Polisi atinga disko akiwa na SMG | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi atinga disko akiwa na SMG

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Mar 2, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Polisi atinga disko akiwa na SMG
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 01 March 2012 21:01 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Daniel Mjema,Moshi
  POLISI mkoani Kilimanjaro wanamshikilia mmoja wa askari wake (jina tunalihifadhi kwa sasa) kwa tuhuma za kutoroka lindo, kisha kwenda klabu ya usiku mjini Moshi akiwa na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) usiku wa kuamkia jana.

  Kitendo hicho kilisababisha mtafaruku katika klabu ya Pub Alberto baada ya meneja wa klabu hiyo kumkuta askari huyo akiingia ndani kupitia lango kubwa usiku wa manane, akiwa na silaha hiyo ya kivita.

  Meneja wa ukumbi huo, Thadeus Kimaro alithibitisha tukio hilo na kusema alikutana na polisi huyo akiwa na bunduki hiyo aina ya SMG akitaka kuingia ukumbini humo kupitia lango kuu, kwa kuwa mlango wa kuingilia wateja tayari ulikuwa umefungwa.

  “Wakati natokea Cool bar muda wa saa 9:00 usiku, nilikutana na mtu aliyetaka kuingia na bunduki huku akitweta na akisema kuna mtu amemuudhi ndani na alitaka kumuonyesha,”alisimulia Kimaro.

  Meneja huyo alisema wakati huo tayari muda wa kuingia wateja ulikuwa umepita na hivyo, mlango kufungwa na kuachwa lango kuu ili wateja waliobaki watoke.

  Taarifa zaidi zilisema askari huyo aliyekuwa katika lindo kwenye kituo kikuu cha mkoa, aliondoka lindoni akiwa na silaha hiyo iliyokuwa na risasi 30 ndani yake.

  Inadaiwa kuwa awali polisi huyo alifika eneo la klabu hiyo akiwa kwenye gari binafsi na alikuwa ameongozana na wenzake watatu, lakini kabla ya kuingia ukumbini alibadili sare za kazi na kuziacha kwenye gari pamoja na silaha.

  Muda kidogo baada ya kuingia ndani, alilikorofishana na mmoja wa watu waliokuwa ukumbini hapo, hivyo kuamua kwenda kwenye gari kuchukua silaha kwa malengo ambayo hayakufahamika mara moja, lakini alikutana na meneja huyo akiwa na walinzi ambao walimzuia asiingie ndani.

  Meneja huyo alisema, akishirikiana na walinzi, walimsihi na kumwelewesha kuwa isingekuwa vyema kuingia na silaha kwa kuwa haziruhusiwi ndani ya ukumbi. Aliridhika kwa shingo upande na kurudisha silaha kwenye gari.

  "Kama angefanikiwa kuingia ndani ya ukumbi na silaha hiyo nahisi maafa yangekuwa ni makubwa, kwa kuwa kwa uelewa wangu SMG inabeba risasi 30," alisema Meneja huyo.

  Kauli ya RPC
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma alisema askari huyo alikamatwa muda mfupi tu baada ya baada ya polisi kupewa taarifa hizo.

  “Taarifa zilivyokuja kulikuwa na hisia kwamba inawezekana ni majambazi, kwa hiyo polisi walipofika pale na kuzingira lile gari ndipo tulipobaini kuwa ni askari, lakini wakati huo hakuwa katika sare zake, alikuwa amevaa kiraia,”alisema Mwakyoma.

  Kamanda Mwakyoma alifafanua kwamba, baada ya polisi kupekua gari hilo walikuta sare za askari huyo na bunduki hiyo na kwamba alikuwa hajairudisha kwa vile bado alitakiwa kuwa lindoni.

  “Tunaye hapa lock up (mahabusu) maana tulimkamata hiyo saa 9:00 usiku na mchakato wa kumfungulia mashitaka ya kijeshi unaendelea kwa sababu wakati huo, bado alipaswa awe lindo kituo cha kati, lakini akatoroka kwenda kucheza disko,”alisema Mwakyoma.

