Polisi Arusha wafanya unyama wa Kutisha

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
548
1,000
Kijana Richard Peter Lombo (29) ameuawa na polisi wilayani Arumeru kwa kupigwa Risasi kifuani akiwa ndani ya Kituo cha Polisi Usariva Mkoani Arusha baada ya kufikishwa hapo akituhumiwa kwa uhalifu.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Longinus Tibishubwamu akizungumzia tukio hilo kwa Njia ya simu amesema kuwa kijana huyo alikuwa kibaka na alitaka kuchukua silaha ya askari lakini katika mvutano huo ukasababisha risasi kufwatuka jambo ambalo kaka yake Issa Juma amesema kuwa ameshuhudia askari akimfyatulia ndugu yake huyo risasi ya kifuani na kufariki papo hapo.

Ndugu wa kijana huyo wakiwemo wazazi wake wamemtaka waziri wa mambo ya ndani ,Kangi Lugola kuja mkoani hapa kufuatialia tukio hilo kwani kinachoelezwa na kaimu kamanda in uongo mtupu na unalenga kuipotosha jamii.

Familia imegoma kuuzika mwili wa kijana wao uliipo Mochware wakilalamikia unyama uliofanywa na askari hao wasiofuata na kuzingatia maadili ya Kazi yao kwa kufanya mauaji ndani ya kituo hicho cha Polisi bila woga na kudanganya kuwa alitaka kuwapora silaha
 

Kilwa94

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,924
2,000
Hii imekaa vibaya sana!!
Ila kwanini raia tunaleta mazoea ya kijinga hivi kwa askari wetu,eti bila woga mtu unajaribu kupora silaha ya askari aliyeiva kimafunzo(well trained policeman).

5/5
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,356
2,000
So kama alikuwa anang'ang'ania silaha alitegemea nini zaidi ya askari kujilinda? Sometimes tusiwe mashabiki tu. Poleni kwa familia.
Kwanza kama unasapoti tukio hili unatoa pole ya nini Kwa familia? Unafanya unafiki.

Pili, hakukuwa na njia nyingine ya polisi kumdhibiti kibaka (hata kama alikuwa anang'ang'ania silaha kama unavyotaka tuamini)? Ni kibaka sio jambazi kweli? Ndani ya kituo cha polisi ambako kuna zaidi ya Askari kumi Kwa uchache na ghala la kutunzia aina mbali mbali za silaha ambazo wamejifunza kuzitumia dhidi ya vibaka?

Mkuu muda mwingine tujaribu kuacha mahaba, tuwe binadamu kama Mungu alivyotaka tuwe. Kesho mdogo wako akiuliwa hivi utatoa kauli kama hizi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom