Polisi haisamini wasomi vijana

Kulinda ni jukumu la polisi sasa mkuu yeye hataki kulinda anataka akae ofisini tu!!! Usione watu tunavaa magwanda yamelundikwa nishani na mawe tumepitia hatua hizohizo mkuu. Jeshini uvumilivu, utii na heshima ndio silaha. Sasa kama wewe unaanza kunung'unika hivi sasa usitegemee kupata kitu huko.

Bila shaka mkuu hiyo avatar yako inakuwakilisha majukumu yako kama ulivyosema.

If that is the case, nadhani unaweza kumpa ushauri mzuri sana huyu askari mwenzako.

BTW, hivi hakuna kazi ya kiaskari inayoweza kufanywa na mtu akiwa amekaa ofisini na kufaidi kiyoyozi?
 
Do they add any value kwa kuwa wasomi vijana?
Kama rushwa wanaongoza bado, kubambikia kesi na kushindwa upepelezi kwa wakati
 
da pole sana kwa jeshi la polisi haiko hivo kwanza lazima uzunguke vitengio vyote na kuvifanyia kazi,pia ikumbukwe kuwa kazi ya msingi ya jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zake,katika hili ndo suala la kuzuia makosa yasitendeke ndo linachukua mkondo! Na hili hufanywa kwa kwenda doria,ulinzi maeneo mbalimbali zikiwemo bank,kuweka vizuizi na kuvamia maeneo mbalimbali yenye uhalifu (raid). huwezi ukahitimu leo na kupewa cheo cha ukaguzi,cheo si zawadi,timiza kwanza wajibu ndo upate haki yako hiyo! Pia sometime kazi hizi za polisi ni wito,si lazima kujilinganisha na kazi zingine!
 
bado wanatumia mifumo ya kale nchi zote zimeshatoka huko na wanatumia mfumo wa kurusha vyeo watu wenye elimu kwani si kitu cha ajabu kuona mtu mwenye masters akipewa cheo kikubwa kwani uwezo wa utawala tayari anao na vyeo vikubwa jeshini vinaitaji uwezo wa utawala

andika vinahitaji na sio vinaitaji
 
Kila idara ina vigezo na taratibu zake za kupandisha vyeo watumishi wake.Ni maoni yangu kuwa Polisi kama Idara zingine za serikali ina taratibu na vingezo vingi ikiwa ni pamoja na elimu,si dhani kama ni sahihi kama kila mwenye elimu kubwa anastahili kupandishwa cheo hata kama utendaji kazi wake hauridhishi.Mfano mlevi,mla rushwa, hafati ratiba za kazi,n.k.Binafsi nimebahatika kufanya kazi serikalini idara nyingi tofauti kwa kweli nilibaini vyeo wanapewa watu wasomi ambao pia ni waadilifu,wapenda haki na wachapa kazi hasa kwa sababu cheo hupelekea mtu kupata wadhifa na madaraka kama RPC,RTO,RCO AU ktk idara zingine DSO,DEO,MENEJA,MKURUNGEZI n.k.Hivyo Inatupasa kuwa wazalendo wote waajiri na waajiriwa kwa kufuata misingi yote ya kazi ktk idara.Jamani nani hajui kuwa kuna wasomi ktk utumishi wa umma utendaji kazi wao ni mbuvu?Je, wapandishwe cheo na kupewa madaraka kwa kuwa ni wasomi,japo ni walarushwa, wabadhilifu wa mali ya umma, wazembe na walevi kazini?Binafsi nashauri ni vyema vigezo vyote vifuatwe kupanaisha vyeo kwa watumishi wote wa umma ikiwa ni pamoja na elimu.
 
Back
Top Bottom