  Mwaka 2007, wakili mmoja wa kujitegemea wa jijini Arusha aliwahi kuingia na bastola katika ukumbi huo na kufyatua risasi hali iliyoulazimu uongozi wa klabu hiyo kuweka mashine ya kukagua silaha kabla ya wateja kuingia ukumbini[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Duh, ilikuwa hatari! watu wengine bwana! Sasa si bora angewaachia wenzake mtutu akaenda kucheza hadi mishale ya asubuhi then anarudi lindoni!
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  na kwenye lindo wangeiba ingekuaje?
   
 4. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Za mwizi arobaini,
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ile Disco haikuwa na MABAUNSA?
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Polisi wetu wengi elimu ya uraia hawana.
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Wewe! Baunsa aende wakati mtu ana SMG yenye risasi 30 na magazin ya akiba nayo risasi 30! Hata komandoo kipensi angelala mbele alaaa!
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mnaongelea elimu gani wakati mtu ana hasira?
  Hamsikii matukio kadha hawa jamaa wanajifumua vichwa kwa hizohizo silaha?
  Mtu akighafilika haijalishi kasoma au mweupe!
   
 9. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Polisi wa siku hizi hovyo sana,..kuna polisi hapa arusha central alikuwa(thanks God walimshtukia) anaendesha kituo/jiji akiwa club na radio call....i.e afande chacha nenda kaloreni kuna vurugu hapo, mara nendeni ........anyway ndio polisi wetu hao
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Kama walivyo wafuasi wengi wa CCM_hawana elimu ya uzalendo/uraia.
   
 11. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Itakuwa jamaa aliibiwa demu wake.
   
 12. P

  PAFKI Senior Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45

  hata kidogo ww anaijua smg au anaisikia? Ione pale jamaa kaishika tu ni balaaa!!!
   
 13. m

  mzawahalisi JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Niuzembe na kuchukulia poa. Pia inaonyesha hakuna ufatiliaji wa askari malindoni. Haya huyo kaenda nayo disco, wangapi wanaendanazo kwenye ujambazi?
  Mungu uturehemu na mabalaa haya.
   
 14. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hivi huyo polisi alikuwa anafikiria nini akilini mwake?
  Alifikiri angeenda tu na kuingia na ingekuwa poa tu? Kwasababu ana nguo za kiaskari? au alikuwa keshapata chaArusha?
   
 15. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Hivi mnashangaa nini mbona kawaida kuwakuta BAR wakiwa na Bunduki (Hasa wale askari wa Defender) tena wanakata kinywaji.

  Na huyu hapo alikuwa na dili ya kuangalia nani ananunua sana vinywaji ili ampige risasi kisha aseme alikuwa ni jambazi.

  JE MMESAHAU YULE ASKARI ALIYEUA MWANACHUO KULE MBEYA??

  KAWAIDA YAO, NA UTASHANGAA KESHO ATATANGAZWA KUPANDISHWA CHEO NA ...........



  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 16. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  wengi wao wanafikiria ukorofi tu. Ukifuatilia vijana wanaokwenda kwenye mafunzo ya jeshi siku hizi wengi wao ni wale walioshindikana mtaani. Hivyo akilini mwao vinajaa visasi kwa jamii na kuvuta bangi tu. Nakumbuka hom kipindi fulani tuliwahi kukorofishana na polisi disco akaenda kuwaita wenzake wakaja na bunduki kututisha. Tuliwapokonya ile bunduki na kichapo tukawapitishia. Tangu kipindi kile jamaa wakijua tumerudi vijana wa chuo walikuwa hawaji disco. Sijui siku hizi hali ipoje. Police ni majambazi yaliyokabidhiwa kulinda usalama wa raia.
   
 17. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Dah hii habari kila nikifikiria nachoka kwa kicheko! Hebu fikiria upo Club alafu upo kwenye dance floor unayarudi unakumbana na polisi amebeba SMG nae akiyarudi!! Hakyanani mnaweza kutafutana!!!
   
 18. j

  jane_000 JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  habari sio kweli hakuna mtu anaruhusi kwenda club na smg
   
 19. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  umesoma vizuri kweli iyo habari?please jane be smart
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  hawa polisi wanaomaliza darasa la saba na kuchomekwa na ndugu zao kwa vyrti feki matatizo yake ndio haya
   
Loading...