozana na Tusekile kwenda Mwananyamala Hospitali, walipofika kweli walimkuta mtoto wao taabani, aliweza kuongea kwa shida sana!

"Nimepigwa sana, sidhani kama nitapona, niombeeni sana kwa Mungu, nimeumizwa, nakufa bila hatia yoyote, polisi wakiongozwa na Majuto, walinzi hawa wa raia na mali zao, wamenitesa vikali, wamenipiga kipigo kikali zaidi ya kile cha mbwa koko, wananiua eti kwa sababu nimewakosesha fedha za dhuruma walizotaka kuzipokea kutoka kwenu ndugu zangu, niombeeni, nami naomba, Mungu atanilipia" alisema Issa.

"Cha ajabu, yule mwizi waliyedai ameniuzia TV ya wizi aliachiwa, hakufika hata kituo cha polisi, aliambiwa tukiwa njiani tuna karibia kituo cha Goba atambaye, nakufa, nifikishieni salaam zangu kwa IGP Sirro, askari wake wanawatesa raia, wanawaua kwa kuwapiga wakitaka walipwe pesa kwa makosa ya kutengenezewa ili wapate fedha ya dhuruma, nakuacha mama, niombee kwa Mungu" aliongea Issa kwa majonzi makubwa.

Mwananyamala alifanyiwa kipimo cha cit-scan na MRI kichwani, wakadai mishipa ya mfumo wa fahamu kichwani imeathiriwa pakubwa, damu nyingi imevia, imeganda na kuikandamiza mishipa hiyo kwenye Ubongo.

Ilibidi haraka sana ahamishiwe Muhimbili, ambapo alipokelewa na yuko ICU, kwa mujibu wa maelezo ya madaktari bingwa wa Muhimbili wa mifumo ya fahamu ya kichwa(Neurosurgery) wanaomhudumia, wamesema kupona kwake ni asilimia moja, muujiza tu wa Mungu.!

Ndugu tumekata tamaa, hivyo tunaomba msaada wa kisheria na ushauri.


Sasisho

Polisi watolea ufafanuzi>>> Jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa malalamiko ya mwananchi mmoja dhidi ya askari polisi wa kituo cha polisi Goba
 
Daaaah MUNGU wangu ! Haya yanayotokea naona km ni ndoto jamani Eeh Mungu muweza muokoe Issa asiye na hatia
 
"Nimepigwa sana, sidhani kama nitapona, niombeeni sana kwa Mungu, nimeumizwa, nakufa bila hatia yoyote, polisi wakiongozwa na Majuto, walinzi hawa wa raia na mali zao, wamenitesa vikali, wamenipiga kipigo kikali zaidi ya kile cha mbwa koko, wananiua eti kwa sababu nimewakosesha fedha za dhuruma walizotaka kuzipokea kutoka kwenu ndugu zangu, niombeeni, nami naomba, Mungu atanilipia" alisema Issa.

"Cha ajabu, yule mwizi waliyedai ameniuzia TV ya wizi aliachiwa, hakufika hata kituo cha polisi, aliambiwa tukiwa njiani tuna karibia kituo cha Goba atambaye, nakufa, nifikishieni salaam zangu kwa IGP Sirro, askari wake wanawatesa raia, wanawaua kwa kuwapiga wakitaka walipwe pesa kwa makosa ya kutengenezewa ili wapate fedha ya dhuruma, nakuacha mama, niombee kwa Mungu" aliongea Issa kwa majonzi makubwa.
emoji15.png
emoji15.png
emoji15.png
emoji2827.png
emoji2827.png
emoji2827.png
emoji2827.png
 
Hii stori yote wewe umeipata kutoka wapi? Ulikuwa eneo la tukio au umesimuliwa na mgonjwa? Je wewe ni una uhusiano gani na mgonjwa/ mtuhumiwa?
Wewe ni mgeni wa hili jukwaa? taarifa zote zinazokuja humu watu huwa wanajitetea walivyo zipata?

Mtu anafikisha ujumbe kwa uchungu na kutafuta haki, unaleta ujuaji!? hiyo story kwa kuisoma inaonekana sio ya kutengeneza, bado unaleta ujuaji!
 
Kama hii stori ni ya kweli basi hao askari wana kesi ya kujibu na ushahidi wa maongezi baina yao na ndugu wa mgonjwa utapatikana toka mtandao wa simu uliotumika.

Ndugu wa karibu wangeanzisha kesi mapema mgonjwa akingali anaweza kujieleza ili maelezo yake pia yasaidie.

Poleni sana. Mwenyezi Mungu amuafu mgonjwa na kumjalia uponyaji.
 
Back
Top Bottom