Ujio wa Tundu Lissu, wananchi wamelithibitishia Jeshi lao la Polisi kuwa wao ni watu wa amani na utulivu

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,331
2,000
Hatimaye shujaa wa Taifa hili, Tundu Lissu amewasili nyumbani Tanzania akiwa mzima wa afya, baada ya kutokuwepo hapa nchini kwa takribani miaka 3, akiwa nje ya nchi kwa matibabu ya majeraha makubwa sana aliyoyapata, takribani miaka 3 iliyopita, baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 16, zilizolengwa kwenye gari lake huko Dodoma na watu ambao wamebatizwa jina la "watu wasiojulikana"
waliokuwa na nia ya kumwuua.

Mapokezi makubwa sana aliyopokea shujaa huyo wa Taifa hili, hakika ni tukio la kihistoria.

Tumejionea maelfu kwa maelfu wakiusindikiza msafara huo wa shujaa wetu, tena bila ya ulinzi wowote wa Polisi, bila ya kusikia malalamiko yoyote toka kwa mwananchi yeyote ya kuibiwa kitu chake chochote au kujeruhiwa, katika muda wote wa masaa kadhaa ya msafara huo.

Tendo moja limethibitika katika ujio huo wa Tundu Lissu, kuwa wananchi wa Tanzania ni watu wapenda amani sana na hawana fujo wasipochokozwa na Jeshi la Polisi.

Kumbuka kuwa Jeshi la Polisi hapo awali lilipiga "mkwara mzito" kuwa ni marufuku kwa wananchi hao kwenda kumpokea mpendwa wao Tundu Lissu, ambaye wamem-miss mno, kwa kile walichodai kuwa kusanyiko hilo ni batili ambalo halijaombewa kibali kwao, kwa hiyo litaleta vurugu na kusababisha usalama wa watu hao kuwa shakani.

Tukumbuke pia wananchi wengi walikuwa na hamu mno ya kumwona shujaa wao amerudi akiwa mzima wa afya, baada ya kipindi cha takribani miaka 3 akiwa nje ya nchi kwa matibabu.

Kwa hiyo lilikuwa tegemeo la wananchi hao kuwa Jeshi hilo lisingepiga marufuku wananchi hao kwenda kumpokea huyo shujaa wao na badala yake Jeshi hilo liweke ulinzi kwenye msafara huo

Hata hivyo nilishukuru sana Jeshi hilo la Polisi, kwa kufanya uamuzi wa busara sana katika "dakika za majeruhi" kwa kuamua kutotumia nguvu kuwazuia wananchi hao walioamua wenyewe kwenda kumpokea mpendwa wao.

Ndipo hapo nikapata somo kuwa kumbe vurugu zote ambazo huwa tunaziona kwenye mikusanyiko yoyote huwa zinasababishwa na Jeshi hilo la Polisi kutaka kutumia nguvu kubwa ya kuzuia mikusanyiko hiyo ambayo ni wananchi hao huwa wanakuwa hawajavunja kipengele chochote cha Katiba ya nchi, kwa kuwa mikusanyiko ya wananchi inaruhisiwa kwa mujibu wa Katiba hiyo.

Mfano halisi ni namna Taifa hili lilivyompoteza mwanafunzi mdogo kabisa kwa umri, ambaye alikuwa hana hatia yoyote, Akwilina Akwiline, aliyepigwa risasi za moto na Polisi na kufa papo kwa papo wakati mmojawapo aliyekuwa miongoni ya Polisi hao waliokuja kuzima maandamano hayo ya amani ya wanachadema, kufyatua risasi "kizembe" miaka michache iliyopita wakati Jeshi hilo likitaka kuvunja maandamano hayo kwa nguvu, wakidai yalikuwa haramu na hayakuombewa kibali Polisi

Niwasihi Jeshi letu la Polisi watekeleze wajibu wao kwa weledi na kwa mujibu wa Katiba ya nchi na wasikubali kupokea maagizo haramu toka kwa watawala waliopo wa CCM.

Kwa kufanya hivyo ndivyo tutakavyoweza kudumisha amani na utulivu katika Taifa hili ambalo mara nyingi wanasiasa wetu wamekuwa wakiinadi nchi yetu kuwa ni "kisiwa" cha amani ambayo nchi yetu imejaaliwa.

Mungu ibariki Tanzania
 

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
920
1,000
Umenikumbudha sikuu fulani hivi, mc kwenye ziara ya waziri mkuu alimruhusu kiongozi mmoja wa Chadema kusslimia. Uwanja mzima ulilipuka peoplezz. Baada ya mkutano mc alisndamwa kwa kuipa Chadema sifa.

Wabaya Ni viongozi wa juu kwa hofu ya kutokujiamini. Kesho Lissu akipewa nafasi uwanja utatoa radi
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,331
2,000
Kwa yaliyotokea leo, acheni Mungu aitwe Mungu.
Salary Slip
Hakika Mungu ni mkuu kuliko kitu chochote hapa duniani.........

Alitakalo huwa na asilolitaka, hata kama wewe binadamu utafanya juhudi gani, ATAKATAA LISIFANYIKE

Mfano halisi ni hili la shujaa wetu Tundu Lissu, ingawa watesi wake walipania kumwuua Lissu, lakini Mungu wetu mpenda haki, AKAWAGOMEA!
 

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
7,624
2,000
La Akwilina R.I.P lilitosha kuwa funzo kwa watu wenye kufikiri na twaweza sema kwa tukio la leo mhanga yule damu yake haikwenda bure
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,331
2,000
Jana CHADEMA imethibitisha kuwa wanaoletaga vurugu ni polisi.
MtamaMchungu
Ni kweli kabisa, hilo Jeshi la Polisi ndilo chanzo cha vurugu zote..........

Refer kifo cha mwanafunzi ambaye hakuwa na hatia, Akwilina Akwiline, ambaye alipigwa risasi hadi kufa na mmojawapo wa Polisi aliyeletwa kwa madai ya kutuliza maandamano yaliyokuwa yanaendelea kwa amani ya wanachadema katika kipindi kile
 

Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,975
2,000
Bujibuji
Ni kweli kabisa, tunayaona mabadiliko haya makubwa ya Jeshi la Polisi, baada ya huyo Bashite kutumbuliwa na "Ba'mkubwa" wake 😁 😆
Naona mnamkandia Paulo, lakini haya mambo ni ya system nzima na mauaji hayakutokea Dar peke yake. Mara zote ambazo polisi hawakuingilia kati mambo yalikwenda shwari kama jana. Kumbuka Arusha, Morogoro na kwa Mwangosi na Akwilina hakukuwa na uvunjaji wa amani hadi pale polisi walipoingilia. Kwenye matukio yote hayo hakuna hata mkubwa mmoja alielaumu polisi bali upinzani hasa CDM. Kutumbuliwa Bashite hakuna uhusiano na jinsi polisi walivyo shughulikia swala la jana. Nina hakika system iliwaelekeza watulize mhemko-si walisha onyesha dalili za kukinukisha? Swali ni je system itajifunza kutokana na yalivyotokea jana au ilikuwa special ya kumuaga Mh. Mkapa tu? Time will tell!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom