Polisi Arusha wafanya unyama wa Kutisha

Tumieni njia nyengine ya kuwashikisha adabu hao Askari. Kwa hayo nafikiri Serikali itazifanyia kazi zikitolewa taarifa za namna hiyo.
 
Kwanza kama unasapoti tukio hili unatoa pole ya nini Kwa familia? Unafanya unafiki.

Pili, hakukuwa na njia nyingine ya polisi kumdhibiti kibaka (hata kama alikuwa anang'ang'ania silaha kama unavyotaka tuamini)? Ni kibaka sio jambazi kweli? Ndani ya kituo cha polisi ambako kuna zaidi ya Askari kumi Kwa uchache na ghala la kutunzia aina mbali mbali za silaha ambazo wamejifunza kuzitumia dhidi ya vibaka?

Mkuu muda mwingine tujaribu kuacha mahaba, tuwe binadamu kama Mungu alivyotaka tuwe. Kesho mdogo wako akiuliwa hivi utatoa kauli kama hizi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Panahitajika maombi ya kweli kuisafisha nchi yetu!Uhai wa mtanzania mmoja ,unapaswa kuwa wa thamani kubwa.Tuache majibu rahisi kwenye maswali fikirishi.
 
So kama alikuwa anang'ang'ania silaha alitegemea nini zaidi ya askari kujilinda? Sometimes tusiwe mashabiki tu. Poleni kwa familia.
unakataza watu kushabikia alafu ww unashabikia utetezi wa kamanda una uhakika gani?

ivi ujasiri wa raia kung"ang"ania silaha tena kituoni anautoa wapi?

kifupi akili yako unaitumia kwenda chooni na kuvuka barabara

polisi wa tz lini wameanza kusema ukweli, unajua kisa cha wafanyabiashara wa mahenge. ama aqulina

acha ujinga
 
Mimi nnahakika kwa kua kaka yake kasema ameshuhudia mdogo ake akipigwa ya kifua.lkn kibaka hana ujasiri wa kufanya hivo hasa akiwa kituoni,pale kuna askari wengi.
 
So kama alikuwa anang'ang'ania silaha alitegemea nini zaidi ya askari kujilinda? Sometimes tusiwe mashabiki tu. Poleni kwa familia.
Na kwaakili yako mtu yupo ndani ya kituo cha polisi halafu atake kuiba silaha tena kwa kuvutana na polisi, si bora ingekua mtaani huko wangeweza kutumia hy sababu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So kama alikuwa anang'ang'ania silaha alitegemea nini zaidi ya askari kujilinda? Sometimes tusiwe mashabiki tu. Poleni kwa familia.

Uwe na akiba ya maneno mkuu, ujue unazungumzia uhai wa mtu hapo
 
Ni mtoto wa mfanyakazi mwenzetu,ni ndugu wa kijana staff mwenzetu,ni ndugu binamu wa staff wenzetu wawili tena wameenda msibani!Ngoja nifikirie outside the box,Muhalifu apelekwe mpaka kituoni alafu auwawe hapo akiwa mahabusu?kwa nini wasimpige risasi huko njiani waseme alikuwa anatoroka waje wajiletee kesi bila sababu kwa kumuuwa akiwa kituoni?walikamatwa wawili inadaiwa lakini mmoja akatolewa akaambiwa asiseme chochote akitoka,hii nayo haingii akilini,mwenzio apigwe risasi ukishuhudia alafu wewe uachwe?Nani anataka ushahidi huo?Tusipende kuwalaumu polisi bure.Kwani polisi hujitaftia wahalifu au sisi wenyewe ndio tunapelekana huko kituoni?Imagine upige simu polisi majambazi au vibaka wamekuvamia nyumbani kwako polisi wasije?imagine uende kituoni ukatoe malamiko dhidi ya mtuhumiwa wako polisi wakae kimya?Tuwaache polisi wafanye kazi na tupishe uchunguzi wa vyombo vinavyohusika.Hakuna aliyekuwa kituoni,tuache kusikiliza umbea wa mitaani!Poleni sana staff wenzngu,poleni ndugu zangu wafiwa,mungu awape subra katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu.Haki ya mtu haipotei,huchelewa tu!
Kama nakuelewa vile lakini sikuelewi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanandugu mkazike mwili wa Marehemu,akapumzike kwa amani,safari yake ameimaliza.
Kaka mtu kama ulishuhudia tukio,utakuwa umemkariri huyo afande aliye muua mdogo wako,baada ya msiba mwendee INBOX
 
So kama alikuwa anang'ang'ania silaha alitegemea nini zaidi ya askari kujilinda? Sometimes tusiwe mashabiki tu. Poleni kwa familia.
Ivi mtuhumiwa atanganganiaje silaha akiwa kituo cha police.
chuki tu 😏😏😏
 
Hivi silaha vituoni zinakaa kama vyombo vya kabati la sebuleni au?! Tutasikia Mengi..uzuri damu ya mtu hulilia nafsi...huyo aliyemshoot hata iwe kapitia mafunzo ya kamati ya roho mbaya nafsi itamtesa tu.. Apumzike kwa Amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijana Richard Peter Lombo (29) ameuawa na polisi wilayani Arumeru kwa kupigwa Risasi kifuani akiwa ndani ya Kituo cha Polisi Usariva Mkoani Arusha baada ya kufikishwa hapo akituhumiwa kwa uhalifu.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Longinus Tibishubwamu akizungumzia tukio hilo kwa Njia ya simu amesema kuwa kijana huyo alikuwa kibaka na alitaka kuchukua silaha ya askari lakini katika mvutano huo ukasababisha risasi kufwatuka jambo ambalo kaka yake Issa Juma amesema kuwa ameshuhudia askari akimfyatulia ndugu yake huyo risasi ya kifuani na kufariki papo hapo.


Ndugu wa kijana huyo wakiwemo wazazi wake wamemtaka waziri wa mambo ya ndani ,Kangi Lugola kuja mkoani hapa kufuatialia tukio hilo kwani kinachoelezwa na kaimu kamanda in uongo mtupu na unalenga kuipotosha jamii.


Familia imegoma kuuzika mwili wa kijana wao uliipo Mochware wakilalamikia unyama uliofanywa na askari hao wasiofuata na kuzingatia maadili ya Kazi yao kwa kufanya mauaji ndani ya kituo hicho cha Polisi bila woga na kudanganya kuwa alitaka kuwapora silaha



Sent using Jamii Forums mobile app

So askari ana uadui na huyo kibaka. Mada zenu Wakati mwingine za kiuchochezi sana. Miaka 29 kibaka bado . Najiuliza tu wewe mwandishi huyu kibaka angekutwa mtaani kaiba hata simu tu ya 20 elfu na Mtendewa akaita mwizi itakuwaje. NATURAL LAW inasisitiza. Every one has the right to be heard .. wewe unaonyesha mahaba kwa kibaka bila kusikia upande wa pili.
 
Hivi silaha vituoni zinakaa kama vyombo vya kabati la sebuleni au?! Tutasikia Mengi..uzuri damu ya mtu hulilia nafsi...huyo aliyemshoot hata iwe kapitia mafunzo ya kamati ya roho mbaya nafsi itamtesa tu.. Apumzike kwa Amani

Sent using Jamii Forums mobile app

RIP. Acha kuhukumu . Nyie ndo wauaji wakubwa wa vibaka mtaani. Imagine 29 kibaka. Haiwezi kuwa simple tu. Eti askari kapata hamu tu ya kumpiga risasi na wewe Unakuja unakurupuka tu na itikadi.
 
Back
Top Bottom