Kwa ufupi polisi wetu wameshaona wabongo ni matoinya tu hatuna sumu, wanaweza kutupa hata maelezo ya kipumbavu kwenye jambo linalohitaji maelezo yakinifu.Kuna tukio la kuokotwa mwili unaelea jangwani ,wananchi wakasema kwamba ameuawa na "GENGE LA MUUZA MATAIRI K/KOO" ,polisi wakajitokeza wakasema kwamba ule mwili ni wa kijana ambaye anaishi magomeni alikuwa na matatizo ya kifafa siyo kwamba alitekwa ila wananchi wakahoji sawa alikuwa na kifafa ilikuwaje amefungwa kwenye kiroba? Yaani Polisi majibu/taarifa zao ni za MASHAKA MASHAKA sana.
Mbaya zaidi siku hata polisi nao wanatetewa na raia kwa majibu hayo ya kipuuzi kwenye mambo mazito