Polisi: Hatumsaki Zitto kwa uchochezi

Polisi: Hatumsaki Zitto kwa uchochezi

Hivi adhabu ya kosa la kuwa na gari bila vibali halali ni muda gani jela, au faini kiasi gani au jela na fani vyote kwa pamoja? Halafu je, kuna uwezekano mkubwa wa hakimu/ jaji wa kesi ya namna hii kuchagua jela bila faini?
 
Polisi wanaisaidia TRA kuhakikisha kila kitu kipo sawa.
Kwa hiyo kama dereva yupo ni kwa nini wamtake mmiliki!? Mbona trafiki kila siku wanaandika hizo elfu 30 kwa wanayemkuta na gari!? Tukitaka kupiga hatua kama nchi ni lazima tuambiane ukweli, polisi kuweni wakweli hapa!
 
Kama ni hivyo ....basi anaweza tuma muwakilishi....mwenye power of attorney....akamuwakilisha kuleta vibali....sio lazima awe yy kufika in person ...muwakilishi anatosha..labda kama kuna jingine
 
Sijaona cha maana kwani kutokuwa na vibari ni kosa la dereva kuendesha gari lisilo na vibali na kama wanahitaji vibali sasa ulazima wa zito kupeleka uko wapi? na kama ni ishu ya kujua kama gari limelipiwa hakuna haja ya kulazimisha kuletwa kwa vibali kwani wanaweza kucheki online?. Na kama halikuwa na vibali waliachia la nini? inabidi taarifa zinazotolewa ziendane na uhalisia.
 
JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga limemtaka Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ajisalimilishe kwa kupeleka vibali kuondoa utata wa gari alilokuwa akilitumia katika kampeni za uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22, mwaka huu wilayani Kahama.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita, alisema kiongozi huyo anasakwa kutokana kuwapo taarifa za intelijensia zinazoeleza alikuwa akitumia gari hiyo ambayo haikuwa na vibali.

Mwita alisema jeshi hilo linamtaka Zitto apeleke taarifa kuhusu gari analomiliki aina ya Toyota Land Cruiser V8 ambalo hakulitaja namba za usajili.

“Siku ya kufunga mkutano wa kampeni uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Isagehe wilayani Kahama, tulipata taarifa kwamba Kabwe anatumia gari ambalo si halali, halina vibali.

“Tukawa tumefikiria tumpate baada ya mkutano atupe maelezo kuhusu gari analolimiliki, lakini kabla hata hatujaonana naye, alitoweka,” alisema Mwita.

Alisema Jeshi la Polisi linamtaka kiongozi huyo wa ACT Wazalendo apeleke vibali vya gari hilo.

“Kwa hiyo sisi mpaka sasa Kabwe tunamtaka atuletee vibali vya gari hilo na ndiyo kitu ambacho sisi tunamuhitaji.

“Baada ya kuona gari hilo linachukua muda mrefu kwetu tulimkabidhi dereva wa gari hilo na kumtaka amtafute bosi wake atuletee vibali vya gari hilo,” alisema.

Chanzo: Mtanzania
yeah right...
 
ZZK haya madubuasha yanakudanganya yanataka kukufanya kama lema!! kaa mbali na yule jamaa wa mto ngono
 
Mungu wangu. Gari ndilo lenye makosa, nandio ushahidi wenu. sasa unapoliachia unamaanisha nini?. Halafu unaendelea kumsaka zitto kwa gharama? hii si kweli. Na hivo vibali vingeletwa na mtu yoyote si lzm Zitto, na kama wasongeleta mgelilisizi. hii ni danganya toto.
 
Kuna watu 7 wamekufa katika sandarusi,hakuna anayejali

Kuna kesi hazina majibu hadi leo , hakuna anayejali

Ujambazi umetamalaki hadi walinzi wanavamiwa na kuuwa. Hakuna anayejali

Hivi kweli Taifa hili halina kazi za kufanya kiasi cha kukimbizana na vibali vya gari.!

Kuna umasikini uliojaa miongoni mwa wananchi.
Kuna mambo ya maendeleo yanataka fikra

Leo hatuwezi kujenga std , Kenya wanamaliza.

Halafu kuna watu hawalali wakikimbizana na kadi za magari ambazo hazina maana yoyote

Hizi ndizo dalili za kufeli ! Yaani kama vile hakuna kazi za kufanya kabisa

Mambo ya aibu kila asubuhi, wakimaliza wanapitisha bakuli kuomba pesa za ujenzi wa miundo mbinu

Aibu sana hii nchi! Dah!
 
Salary Slip. Mkuu samahani lakini , hivi Tra Si ndio wanahusika na vibari vya gari?
Police kazi yao Si kukamata na kuwaachia TRA washughulikie?
 
Tuliambiwa kuwa nchi hii ni tajiri hawaitaji msaada kutoka kokote, cha ajabu nimeshangaa mtukufu juzi kati kuomba msaada pamoja na mkopo kutoka Uturuki!
 
Kama walilikamata gari, kwa nini hawakuwaomba Tra wawape maelezo yote kuhusu hilo gari kupitia namba za usajiri? au halikuwa na namba za usajiri? Polisi wetu mmhh!
Shida sio gari ni ZZK,kamanda anajichanganya,wanakawida ya kusema uchunguzi unaendelea wakiwashikilia watu na mali mbali mbali,dereva aliwapa vielelezo in a mana vilikuwa sahihi ndio sababu ya kumuachia,kama sio sahihi bad mnamashaka mlimuachia vipi,iwapo akajitokeza mtu leo akasema nimepotelewa na gari akitaja sifa za ilo gari amuoni kama policcm ni wazembe,mmekishika kizbit bado mnamashaka nacho,mnakiachia kweli nyie ni polisi au vituko,kama kweli wameliachia kwa misingi iyo uyo policcm nina mashaka na uwezo wake kikazi,la msingi waseme shida sio gari ila ni ZZK kuna maagizo toka juu.
 
Kuna gar dar lina platen number za hapa kazi tu. Ila vibali vime-expire
 
Back
Top Bottom