Polisi: Bodaboda msizidishe abiria zaidi ya mmoja

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,791
218,420
Taarifa ya Jeshi la Polisi limewataka waendesha bodaboda kutopakia abiria zaidi ya mmoja (mishikaki) kama alivyosema Kinana kwenye mikutano ya ccm , na badala yake waendelee kufuata utaratibu wa zamani .

Taarifa yao hii hapa .

Screenshot_2023-07-28-23-05-57-1.jpg

Jeshi la polisi limesema limeendelea kupokea maswali toka kwa Wanahabari na Wananchi wa kada mbalimbali kufuatia matamshi ya Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara aliyoyatoa tarehe 27/07/2023 huko Bariadi Mkoa wa Simiyu kwamba watazungumza na kuishauri Serikali katika kupitisha sheria Bodaboda wabebe Watu zaidi ya mmoja.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema “Wote wanaotupigia simu wanataka kujua nini msimamo wa Jeshi la Polisi, kimsingi Jeshi la Polisi ni Wasimamizi wa sheria zilizotungwa na Bunge letu tukufu miongoni mwa sheria hizo ikiwa ni kifungu namba 59 cha Sheria ya Usalama Barabarani Sura 168 ambacho kinakataza pikipiki kubeba abiria zaidi ya mmoja”

“Hata hivyo Kinana hakusema bodaboda wapakie abiria zaidi ya mmoja bali 'wataenda kushauri' hivyo tunawaelekeza bodaboda wafuate sheria iliyopo kwa sasa ambayo tunaisimamia yene katazo hilo na endapo ushauri utakaotolewa utakubalika na sheria kubadilishwa basi tutasimamia sheria ya wakati huo, kwa sasa sheria ya kutopakia abiria zaidi ya mmoja iendelee kufuatwa na kuzingatiwa ipasavyo, hii itatusaidia sote kuendelea kuwa salama tunapotumia barabara”.

Pia soma:
- Kinana kuongea na mamlaka bodaboda wabebe abiria zaidi ya 1 (mshikaki)
 
Back
Top Bottom