Polisi hawana mamlaka kuzuia maandamano ila mahakama - Kimongoro

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
Ndesamburo(6).jpg

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (kulia) na
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa,
wakiwa nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana.


Wakili: Mbowe, Slaa, wabunge wamefunguliwa kesi ya kufikirika



Wakili wa utetezi Kimomogolo
katika kesi inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amewashauri polisi kwenda shuleni ili kusomea sheria kwa ajili ya kuepuka kesi za kufikirika kuzipeleka mahakamani na kusababisha kukwama kwa kazi za maendeleo kwa sababu ya kushughulikia kesi hizo. Aidha, amesema polisi hawana mamlaka ya kuzuia maandamano au mikusanyiko, isipokuwa ni hakimu pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuzuia maandamano au kama hakimu imethibitika hayupo anaruhusiwa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa mkoa kuzuia maandamano hayo kwa kupewa maagizo na hakimu.


Wakili huyo, Method Kimomogolo,
alidai hayo jana alipokuwa akitoa mapingamizi yake dhidi ya maelezo ya mashitaka yaliofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya wateja wake ya kufanya maandamano bila kibali na kutoa lugha za uchochezi. Kimomogolo alisema kuwa mapingamizi yake yanahusu mashitaka nane yanayowakabili washitakiwa wake 19, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa; wabunge, viongozi wa ngazi mbalimbali na wafuasi wa chama hicho. Wabunge hao ni Godbless lema (Arusha Mjini), Joseph Selasini (Rombo) na Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini).


Kimomogolo aliwasilisha taarifa yake kwa maandishi
kwa ajili ya kuipatia mahakama kumbukumbu na pia alitoa maelezo ya mdomo ili mahakama iweze kuyasikiliza. "Naanza kwa kusema kuwa hizi sheria lazima kila mmoja azipitie na kuzielewa, kesi hii imekosewa kuanzia mwanzo hadi mwisho na kwa kuwa imekosewa kuanzia mwanzo, imezaa makosa mengine yote," alidai.


Alidai kuwa katika shitaka la kwanza,
washitakiwa hao wanashitakiwa kwa kutenda makosa sita tofauti, wakati kisheria yalipaswa kuwa katika chaji sita tofauti yakiwa na maelezo ya kina, lakini hakuna kitu kama hicho. "Mfano, hapa inasema Chadema na washitakiwa walitoa taarifa kwa OCD Arusha saa zaidi ya 100 kabla ya mandamano waliyokusudia kufanya hapo Januari 5, 2011 na iliandikwa barua ya mombi hayo Desemba 31, mwaka jana 2010," alidai Kimomogolo. Alidai kuwa kosa hilo halipo kisheria kwa sababu maelezo hayo yanakiri kuwa taarifa ilitolewa saa 100 ambao ni muda unaotakiwa, hivyo maelezo ya kosa yanapishana yenyewe."


Shitaka la pili
linawakabili washitakiwa 18 isipokuwa mshitakiwa wa 19, Samson Mwigamba, ambalo wanashitakiwa kutotii amri halali ya polisi. Hapo pia hakuna sababu iliyoelezwa wala haikutajwa amri hiyo ni ipi waliyokataa kuitii, wakati sheria ya polisi kifungu 42, kifungu kidogo cha kwanza kinaeleza ni lazima amri inapotolewa imtaje aliyetoa order hiyo, kwa hapo haikutaja mtu aliyetoa amri hiyo," alidai na kuongeza: "Hapa alitakiwa kutajwa kama ni Polisi ni yupi na mwenye cheo gani, ingawa tunafahamu sheria inamtaka hakimu ndiye atoe tangazo la kuzuia maandamano na akishindwa basi RPC, baada ya kupewa kibali maalum na hakimu, na tukio hilo lilifanyika jirani na mahakama, hivyo hakukuwa na haja maagizo ya sheria kukiukwa kwa kutolewa amri hiyo na polisi wa kawaida."Aliendelea kudai kuwa kutokana na amri hiyo kutolewa na polisi wa vyeo vya chini wasiojulikana kisheria, hivyo kosa hilo halipo na limekufa na limepelekwa mahakamani hapo kwa kufikirika tu.


