Polisi haisamini wasomi vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi haisamini wasomi vijana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ACTIVISTA, Aug 22, 2011.

 1. A

  ACTIVISTA Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi hii ni ya ajabu, yaani kijana kajipinda kasoma ili ajikombee yeye na jamii yake lakini hasaminiwi... huwezi amini vijana wanomaliza vyuo vikuu na kujiunga na jeshi la polisi wanaanza bila cheo hata mbavu moja... na pia majukumu yao ya kazi ni tofauti kabisa na fani wlizosomea... uwe muhasibu, dokta.. nk..

  Utalinda kwa ocd, utazungushwa doria, na kazi zote za hovyo zinazoidharilisha elimu yako,,,, msomi aliye maliza chuo akajiunga na polisi hatamani kukutana na ndugu au rafiki akiwa na uniform coz ni aibu kazi anayofanya.... hailingani na elimu yake wala ujuzi wake... huku ni kutesa vijana waoipenda nchi yao na jeshi la polisi.... naipenda polisi, polisi naomba iliangalie hili.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Labda wanawazungusha kulinda kwa OCD, kwa RCO, kwa RPC, kwenye mabenki na nyumbani kwa viongozi wengine wa serikali ili kuwatengeneza vizuri zaidi, hii tuiite kama "internship" baada ya kumaliza huo mzunguko wa internship sasa mnaweza kuarudishwa kutumika fani zenu.

  Hilki la kutoanza na cheo ni kawaida kwa majeshi yote, isipokuwa majeshi mengine yanakuwa na utaratibu mzuri kwamba baada ya muda mfupi tangu kumaliza mafunzo ya awali wanapelekwa vyuoni(vyuo vya kijeshi) kwa ajili ya mafunzo zaidi na hatimaye wanapata vyeo. Kama polisi hawana utaratibu kama huo, basi hapo kuna utata.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona na wewe huthamini Kiswahili!!!

  Kwa hiyo mkuu ulitaka mtu akitoka na Degree basi awe Inspector (Mrakibu wa Polisi)? Hivi vyombo vya ulinzi na usalama nadhani vina taratibu zake za kikazi huwezi kutoka tu na kuchukua jicheo; kuna mchakato. Inabidi upitie huo mchakato na baadaye utapata tu cheo.


  Nafahamu kuwa watu wenye degree wakijiunga na jeshi wanapata uluteni usu na baada ya muda tu wanapata uluteni kamili lakini lazima waende monduli wakautafute huo uluteni hauji tu kwenye sahani ya dhahabu.

  Kuna rafiki yangu alimaliza degree yake akajiunga na JWTZ lakini akaogopa kwenda monduli aliiishia kuwa mwanajeshi asiye na cheo hadi leo ndio amepata ukoplo ili hali wenzake aliokuwa nao chuoni na kujiunga nao jeshini wengine ni mameja!!! Mkuu mchakato jeshini ni muhimu.
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,958
  Likes Received: 23,634
  Trophy Points: 280
  Kusamini maana yake nini? "kudhamini" au "kuthamini"
   
 5. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  We unaonekana ni polisi uliyeenda chuoni kwa matarajio kwamba ukirudi kazini utakuwa umeshaula. Umejidanganya kwasababu utaratibu ni tofauti sana, unatakiwa ufanye kazi za kulinda mpaka ipite miaka mitatu ndiyo ufikiriwe kupandishwa cheo. Chapa kazi bwana mdogo wenzako tumesota sana mpaka tumefika hapa tulipo.
   
 6. NAIPENDA TANZAN

  NAIPENDA TANZAN Member

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kafanye kazi ya fani yako. Kazi ya police ni kulinda raia na mali zao, hawana hospital wala mashamba. Unapokuwa police fani yako no ulinzi, hii haijalishi unalinda benki, sokoni, kwa RPC, OCD au hata kwa mlalahoi yeyote, kazi yako ni kulinda na kuhakikisha kile unacho kilinda kinabaki salama. Huwezi hiyo achana nayo.
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hasira za graduate kupelekwa guard kwa OCD mkuu usimlaumu sana. Una ushauri gani kwa huyu Inspector mtarajiwa.
   
 8. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Anataka cheo wakati hata shule hakufanya vizuri, graduate mzima unaandika samini badala ya thamini, halafu sikuwa nimejua kumbe polisi kuna kazi zingine ni za hovyo, hii ina maana gani sijui. Nina mashaka na attitude ya mtoa mada.
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Samani maana yake ni furniture.

  Ulitakiwa useme Thaminiwa.

  Hii inaonyesha kuwa kijana hukupita JKT. na kama ungepita JKT basi usingekurupuka na kulalama kwa hilo.

  Unatakiwa ujuwe kuwa kiongozi mzuri ni yule aliyepitia ngazi zote yaani kuanzia ukuruta kisha kupanda mpaka ofisa. Sasa hata akiwa kiongozi basi anajua makuruta kule angani wanazungumza na kuishi vipi na hata namna wanavyoweza kujongo kazi. Huyo ndio ofisa mzuri.

  kama watakuwa na utaratibu huo basi ni mzuri sana kwa viongozi ambao ni maofisa kujua makuruta or NCOs wanaishi vipi ili waweze kuwa manage vizuri.
   
 10. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Si ajabu mheshimiwa graduate anakuwa korokoroni wa OCD aliyemaliza darasa la nane la enzi hizo patamu hapo.
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Kulinda ni jukumu la polisi sasa mkuu yeye hataki kulinda anataka akae ofisini tu!!! Usione watu tunavaa magwanda yamelundikwa nishani na mawe tumepitia hatua hizohizo mkuu. Jeshini uvumilivu, utii na heshima ndio silaha. Sasa kama wewe unaanza kunung'unika hivi sasa usitegemee kupata kitu huko.
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwani kazi nyingine hakuna????wewe umemaliza chuo una shahada unakimbilia UPOLISI,DAH
   
 15. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  People want to go to heaven,,but none of them want to die,, mkuu haiwezekani vile tu ni graduate utoke recruit (ccp) moshi na kuanza na cheo lazima usote (kupitia mchakato) kwa maana ya kujifunza kazi kutoka kwenye roots. Be eager to learn uonyeshe thamani halisi ya kusoma kwako before you start climbing ladders
   
 16. k

  king11 JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bado wanatumia mifumo ya kale nchi zote zimeshatoka huko na wanatumia mfumo wa kurusha vyeo watu wenye elimu kwani si kitu cha ajabu kuona mtu mwenye masters akipewa cheo kikubwa kwani uwezo wa utawala tayari anao na vyeo vikubwa jeshini vinaitaji uwezo wa utawala
   
 17. T

  The Priest JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Jeshi la wananchi,graduate akitoka recruit,anaunganisha Monduli kule akimaliza 9 months,anapewa nyota 2(leutenant)while police akitoka ccp anaanza na kuwa constable for three years!why that difference?
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mgawanyo wa kazi huo!
   
 19. A

  ACID Member

  #19
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NDUGU,pamoja na kwamba unatakiwa uvumilivu...ila huku polisi kinachoharibu zaid ni uwezo wa kuongoza kwa viongoz wao! mtu kama mwema,alitakiwa awe shekh,pia mwema alishakuwa raia alipokwenda interpol..kwahyo kumpa jeshi ni sawa kumpa bata mayai ya kuku atotoe vifaranga!
   
 20. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamani kazi hakuna, graduate kibao wanazunguka na Bahasha posta,viatu vimeisha upande mmoja.Nafasi 100 applicant 7000 .KAKA KUWA MVUMILIVU VYEO VINAKUJA .
   
Loading...