Polisi: Hatumsaki Zitto kwa uchochezi

Polisi: Hatumsaki Zitto kwa uchochezi

wangapi tunaendesha magari hayana vibali lakini tunadunda mtaani ...polisi kutumika ni dhambi kubwa sana.
 
Tz. Ni nchi ya pekee ktk sayari ya Tatu yaani Dunia iliyojaa maajabu.
Intelijensia ya gari lisilo na vibali ila hakuna intelijensia ya Vifo vya ajabu vya watu kule ruvu,kupotea kwa Ben n.k.n.k
Inatia hasira sana Taifa hili,concentration for useless thns than positive thns so miserable for sure if politics involve all matters and all govt sectors with officials.
 
Zitto alishawahi kusema hamuogopi Magufuli anamuogopa Mungu tu,leo hii kajificha Bujumbura
Na kwa nini Rais aogopwe..tumechagua kwa kura nyingi ili atuhudumie sio kutishia MTU hata kama hajamchagua. Najua hakuna anayetishiwa na Mh. RAIS anafanya kazi kwa Sheria na Katiba kama Muongozo. Sipendi aogopewe Bali aheshimiwe na nadhani mwenyewe anapenda iwe hivyo.
 
ukipanda gari tuu ni lako ulete vibali je kama aliazima huko iweje mseme gari la zitto na kama umiliki wa gari una utata TRA si ndio kazi yao wanachukua gari mpaka ukamilishe karatasi hapo Police sijawaelewa kabisa ongeeni ukweli..
 
Heee..!

Na hilo gari lenye shida ya vibali mmeshaliachia kumbe..!??

I doubt kama hilo gari lina shida yoyote ya vibali...
Mbona mmeliachia??

Si ndio kosa lilipo..?? Unaliachia vipi gari.

Shida inaweza kuwa mlikuwa mnamtafuta ZZK kutokana na hotuba yake kwenye huu mkutano.. Au ndio mlikuwa mnahakikisha ulinzi wake kama wa Lowassa kule Geita??

Jeshi hili liache kutumika jamani.

Mnajidhalilisha sana kwa kweli.
Polisi wanasahau kwamba ni raia!
 
Uwongo nao ukizidi sana unakuwa na madhara Kwa taifa sijawahi ona Gari linakamatwa Kwa Makosa mwisho wa siku mmiliki asipopatikana anatafutwa dereva anapewa Gari akamtafute mmiliki?? Haya mambo yanapatikana Tanzania tu
 
JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga limemtaka Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ajisalimilishe kwa kupeleka vibali kuondoa utata wa gari alilokuwa akilitumia katika kampeni za uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22, mwaka huu wilayani Kahama.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita, alisema kiongozi huyo anasakwa kutokana kuwapo taarifa za intelijensia zinazoeleza alikuwa akitumia gari hiyo ambayo haikuwa na vibali.

Mwita alisema jeshi hilo linamtaka Zitto apeleke taarifa kuhusu gari analomiliki aina ya Toyota Land Cruiser V8 ambalo hakulitaja namba za usajili.

“Siku ya kufunga mkutano wa kampeni uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Isagehe wilayani Kahama, tulipata taarifa kwamba Kabwe anatumia gari ambalo si halali, halina vibali.

“Tukawa tumefikiria tumpate baada ya mkutano atupe maelezo kuhusu gari analolimiliki, lakini kabla hata hatujaonana naye, alitoweka,” alisema Mwita.

Alisema Jeshi la Polisi linamtaka kiongozi huyo wa ACT Wazalendo apeleke vibali vya gari hilo.

“Kwa hiyo sisi mpaka sasa Kabwe tunamtaka atuletee vibali vya gari hilo na ndiyo kitu ambacho sisi tunamuhitaji.

“Baada ya kuona gari hilo linachukua muda mrefu kwetu tulimkabidhi dereva wa gari hilo na kumtaka amtafute bosi wake atuletee vibali vya gari hilo,” alisema.


Chanzo: Mtanzania
Eti samahani jamani nikicheka naweza kuitwa mchochezi?[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Sasa mbona wamemkabidhi huyo dereva kama halina vibali?
 
Gari lina vibali tata, umelikamata, mwenyewe haonekani unaliachia kabla ya kuviona vibali vyake ujiridhishe, unaliachia kwanini?! Mwanzo wa series nyingine huu?!
 
Back
Top Bottom