Katika kosa la tatu,
ambalo wanashitakiwa kufanya mkusanyiko usio halali, alidai kuwa kosa hilo halipo kisheria kwa sababu kwa mujibu wa Sheria ya Polisi kifungu cha 74 na 75 vya Kanuni ya Adhabu, kifungu cha 45 kinataka waseme walikusanyika eneo gani, lakini haikusema wapi, na walikuwa na lengo gani na kuongeza kuwa nalo ni la kufikirika tu. "Hapa wanadai maelezo ya kosa kuwa washitakiwa walikusanyika zaidi ya watatu katika Hoteli ya Mount Meru na hawakusema walikuwa eneo gani na amri ya kuwataka kutawanyika ilitolewa na nani? Hapa pia kosa halipo," alidai.


Kimomogolo alidai
polisi hawana mamlaka ya kuzuia maandamano wala kuzuia mkusanyiko, isipokuwa kazi yao ni kulinda amani na kuhakikisha hawasababishi madhara makubwa katika mkusanyiko. "Hapa sheria inasema Polisi kama wataalamu, walipaswa kutumia utaalamu wao kutumia busara ya kuruhusu mandamano ili yaende yalikopangwa, lakini pale walipotumia nguvu ya kuzuia kwa mabomu ya machozi na hapo walisababisha madhara makubwa, wakati wangetumia busara madhara yasingetokea," alidai Kimomogolo.


Shitaka la nne
nalo alilipinga kuwa halina nguvu za kisheria kwa sababu linawahusu washitakiwa 18 kutotii amri halali ya Polisi ya kuwataka kutawanyika, kwa kudai kuwa polisi hawakupaswa kuzuia maandamano hayo na kama ilibidi kufanya hivyo, angeenda ofisa wa polisi na kuzuia, tena kwa kupata ruhusa ya hakimu. Baada ya Kimomogolo kudai hivyo, hakimu nayesikiliza kesi hiyo, Charles Magesa, aliingilia kati na kusema kuwa mahakimu wapo wachache ambao hawazidi 11, halafu akacheka akamruhusu Kimomogolo kuendelea.


Kuhusu shitaka la sita na la tano
yanayowakabili Dk. Slaa na Ndesamburo, alidai kuwa pia limekosewa kisheria. Alidai shitaka hilo la kutoa lugha za uchochezi, sheria inataka itaje maneno hayo na kutajwa jamii iliyokwazika. "Hapo hakuna kitu kama hicho, hivyo nalo ni batili," alidai. Alidai kuwa sheria hiyo ya mwaka 1955 ilitungwa kwa ajili ya kuzuia wakoloni wasilete chokochoko za kisiasa wakati huo, lakini siyo sahihi kuitumia katika kosa hilo ambalo kimsingi, alidai ni la kufikirika.


Katika shitaka la saba
linalowakabili Ndesamburo, Dk. Slaa na Samson Mwigamba kwamba waliwachochea watu waliokusanyika eneo la viwanja vya NMC Januari 5, 2011 na kuwafanya watende kosa, alidai kuwa hapo napo hayakutajwa maneno hayo ya uchochezi hivyo kosa hilo kisheria limekosewa. Kuhusu shitaka la nane la washitakiwa wote 19 kukataa amri ya kutawanyika, Kimomogolo alidai kuwa kosa hilo kisheria halipo pia kwa sababu penye mkusanyiko wa watu wengi usitegemee kutoa amri ya kutawanyika halafu watu wakatawanyika kama barafu, ni lazima waongozane.


Kimomogolo alisema
kuna mikusanyiko miwili kisheria inaruhusiwa na kutambulika kama kusanyiko la kwanza la michezo, watu wa dini na jamii linaruhusiwa na halihitaji kibali cha polisi, lakini kusanyiko la pili la watu wa kisiasa na wengine wanahitaji kutoa taarifa polisi na hapo kama polisi hawatoridhika, pia hawaruhusiwi kusimamisha tu kienyeji, bali kwa utaratibu wa sheria ni hakimu au RPC aliyepewa kibali na hakimu. "Mheshimiwa Hakimu, naomba uyafutilie mbali makosa haya baada ya kupitia sheria, sababu tukiendelea hivi kila kukicha kesi, kesi, kazi hazitaendelea na maendeleo hayatakuja kwa mtindo huu wa kesi za kufikirika," alidai Kimomogolo.


