Polisi: Hatumsaki Zitto kwa uchochezi

Polisi: Hatumsaki Zitto kwa uchochezi

Taarifa hii ndo ipo kichochezi, kweli mtanzania halikuhoji yafuatayo!
1. Kwa hiyo alitoweka akaliacha gari?
2. Dereva walimkamata akiwa na gari ama wapi?
3. Wamemwachia kazi Dereva kumtafuta Zitto wao wafanye kazi gani?
3. Kama walilikamata gari na Dereva, kwa kumuachia Dereva, gari nalo wamemwachia?
Ndo, maana nikasema, taarifa hii ndio imekaa kichochezi!
Hizo ndio habari zinazotakiwa nowdays, marufuku kutumia zile 5W kwenye kazi ya uandishi. Andika utakaloambiwa.PERIOD
 
JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga limemtaka Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ajisalimilishe kwa kupeleka vibali kuondoa utata wa gari alilokuwa akilitumia katika kampeni za uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22, mwaka huu wilayani Kahama.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita, alisema kiongozi huyo anasakwa kutokana kuwapo taarifa za intelijensia zinazoeleza alikuwa akitumia gari hiyo ambayo haikuwa na vibali.

Mwita alisema jeshi hilo linamtaka Zitto apeleke taarifa kuhusu gari analomiliki aina ya Toyota Land Cruiser V8 ambalo hakulitaja namba za usajili.

“Siku ya kufunga mkutano wa kampeni uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Isagehe wilayani Kahama, tulipata taarifa kwamba Kabwe anatumia gari ambalo si halali, halina vibali.

“Tukawa tumefikiria tumpate baada ya mkutano atupe maelezo kuhusu gari analolimiliki, lakini kabla hata hatujaonana naye, alitoweka,” alisema Mwita.

Alisema Jeshi la Polisi linamtaka kiongozi huyo wa ACT Wazalendo apeleke vibali vya gari hilo.

“Kwa hiyo sisi mpaka sasa Kabwe tunamtaka atuletee vibali vya gari hilo na ndiyo kitu ambacho sisi tunamuhitaji.

“Baada ya kuona gari hilo linachukua muda mrefu kwetu tulimkabidhi dereva wa gari hilo na kumtaka amtafute bosi wake atuletee vibali vya gari hilo,” alisema.


Chanzo: Mtanzania
Sikiliza kauli hii ya dereva juu ya kukamatwa kwa gari la Zitto.
Dereva wa Zitto Kabwe aongea baada ya kukamatwa na Polisi - millardayo.com
 
Gari lina vibali tata, umelikamata, mwenyewe haonekani unaliachia kabla ya kuviona vibali vyake ujiridhishe, unaliachia kwanini?! Mwanzo wa series nyingine huu?!
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Heee..!

Na hilo gari lenye shida ya vibali mmeshaliachia kumbe..!??

I doubt kama hilo gari lina shida yoyote ya vibali...
Mbona mmeliachia??

Si ndio kosa lilipo..?? Unaliachia vipi gari.

Shida inaweza kuwa mlikuwa mnamtafuta ZZK kutokana na hotuba yake kwenye huu mkutano.. Au ndio mlikuwa mnahakikisha ulinzi wake kama wa Lowassa kule Geita??

Jeshi hili liache kutumika jamani.

Mnajidhalilisha sana kwa kweli.
 
Si mngemtuma hyo hyo dereva akelete vibali badala ya zitto
 
Pumbavu kabisa,umewai kumiliki gari wewe,uliwai kusikia wapi mtu akitaka kununua gari polisi wanausika,iyo itakuwa bunduki,icho unachokiongelea ni baada ya gari kuanza kutumika,ni usalama wa gari,kuwa linakidhi utaratibu wa kutumika sio umiliki,iwapo mtu akanunua gari akaliweka gerage ao traffic vehicle inspection watakuja huko,kama watakuja ni kupekua kama wanaisi la wizi au la magumashi,hapa patakuwa na documents za TRA na wauzaji tu sio za polisi.
 
Pumbavu kabisa,umewai kumiliki gari wewe,uliwai kusikia wapi mtu akitaka kununua gari polisi wanausika,iyo itakuwa bunduki,icho unachokiongelea ni baada ya gari kuanza kutumika,ni usalama wa gari,kuwa linakidhi utaratibu wa kutumika sio umiliki,iwapo mtu akanunua gari akaliweka gerage ao traffic vehicle inspection watakuja huko,kama watakuja ni kupekua kama wanaisi la wizi au la magumashi,hapa patakuwa na documents za TRA na wauzaji tu sio za polisi.
 
Polisi wenyewe wanalipwa mshahara MBUZI sana na hawa watawala wanao walamba viatu vyao
Anajichanganya tu hapa huyu kaimu RC
Kama gari lina matatizo ya usajili kwa nn mliliachia?
Polisi ni TRA siku hizi?
Puuzi kabisa!
 
Upimbi kabisa, eti tunamsaka kutokana na taarifa za kiintelijensia kuwa gari analolitumia halina vibali halali....hivi kujua uhalali wa vibali vya gari unahitaji intelijensia???? Idiot
 
Kama ni hivyo ....basi anaweza tuma muwakilishi....mwenye power of attorney....akamuwakilisha kuleta vibali....sio lazima awe yy kufika in person ...muwakilishi anatosha..labda kama kuna jingine

Yeye Mwenyewe anaogopa nini?
 
Back
Top Bottom