Askari wa TAWA auwawa

Askari wa TAWA auwawa

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
21,174
Reaction score
54,553
IMG-20260920-WA0047.jpg

Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) anayefahamika kwa jina la Gift Eliaika (34) mkoani Tabora (pichani), ni miongoni mwa watu sita waliouawa baada ya baadhi ya wananchi kuvamia kambi ya askari waliokamata mifugo ya wananchi kutokana mifugo hiyo kudaiwa kuingia hifadhini mkoani humo.

Katika taarifa ya jeshi la polisi mkoani humo ambayo imetolewa kwa umma Septemba 19, 2026, imesema kuwa wananchi hao walifanya uvamizi huo wakiwa na silaha za jadi wakishinikiza wapewe mifugo yao iliyokamatwa.

Kadhalika, inaelezwa kuwa tukio hilo pia limesababisha majeruhi ya watu watano, huku silaha ya kivita aina ya AK47 pamoja na gari aina ya Toyota Land Cruiser kuchomwa moto.
 
View attachment 3674339

RIP hayo yote yataisha endapo tu utakuwa na katiba mpya.juzijuzi tu kama sikosei kiongozi mkubwa alitamka ng'ombe wakishikwa hifadhini wasitaifishwe wala kutozwa faini leo hii imekuwaje wananchi kuchukua sheria mikononi mwao.hapa napata picha kuwa yale yalikuwa matamshi yasiyo tekelezeka ndiyo maana wananchi hao wamepata hofu kuwa mifugo yao itapokonywa/kutaifishwa.sitetei vurugu bali natetea mabadiliko makubwa ya kimfumo,kisheria nk yafanyike.
 
Kuhusu kuuawa kwa huyu askari, pamoja na wananchi kuvamia ofisi za vyombo vya usalama, kuchoma magari na silaha haya ni matukio mazito ambayo hayapaswi kutazamwa kwa jicho moja tu.
Wakati raia wanapohisi kwamba wanakandamizwa, wanaonewa au hawapati haki, hasira hujikusanya taratibu moyoni,Na hasira inapofika mahali pa kuchemka, madhara yake yanaweza kuwa makubwa sana. Tumewahi kuona mifano ya matukio ambayo wananchi wamepoteza imani na vyombo vya usalama baada ya matukio ya vifo au matumizi ya nguvu yanayodaiwa kutokuwa na sababu za msingi mfano mauaji ya oct29,polepole,mauaji/kutekwa kwa wamasiasa wa upinzani nk.
Tatizo kubwa si tukio moja pekee; tatizo ni pale ambapo raia wanaanza kuona kwamba hakuna njia ya kusikilizwa, hakuna uwajibikaji na hakuna haki inayopatikana kwa wakati.
Huko nako kunaongeza kuchochea kisasi na vurugu. Leo anauawa askari, kesho raia, kesho yake mwingine mwisho wa siku tunaanza kuishi kama maadui ndani ya nchi moja.
Kuna wakati kikomo cha uvumilivu wa mwanadamu kinaweza kufika mwisho. Mtu akifika mahali anahisi hana cha kupoteza, anaweza kusema “liwalo na liwe.” Hapo ndipo tunapaswa kuwa waangalifu zaidi, kwa sababu hatua hiyo ni hatari sana kwa taifa.

Tusifike mahali ambapo raia wanawaona askari kama maadui, na askari wanawaona raia kama maadui. Tukifika huko, amani tunayodhani ni ya kawaida inaweza kuwa historia.

Taifa halijengwi kwa kisasi. Haki ikikosekana, tafutwe kwa njia ya sheria na uwajibikaji; lakini tusiruhusu hasira izalishe vurugu, na tusiruhusu vurugu izalishe kisasi.

Maana mwisho wa siku, tukianza kuwindana, hakuna atakayeshinda—tutakuwa tumepoteza wote.
 
Hao wananchi wajiandae Kwa gharika kuu litakalokuja hivi karibuni.

Halitasalia jiwe juu ya jiwe koo na jamii zao zinaenda kufutika
Dah sasa hivi wanajuta. Normal life waliokuwa wanaishi hawataweza tena kuishi hivyo milele. Nawaonea huruma hawataacha kuona kila rangi. Hasira hasara. Haya majitu unamwachia mungu tu ni makatili balaa yani yatakavyolipiza kisasi.
 
RIP hayo yote yataisha endapo tu utakuwa na katiba mpya.juzijuzi tu kama sikosei kiongozi mkubwa alitamka ng'ombe wakishikwa hifadhini wasitaifishwe wala kutozwa faini leo hii imekuwaje wananchi kuchukua sheria mikononi mwao.hapa napata picha kuwa yale yalikuwa matamshi yasiyo tekelezeka ndiyo maana wananchi hao wamepata hofu kuwa mifugo yao itapokonywa/kutaifishwa.sitetei vurugu bali natetea mabadiliko makubwa ya kimfumo,kisheria nk yafanyike.
Usije kuyaamini matamko ya kisiasa wanatamka jukwaani bila kuandaa waraka wa utekelezaji
 
View attachment 3674339
Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) anayefahamika kwa jina la Gift Eliaika (34) mkoani Tabora (pichani), ni miongoni mwa watu sita waliouawa baada ya baadhi ya wananchi kuvamia kambi ya askari waliokamata mifugo ya wananchi kutokana mifugo hiyo kudaiwa kuingia hifadhini mkoani humo.

Katika taarifa ya jeshi la polisi mkoani humo ambayo imetolewa kwa umma Septemba 19, 2026, imesema kuwa wananchi hao walifanya uvamizi huo wakiwa na silaha za jadi wakishinikiza wapewe mifugo yao iliyokamatwa.

Kadhalika, inaelezwa kuwa tukio hilo pia limesababisha majeruhi ya watu watano, huku silaha ya kivita aina ya AK47 pamoja na gari aina ya Toyota Land Cruiser kuchomwa moto.
Pole kwa Wafiwa!, ina maana Tawa ndiyo Wanatumia hizo AK 47?. hawa jamaa Kingwangalq alivyokuwa Waziri wao ndiyo aliwapa kiburi, wanauwa sana watu maenep mengi ya nchi hii...Hapo uhasama ushaingia kati ya hizo jamii na hao Tawa...Busara yapaswa kuchukua nafasi.
 
Tanzania tumefka huko yani SHERIA ni kujiongeza tu.

haya yote chanzo ni mifumo ya serikali kandamizi.
Raia hana mtetezi tena, hana pa kumpa haki yake iwe mahakaman n.k.

Ndo matunda yake haya, raia anaamua ajisaidie yey kama yeye.

Na hawa maaskari mistu ni makatiri sana huuwa raia bila huruma kama wanaua mbuzi tu, leo hii askari wao kauawa imewauma kweli na watafanya msako mkali mno.
Hzo juhud watazotumia kuwasaka watuhumiwa wangekuaga wanazitumia pia kumtetea raia alie uwawa na asikari mstu ingependeza.

MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAM MCHUNGU
 
Back
Top Bottom