Nimetokea maeneo ya Njiro kuja town kupitia Keep-Left ya Impala, kuingia hadi Clock tower (Arusha hotel) hadi CRDB friends corner kuelekea stendi kuu ya mabasi, sikufanikia kuona Police-Traffic hata mmoja!
wanaogopa kusimama barabarani.
Nimekutana na Deffender zaidi ya Tano zenye polisi wenye sillaha nzito nzito, Mbwa, na mabomu ya machozi.
Nikashuka kuingia ATM ya CRDB pale maeneo ya Friends kona, nikakuta maafisa Usalama wa Taifa zaidi ya watatu wakiwa na Com-Sets zao masikioni, na wengine na radio-calls ndogondogo, wakiwa very busy kutoa report!
Kwa kweli hali si shwari hapa Arusha.
Nimepitia hadi Viwanga vya nmc, hakuna yeyote pale! kuna mabaki ya mipira iliyochomwa jana, na kuni ambazo watu waliota jana usiku.
It is real PIPOZ PAWA!
I SUBMIT WAUNGWANA!