Polisi anapogeuka kuwa mwizi...............!

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Inatisha........, kila sifa jeshi letu la polisi linazo. kabla ya wingu la mauaji ya mwandishi (shujaa) MWANDOSI halijafutika juzi askari mwingine toka tazara amekamatwa na wenzake, wakiiba mali toka zambia huko bandalini,na wengine wakakimbia na madumu ya petroli. ili hali ya jeshi hili iboreke ninini la kufanya watanzania wenzangu.....mbona ni kuchefuchefu kitupu jeshi hili.................?
 
mishahara wanayolipwa wala siwalaumu kwa wao kuiba...wewe unasema polisi wanaiba...kwani kuna mtu haibi? kuanzia serikalini mpaka chini
 
mishahara wanayolipwa wala siwalaumu kwa wao kuiba...wewe unasema polisi wanaiba...kwani kuna mtu haibi? kuanzia serikalini mpaka chini

mshahara wako ni mkubwa kuliko wa polis?!, ndo maana huibi?!, mshahara wako ni mdogo kuliko wa polisi?!, ndo maana unaiba?
 
kila mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamaba yake
 
Jeshi la Polisi linahita kufanyiwa mambo yafuatayo:
i)Kuondoa uongozi wa juu wote kabisa, kwa kuwastaafisha au kuhamishia magereza, na kuleta wengine kutoka JWTZ.

ii)Kufanya vetting kwa hawa askari wa kawaida kupitia kura ya siri ya wananchi wa kawaida, na kisha wale ambao watakuwa wameonekana hawafai watolewe, na kama makosa yao ni ya jinai na yanathibitika washitakiwe mahakamani.

iii)Uteuzi wa IGP ukifanyika upitishwe Bungeni ili aweze kuthibitushwa au kukataliwa

Wakuu naomba niwakilishe hoja yangu.
 
Ningewatetea kwa kusema kila mtu anaiba so sishangai kusikia ati polisi kaiba! ningewatetea kwa kusema mishahara yao midogo ndiyo maana wanaiba kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine!
Lakini nashindwa kwa sababu whatever the reason its iimoral kuiba...eniwei, kwa sababu ni polisi tuendelee kuwaponda tu!
viva wezi wakubwa...
 
Jeshi la Polisi linahita kufanyiwa mambo yafuatayo:
i)Kuondoa uongozi wa juu wote kabisa, kwa kuwastaafisha au kuhamishia magereza, na kuleta wengine kutoka JWTZ.

ii)Kufanya vetting kwa hawa askari wa kawaida kupitia kura ya siri ya wananchi wa kawaida, na kisha wale ambao watakuwa wameonekana hawafai watolewe, na kama makosa yao ni ya jinai na yanathibitika washitakiwe mahakamani.

iii)Uteuzi wa IGP ukifanyika upitishwe Bungeni ili aweze kuthibitushwa au kukataliwa

Wakuu naomba niwakilishe hoja yangu.

Seriously kuna haja ya kufanyika mapinduzi (mabaliko makubwa) ndani ya vyombo vyetu vya usalama VINGINEVYO TUNAPOKWENDA SIPO. System take the note najua mnasoma hizi threads
 
Mbona hawaibi saa na kutia watu roba mitaani kama kweli mishahara midogo, manake mtu anaenda kuiba shaba ya 1bn useme njaa huo ni wizi uliotukuka.

Sema kuna wezi ambao nao ni askari kuna askari wameoa au kuolewa na waarifu na wao wakabadilika kuwa waalifu kama wenza wao. We mke wa kamishna anapiga magumashi hapo kweli ni mshahara mdogo. Jembe liitwe jembe jamani msilete udambu udambu.

Kuna waarifu ambao ni polisi, kuna polisi wamegeuka kuwa waalifu kutokana na tamaa za ajabu ajabu.
 
unanipa taswira ya jinsi watanzania tulivyo...binafsi sielewi unataka nikujibu nini kwa kuwa sioni mantiki ya swali lako, elewa kwanza ndio uulize

umetoa vague statement... not sure unahalalisha au unalaani wizi wa polisi
 
Polisi wetu huendelea kufanya ufedhuri kwa sababu wao wanajilinda sana kana kwamba wa sheria haziwagusi ifike muda ambapo police wakipatikana kuvunja sheria wafungwe kama kawa bila hivyo tutengemee MABAYA ZAIDI KUTOKA KWA POLISI.
 
Hii ndo tz.

Tusiishie tu kukubali kwamba hii ndio Tz, I say something must be done! Niliwahi kusuggest humu kuwa Polisi hii tuliyonayo sasa( I don't call it 'jeshi' kwa sababu halikidhi vigezo vya kimafunzo vya kuwa jeshi kutokana na matendo yao yanayojiri kila uchwao) linahitaji kuvunjwa na kufinyangwa upya! Fukuza kazi manjago wote waliopo kazini hivi sasa, recruit new fresh boys and girls teach them a good Civic lesson use Police trainers from abroad sio wale waliopo pale Ccp Moshi au Kilwa Road maana maadili yao yamekaa kimagambamagamba na hawa ndio chanzo cha maadili ya hovyo ya mapolisi tunayoyaona sasa
 
Back
Top Bottom