Nimesikiliza radio Wapo asubuhi, wanasema polisi walikuwa wanashinikiza kuwa marehemu wawili walifariki kwenye ajali ya pikipiki, lakini baada ya mabishano na uchunguzi ulipofanyika ndipo ilipothibitishwa kuwa wote walifariki kutokana na kupigwa risasi, marehemu mmoja alikuwa na majeraha ya risasi na mwingine alikutwa na ganda la risasi mwilini. Kwa mujibu wa mwandishi wa Wapo radio, ilikuwa tukio lingine la aibu kwa polisi.
Sijajua hawa polisi walipata wapi ujasiri wa kutaka kuupindisha ukweli unaojulikana kwa wakazi wote wa Arusha. Na kama jambo kama hili lililo wazi kabisa polisi wanaweza kupotosha ukweli, je ni mangapi tunayoambiwa kutoka kwao tuamini.