Ni mtoto wa mfanyakazi mwenzetu,ni ndugu wa kijana staff mwenzetu,ni ndugu binamu wa staff wenzetu wawili tena wameenda msibani!Ngoja nifikirie outside the box,Muhalifu apelekwe mpaka kituoni alafu auwawe hapo akiwa mahabusu?kwa nini wasimpige risasi huko njiani waseme alikuwa anatoroka waje wajiletee kesi bila sababu kwa kumuuwa akiwa kituoni?walikamatwa wawili inadaiwa lakini mmoja akatolewa akaambiwa asiseme chochote akitoka,hii nayo haingii akilini,mwenzio apigwe risasi ukishuhudia alafu wewe uachwe?Nani anataka ushahidi huo?Tusipende kuwalaumu polisi bure.Kwani polisi hujitaftia wahalifu au sisi wenyewe ndio tunapelekana huko kituoni?Imagine upige simu polisi majambazi au vibaka wamekuvamia nyumbani kwako polisi wasije?imagine uende kituoni ukatoe malamiko dhidi ya mtuhumiwa wako polisi wakae kimya?Tuwaache polisi wafanye kazi na tupishe uchunguzi wa vyombo vinavyohusika.Hakuna aliyekuwa kituoni,tuache kusikiliza umbea wa mitaani!Poleni sana staff wenzngu,poleni ndugu zangu wafiwa,mungu awape subra katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu.Haki ya mtu haipotei,huchelewa tu!