GE2025 Polepole: CCM tunakaribia kutekwa na kundi la wanamtandao

GE2025 Polepole: CCM tunakaribia kutekwa na kundi la wanamtandao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Agosti 13, 2025 wakati Humphrey Polepole akiendelea na mazungumzo yake kupitia mitandao ya kijamii ameeleza kuwa CCM inakaribia kutekwa na Wanamtandao na watu wanajua ingawa wanawaogopa ila yeye hawaogopi.

"Huku sisi tunakaribia kutekwa na kundi la wanamtandao mtu yeyete aliyekuwepo toka zamani anajua hizi issue. Sema watu wanawaogopa umenielewa eeh? kwa sababu hawa jamaa wana mbinu nyingi ndiyo maana watu wanawaogopa. Mimi siwaogopi hamna nafasi kwenye chama cha mapinduzi untill it's done" - Humphrey Polepole
View attachment 3440777

Yeye lengo lake wana mitandao wa Ccm, lenho letu ni kuondoa hiyo ccm na mizizi yake.
 
Agosti 13, 2025 wakati Humphrey Polepole akiendelea na mazungumzo yake kupitia mitandao ya kijamii ameeleza kuwa CCM inakaribia kutekwa na Wanamtandao na watu wanajua ingawa wanawaogopa ila yeye hawaogopi.

"Huku sisi tunakaribia kutekwa na kundi la wanamtandao mtu yeyete aliyekuwepo toka zamani anajua hizi issue. Sema watu wanawaogopa umenielewa eeh? kwa sababu hawa jamaa wana mbinu nyingi ndiyo maana watu wanawaogopa. Mimi siwaogopi hamna nafasi kwenye chama cha mapinduzi untill it's done" - Humphrey Polepole
View attachment 3440777
Polepole alikuwa na nafasi ya kumueleza JPM (Rip) adui yake halisi ni hao 'wanamtandao' na sio Tundu Lissu na Chadema kama alivyoamini hata akaishia kuwatesa na kuwakandamiza, hili Polepole hajaonyesha kulijutia.

Tindo JokaKuu zitto junior
 
Slowslow ana mkwala 😄
Hao so called mtandao mbona
Washakishika chama
Hii episode sjui season haina mwisho

Ova
 
Maneno matupu hayavunji mfupa
Alipaswa kutuambia after hayo maneno yake ana strategy plan ipi ya kuwazuia hao Wana mtandao

For now everyone knows ccm imeshikwa sana na kundi la wapiga deal Mabwanyenye na sio hivyo tu kundi Hilo Lina wadharau Watanzania sana kitendo Cha mtu kama Seth ambaye ana kashfa kibao za Upigaji kuonekana katika Hafla za ccm Inaonyesha wazi kwamba serikali imewadharau Wananchi wake na Wala haijali kabisa kuhusu maisha Yao na lawama zao so yote hayo tunayajua

So pole pole anapaswa kutuambia what he's planning to do ili kuua Hilo kundi la Wana mtandao au Amechagua kuishia kuwa mpiga zumari tu,

Hizo mbinu za Upigaji zumari zimeshatumika sana Na kina Lissu and the likes but it won't help
Samia na genge lake wanawadharau sana watanganyika, kitendo cha yule Seth kuonekana hadharani vile kwamba anashiriki kuifadhili ccm iendelee kubaki madarakani ilikuwa ni sababu tosha kabisa ya kuiondoa serikali iliyopo, maana imeonesha wazi kuwa inaongozwa na majizi pamoja na wahujumu uchumi.

Sasa kivip tuendelee kuongozwa na viongozi ambao wanafadhiliwa na watu wanaolirudisha nyuma taifa letu kwa kulihujumu? Hayo maendeleo tutayapataje?

Kwa ufupi tu mpaka hapa serikali ya samia imeshapoteza sifa za kuliongoza taifa.
 
Agosti 13, 2025 wakati Humphrey Polepole akiendelea na mazungumzo yake kupitia mitandao ya kijamii ameeleza kuwa CCM inakaribia kutekwa na Wanamtandao na watu wanajua ingawa wanawaogopa ila yeye hawaogopi.

"Huku sisi tunakaribia kutekwa na kundi la wanamtandao mtu yeyete aliyekuwepo toka zamani anajua hizi issue. Sema watu wanawaogopa umenielewa eeh? kwa sababu hawa jamaa wana mbinu nyingi ndiyo maana watu wanawaogopa. Mimi siwaogopi hamna nafasi kwenye chama cha mapinduzi untill it's done" - Humphrey Polepole
View attachment 3440777
Hizo bilioni za wahuni zitawatokea puani. Yetu macho
 
Interesting. Polepole ndio kwanza anaamka kuhusu wana mtandao? Leo hii?

Nyerere mwenyewe alilazimika kutoka Butiama mbio kuja DSM Lumumba kupunguza spidi ya hao jamaa kuteka chama na Ikulu mwaka 1995. Wakati huo wakijulikana kama boyz-to-men. Bila Nyerere Mkapa asingekuwa Rais wa awamu ya tatu. Toka 2005 walipoingia Ikulu, CCM imekuwa yao. Miamba kama Rostam Aziz ndio ikaanza mipango mikakati wakati huo.

Walibabatizwa tu 2015, "mtu baki" akapenya. Polepole na wenzake nao badala ya kumsaidia mtu baki aung'oe mtandao jumla wakaishia kuzuzuka na mavieite na ufahari wa Ikulu huku waki-terrorise wakosoaji na kuangamiza upinzani wakiamini ndilo tatizo lao kubwa. Rostam na Lowasa wakarejea na kupokelewa kwa mbwembwe!

Wanamtandao wakavuta subira wakijua ipo siku "washamba" wataachia ngazi na kurejea "kijijini" walikotokea na wao watashika hatamu tena.

Safari hii wamejiweka sawa. Si rahisi kuwang'oa. Tena wamerithi mbinu za kuzuzua (mesmerise) wajinga, ku-terrorise wakosoaji/wenye akili, kupanga matokeo ya uchaguzi mezani, na kujigawia hazina bila taratibu. Awamu ya tano iliua bunge, halmashauri na mahakama. Wanamtandao safari hii hawahitaji tena kupanga dili kama za escrow, epa, rada, n.k. Ni mwendo wa NO scandal tena. Ni wao kujizolea mabilioni na wajinga kusifu miradi tu.

Imebakia kwa Watanzania tu kuamka na kuchukua hatua. Nje ya hapo tuna CCM ya wenyewe na serkali yao milele daima!
 
Back
Top Bottom