Wakili wa Serikali , Edwin Kakolaki, akisaidiwa na Mwahija Ahmed, aliomba mahakama kumpatia muda wa kutosha kuyapitia mapingamizi hayo ambayo alidai ni mengi na yanahitaji muda wa kutosha ili awasilishe na akaahidi kuyawasilisha Jumatatu. Lakini kabla ya mapingamizi hizo kuwasilishwa, kulizuka utata wa kutaka kufahamu washitakiwa watatu, akiwemo Joseph Selasini ambaye hakufika kwa sababu ya kushughulikia miili ya mapadre waliofariki katika ajali. Wakili Kimomogolo, alidai kuwa Selasini ni kiongozi wa kanisa, hivyo analazimika kushiriki katika mipango ya kusafirisha miili ya mpadre hao.


Kuhusu washitakiwa wengine Dady Igogo na Nai Stephen, hakimu aliamuru wapatiwe taarifa kuhusu tarehe ya kesi wafike mahakamni hapo vinginevyo hatua kali za mahakama zitachukuliwa dhidi yao. Hakimu Magesa alisema hivyo kufuatia ombi la Wakili Kakolaki kutaka itolewe hati ya kukamatwa washitakiwa hao. Hakimu Magesa aliahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu upande wa mashitaka utakapoleta majibu ya mapingamizi ya utetezi.

IPPMedia

 
Hapa inaonekana kabisa wanasheria wa serikali hawana uelewa wa sheria

Malalamiko ya polisi kupindisha ukweli wa sheria ya maandamano umekuwa ukilalamikiwa kila mara tangu kipindi cha Mrema, CUF visiwani lakini hawabadiliki.

Nataka nione mahakama ya Arusha itachukua uamuzi gani juu ya hoja nzito nzito alizotohoa huyu mwanasheria mahiri Kimomogolo.
 
Aidha, amesema polisi hawana mamlaka ya kuzuia maandamano au mikusanyiko, isipokuwa ni hakimu pekee ndiye mwenye mamlaka ya kuzuia maandamano au kama hakimu imethibitika hayupo anaruhusiwa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa mkoa kuzuia maandamano hayo kwa kupewa maagizo na hakimu.

Hii imetulia
 
Polisi wengi hawana shule ni mafelia yaani kichwani ni weupe kabisa,ndio maana hawajui sheria zaidi ya kutumia mabavu.
 
Polisi wengi hawana shule ni mafelia yaani kichwani ni weupe kabisa,ndio maana hawajui sheria zaidi ya kutumia mabavu.

kweli kabisa! Waliowengi ni walikuwa watoro, drs hewa, mara nyingi hushinda kwenye MABANDA YA VIDEO. Polisi waliowengi ni vichwa maji. Dvs iv na 0.
 
Polisi wengi hawana shule ni mafelia yaani kichwani ni weupe kabisa,ndio maana hawajui sheria zaidi ya kutumia mabavu.

Kwenye kumbukumbu zangu polisi wengi ni wale walio na vyeti feki vya kuhitimu mashuleni, na badhi ni wale walioishia na daraja la 4 na 0. Utazamie nini kwa watu hawa? Hata walio viongozi wa juu jeshi la polisi ni hao hao wa division 0 na waliojitahidi ni division 4. Hawana reasoning bali force.
 
hivi tuna wanasheria serikalini au ni changa ya macho?

wanasheria wapo wengi tu na sheria wanasijua vizuri tu. Ila tatizo wanalazimika kufanya mambo mengine kisiasa zaidi. Sasa kama amri ya kusitisha maandamano inatolea na kiongozi wa kisaisa huwezi kutegemea sheria kufuatwa hapo.
 
wanasheria wapo wengi tu na sheria wanasijua vizuri tu. Ila tatizo wanalazimika kufanya mambo mengine kisiasa zaidi. Sasa kama amri ya kusitisha maandamano inatolea na kiongozi wa kisaisa huwezi kutegemea sheria kufuatwa hapo.

Ina maanisha jeshi la polisi halina determination katika utendaji wao wa kila siku? Sheria za utandaji wao ziko wazi iweje upenyezaji wa maagizo toka ikulu yawe na nguvu kuvunja sheria za nchi?
 
Hapa inaonekana kabisa wanasheria wa serikali hawana uelewa wa sheria

wana uelewa wa kisheria isipokuwa hawatekelezi taaluma yao ya sheria kwa makusudi. They are remotely controlled!
 
