wewe vipi TZ hatumiliki pingu za nini bana
Kwa nini hatumiliki? Kuna sheria yeyote inayokataza umiliki wa pingu?
Nafikiri hakuna sheria hiyo kwa sababu hakuna sababu za kumiliki pingu za nini kwanza kwani umekosa kamba
Itakuwa vigumu kumtia hatiani jamaa kwa vile hakuna sheria inayokataza kumiliki pingu.
Kuna wengine watakamatwa kwa kumiliki kondom huku wakiwa na mwanamke mke wa mtu.
Na hapo polisi wamebugi, na hicho ndicho kielelezo kuwa wameset the whole thing, kwanza sidhani kama kuna maduka duniani yanoyouza pingu kwa raia wa kawaida ila silaha peke yake. Na ikiwa Jerry alikuwa na pingu maana yake aliipata through security organs-polisi.
hapo Kova amechemsha.
Wanamwonea tu dogo.
Tanganyika ARMS wanauza pingu, technically ni ruksa kumiliki pingu kwa matumizi binafsi, kwa sababu hakuna sheria inayokataza.
Kwani nyie hamjawahi kufungwa pingu kitandani na wapenzi wenu?
FETISH ni kitu ngeni kwa Watanzania wa nyumbani.....usikutane nayo ni balaa utapigwa mijeledi na pingu umefungwa kwenye tendegu za kitanda...
Kwani kazi ya pingu ni NINI?
Hivi mnafikiri mtu akitaka kufunga mtu mwingine anahitaji PINGU tu?
Alikuwa anazitumia pingu kwa ajili gani, hiyo ni juu yake. Kama kuna mtu akiona PINGU basi anaanza kutetemeka, basi huyo ana matatizo. Mbona Mgambo huwa wanafunga watu mashati, sasa mtu ukikutwa na shati basi ukamatwe kuwa una PINGU.
Mwisho, POLISI wawaelimishe wananchi kuwa ni watu gani wana kazi gani. Unakuta hata Mwana jeshi wa JWTZ ana kagua watu na mizgo yao barabarani. Polisi anakuwa JAMBAZI, mgambo anakuwa POLISI, Jembe Auction wanakuwa POLISI ...... mhhhhhhhhhhhh
Hizi plastic hapa chini ni kwa ajili ya kutumia kwenye kuweka waya za umeme/alectronics pamoja, mabomba, nk. Ila hapa zinakuwa Pingu. Labda akienda dangulo anataka wamfunge pingu................