Polisi: Hatumsaki Zitto kwa uchochezi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,843
JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga limemtaka Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ajisalimilishe kwa kupeleka vibali kuondoa utata wa gari alilokuwa akilitumia katika kampeni za uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22, mwaka huu wilayani Kahama.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita, alisema kiongozi huyo anasakwa kutokana kuwapo taarifa za intelijensia zinazoeleza alikuwa akitumia gari hiyo ambayo haikuwa na vibali.

Mwita alisema jeshi hilo linamtaka Zitto apeleke taarifa kuhusu gari analomiliki aina ya Toyota Land Cruiser V8 ambalo hakulitaja namba za usajili.

“Siku ya kufunga mkutano wa kampeni uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Isagehe wilayani Kahama, tulipata taarifa kwamba Kabwe anatumia gari ambalo si halali, halina vibali.

“Tukawa tumefikiria tumpate baada ya mkutano atupe maelezo kuhusu gari analolimiliki, lakini kabla hata hatujaonana naye, alitoweka,” alisema Mwita.

Alisema Jeshi la Polisi linamtaka kiongozi huyo wa ACT Wazalendo apeleke vibali vya gari hilo.

“Kwa hiyo sisi mpaka sasa Kabwe tunamtaka atuletee vibali vya gari hilo na ndiyo kitu ambacho sisi tunamuhitaji.

“Baada ya kuona gari hilo linachukua muda mrefu kwetu tulimkabidhi dereva wa gari hilo na kumtaka amtafute bosi wake atuletee vibali vya gari hilo,” alisema.

Chanzo: Mtanzania
 
Heee..!

Na hilo gari lenye shida ya vibali mmeshaliachia kumbe..!??

I doubt kama hilo gari lina shida yoyote ya vibali...
Mbona mmeliachia??

Si ndio kosa lilipo..?? Unaliachia vipi gari.

Shida inaweza kuwa mlikuwa mnamtafuta ZZK kutokana na hotuba yake kwenye huu mkutano.. Au ndio mlikuwa mnahakikisha ulinzi wake kama wa Lowassa kule Geita??

Jeshi hili liache kutumika jamani.

Mnajidhalilisha sana kwa kweli.
 
Jeshi la policcm ,mahakama ccm sasa hivi vinatafuta vyeo vya kujipendekeza kutoka kwa dikteta uchwara,siku vyama vingi vikitoweka mtamfunga nani na kumkamata nani ?kwasabbu kwa ccm hata balozi hamna ubavu wa kumkamata balozi wa nyumba kumi.
 
Taarifa hii ndo ipo kichochezi, kweli mtanzania halikuhoji yafuatayo!
1. Kwa hiyo alitoweka akaliacha gari?
2. Dereva walimkamata akiwa na gari ama wapi?
3. Wamemwachia kazi Dereva kumtafuta Zitto wao wafanye kazi gani?
3. Kama walilikamata gari na Dereva, kwa kumuachia Dereva, gari nalo wamemwachia?
Ndo, maana nikasema, taarifa hii ndio imekaa kichochezi!
 
Kwanini wasimkamate dereva ambaye ndiyo yuko na gari mpaka wamtafute Zitto ambaye siyo dereva? hapa kuna jambo limejificha.
 
Heee..!

Na hilo gari lenye shida ya vibali mmeshaliachia kumbe..!??

I doubt kama hilo gari lina shida yoyote ya vibali...
Mbona mmeliachia??

Si ndio kosa lilipo..?? Unaliachia vipi gari.

Shida inaweza kuwa mlikuwa mnamtafuta ZZK kutokana na hotuba yake kwenye huu mkutano.. Au ndio mlikuwa mnahakikisha ulinzi wake kama wa Lowassa kule Geita??

Jeshi hili liache kutumika jamani.

Mnajidhalilisha sana kwa kweli.
Maadili ya kazi sio dili tena.
 
Kama lilikua swala LA vibali kulikua na haja gani ya kwenda na magari zaidi ya 4 yaliyojaa polisi waliojihami tena kwa siraha Kali?
Walishindwa nini kumpelekea wito tu kwa ajili ya mahojiano nae hadi wapeleke jeshi lilojihami?
Acheni usanii kwa kupenda vyeo kutoka kwa malaika mtukufu kwa kutenda maovu dhidi ya raia
 
Back
Top Bottom