Huyu jamaa ni kichwa nimemkubali kama wanasheria wote wangekuwa hivi huenda tusingebambikiwa kesi.
 
Haki ya Mungu hata mimi sijasoma sheria lakin kwa maelezo hayo tuu nimeshaziona ni kesi za kufikirika kurudisha maendeleo nyuma na kupoteza muda wa watu....Ishahhlah tutafika tuu hata kupanda mlima mlima Kilimanjaro lazima kunakuteleza na kurudi nyuma,Hakuna mafanikio yasiyokuwa na magumu.:ballchain:
 
Hakika sasa wacha tuone uelewa wa kijana huyu Kalokola ni kipenzi sana cha DPP wa sasa .Naona katolewa Mwanza kuja Arusha sijui kapanda cheo kashuka maana alikuwa mwanasheria wa Kanda .Kazi ndiyo kwanza imeanza shame on them na sheria zao za kikoloni .
 
Haki ya Mungu hata mimi sijasoma sheria lakin kwa maelezo hayo tuu nimeshaziona ni kesi za kufikirika kurudisha maendeleo nyuma na kupoteza muda wa watu....Ishahhlah tutafika tuu hata kupanda mlima mlima Kilimanjaro lazima kunakuteleza na kurudi nyuma,Hakuna mafanikio yasiyokuwa na magumu.:ballchain:

Duuh! mie hilo bango tu! mbeya....... rais.....
 
Kumbeee???? hivi hamjui ni sasa tu ndio graduates wanaanza kuajiliwa Polisi na kwa kweli sio wengi na hasa upande wa sheria ni wachache sana. Wengi uomba kwenda polisi lakini wanavyowa treat kama wasio na elimu, utimka na kuachana na geshi la bolisi.
Viongozi polisi kwa sasa waliopo ni wale waliopata div 4 au 0 lakini walikuwa na bidii kuwatafutia wakubwa mademu tena maWP, ndio walio na vyeo na wanajifanya kujua sheria. ptuuuuu.
 
Polisi hawana mamlaka kuzuia maandamano ila mahakama - Kimongoro
Maafande wanazuia maandamo kwa kwenda mbele kila kona ya nchi mbona hakuna aliyewahi kupinga amri kama sio sheria?

CAP. 322 OF LAWS, Sect. 43(1)(2)

( 1 ) Any person who is desirous of convening, collecting, forming or organising any assembly or procession in any public place shall, not less than forty eight hours before the time when the assembly or procession is scheduled to take place, submit a written notification of his impending assembly or procession to the police officer in charge of the area

specifying–

(a) the place and time at which the meeting is to take place;
(b) the purpose in general of the meeting; and
(c) such other particulars as the Minister may from time to time, by
notice published in the Gazette, specify.

( 2 ) Where a person submits a notification in accordance with subsection (1), he may proceed to convene, collect, form or organise the assembly or procession in question as scheduled unless and until he receives an order from the Police Officer in charge of the area directing that the assembly or procession shall not be held as notified.
 
Maafande wanazuia maandamo kwa kwenda mbele kila kona ya nchi mbona hakuna aliyewahi kupinga amri kama sio sheria?

CAP. 322 OF LAWS, Sect. 43(1)(2)

( 1 ) Any person who is desirous of convening, collecting, forming or organising any assembly or procession in any public place shall, not less than forty eight hours before the time when the assembly or procession is scheduled to take place, submit a written notification of his impending assembly or procession to the police officer in charge of the area

specifying–

(a) the place and time at which the meeting is to take place;
(b) the purpose in general of the meeting; and
(c) such other particulars as the Minister may from time to time, by
notice published in the Gazette, specify.

( 2 ) Where a person submits a notification in accordance with subsection (1), he may proceed to convene, collect, form or organise the assembly or procession in question as scheduled unless and until he receives an order from the Police Officer in charge of the area directing that the assembly or procession shall not be held as notified.

Uamuzi wa wataalamu wa sheria huwa hawasimami katika kujenga utetezi kwa kifungu kimoja, kuna vifungu vingine umevuruka, umeweka kifungu hiki cha sheria tu kwa ajili ya kutetea hoja. Jaribu kutuwekea na vile vifungu ambavyo Kimomogolo alisema kifungu 42, 45, 74 na 75
 
Back
Top Bottom