Polepole athibitisha unafiki wa urafiki ndani ya CCM

Polepole athibitisha unafiki wa urafiki ndani ya CCM

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,268
Reaction score
13,895
Polepole athibitisha unafiki wa urafiki ndani ya CCM! Yaani mtu ambaye mlikuwa karibu hutaki hata kujua hali yake hata baada ya Mama mzazi wake kuongea hujali hata kuuliza na hata kusema basi unamuombea na kumuombea shinikizo aachaliwe. Yaani muongeaji pekee ni Heche!!!! huko CCM kuna binadamu kweli!!!

Watu hawajali hata ubinadamu wako! yaani huyu kijana anapoteza maisha kwa lipi hasa??? tujiulize kama jamii ? kama wewe unanyamaza je wewe umechangia huyu kijana kufa? kutokujali kwako kunaweza kuuwa wengi
 
Zamani nilikuwa nafikiri kwamba viongozi wakubwa wa nchi wanajuana, wamesoma pamoja, wanalindana, etc.

Sasa kuna mshua mmoja wa kwenye familia alikuwa kwenye uongozi hivyo, akapata kazi ya ubalozi mkubwa sana , akaja nchi niliyokuwapo, mji niliokuwapo.

Sasa nilivyojua hivyo, nikamtembelea kumkaribisha. Si mzee wa familia kaja kwenye kituo kipya cha kazi mjini kwangu? Nikaenda hotelini kwake alikuwa hata nyumba hajahamia.

Dah, sasa nilivyofika pale alifurahi sana. Mtu wa stories sana. Ikafika wakati yeye na mkewe wakawa kama wanapiga stories, sasa mimi wananiona mtu wa familia tu wakawa wanapiga stories zao za mambo ya wakubwa serikalini. Ebwanaaa, stories zao sasa. Nani kamzunguka nani, nani kapiga pesa za wapi, nani haaminiki, yani ni kusalitiana, kupigana, kushindana, kuzikana kutupu.

Nilivyotoka hapo nikawa na uelewa tofauti kabisa na ile dhana kwamba wakubwa wana umoja, wanalindana.

Kila mtu anapigania kula kwake.
 
Maisha haya bila kuwa na imani ni vigumu kuwa na utu, matatizo yako ni fursa kwa mwingine. Mfano, ufukuzwapo kazi ni fursa kwa mwingine kupewa hiyo nafasi, upatapo umauti ni fursa kwa mwingine kukuuzia jeneza, upatapo kesi ni fursa kwa wakili kupata pesa n.k​
 
Back
Top Bottom