Polepole: Ukitukana tusi moja namchomoa Kiongozi mmoja DSM

Polepole: Ukitukana tusi moja namchomoa Kiongozi mmoja DSM

maforce

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2017
Posts
676
Reaction score
644
Leo January 4, 2018 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amewatahadharisha Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) ndani ya mkoa wa Dar es salaam kuwa atamng’oa kiongozi mmoja wa chama hicho.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Polepole amesema baada ya madiwani wawili wa CHADEMA kuachia ngazi Mjini Iringa, ambapo ametoa sababu ya Madiwani hao kuhamia CCM kuwa ni kumuunga mkono President JPM.

“Leo Madiwani wengine wawili wamehama na kujiunga na CCM. Ukiwasikiliza kilichowaondoa ni Uongozi Mbovu na Ubabe pale Iringa. Nasikia wameambiwa “never outshine your master”. Mimi nilidhani “masta” ni wananchi kumbe ni “pasta”. Ukitukana tusi moja Kiongozi mmoja nachomoa DSM ” – Polepole

f90761d43a9a3f5337121b1adead17dc.jpg
85df185c8a47179f9821e8feed059b05.jpg
 
Nashangaa hi akili ya nunua,kwann wasitumie wazo la mbowe na kakobe yakufuta vyama vingi nakuwa na ccm tu ili kuepuka kuwabebeshea garama wananchi isiyo na msingi.tumechoka nahaya namasikio yetu yamechoka nahuo uozo,.badala ya hapa kazi tu imekuwa sasa hamahama tu
 
Halafu na hao wanaokubali kuchomolewa kwa dharau hizi za Polepole ni wajinga kweli! Njaa kamwe isikuaibishe kiasi hicho. Anasema kabisa akijisikia kumchomoa mtu anamchomoa na bado yapo mazuzu yanayoenda eti tunamuunga mkono Magufuli!
 
Ishakuwa zilipendwa sasa ccm mje na mipango mipya upinzani kwenda ccm hakuwezi kukifanya chama cha mapinduzi kuwa kitakatifu.
 
kwaiyo ni jeuri ya Pesa siyo hakuna siasa tena !!!
Nani kawaloga nyie vijana!
 
Nashangaa hi akili ya nunua,kwann wasitumie wazo la mbowe na kakobe yakufuta vyama vingi nakuwa na ccm tu ili kuepuka kuwabebeshea garama wananchi isiyo na msingi.tumechoka nahaya namasikio yetu yamechoka nahuo uozo,.badala ya hapa kazi tu imekuwa sasa hamahama tu
Wewe ulitrgemea na kuamini kauli mbiu ya " hapa kazi tu" itadumu hadi 2018?
 
Naona biashara ya Ujenzi wa Viwanda ndio imekufa rasmi sasa..
Ni mwendo wa CCM kununua Viongozi wa CHADEMA tu.
Duh! Tangu Mbowe afike bei na CCM 2015
Chama chetu kimekuwa na viongozi wanaonunulikanunulika kirahisi sana! kiasi kwamba hatujui nani mwingine ananunuliwa kesho.
 
Madiwani hawana misharara wala dili za kupiga. Acheni wapokee hela, maana wasipopokea watabaki maskini. Hata madiwani wa CCM wanatamani na wao atokee mtu wa kuwanunua, maana hali ni ngumu. Haiwezekani uifanye kazi miaka mitano kwa kujitolea
 
Kauli zingine ni sawa na kufanya comedy tu

Ova
 
Back
Top Bottom