Balozi
Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye amaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba.
Mnamo mwezi Julai 13, 2025 Polepole, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram alichapisha
barua iliyotoa taarifa ya kujiuzulu nafasi ya ubalozi, ambapo kabla ya Taarifa hiyo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba.
Tarehe 18, Julai 2025 Balozi polepole alifanya mkutano na waandishi wa habari mbashara kupitia ukurasa wake wa
Facebook ambapo
awali alifafanua kuwa mkutano huo ni kwa ajili ya kufafanua barua ya kujiuzulu aliyomuandikia Rais.
"Nitaifafanua barua niliyomuandikia Mhe. Rais kwa hatua na kwa maana njema ili kuondoa upotoshaji"
Taarifa inayomhusisha Polepole
Baada ya mkutano huo, katika mtandao wa Facebook kumekuwepo na taarifa inayosambazwa, ikitumia utambulisho wa grafiki za Millard Ayo, kuwa Balozi Polepole amewataka wagombea wa CCM kudumisha uvumilivu.
Je ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu, pamoja na marejeo ya video, umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli, kama inavyoeleza kwani kauli hiyo haijatolewa na Polepole katika
mkutano wake.
Pia grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo isiyo ya kweli, ni ya kughushi kwani haijachapishwa katika kurasa rasmi za
Millard Ayo kwenye mitandao ya kijamii.
Aidha katika mkutano wake na waandishi habari pamoja na mambo mengine Polepole alikosoa vikali utaratibu uliotumika kumpata mgombea wa Urais pamoja na makamu wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
akisema 'Wakati mwingine inabidi tubomoe ili tujenge. Mchakato wa kupata wagombea tumeukosea'
"Unajua wakati mwingine lazima tubomoe ili tujenge mimi mkristo kuna mstari unasema wakati mwingine inabidi tubomoe ili tujenge. Huu mchakato wa kupata wagombe kwa kweli tumeukosea"
Kadhalika Polepole aliendelea kusisitiza kuwa mchakato uliotumika haukuwa halali kwani kwani hautakiwi kuingizwa waa kunakoweza kusababisha kutia doa wagombea.
"Ule mchakato ni kama mtakatifu, hautakiwi kuwa na waa lakini ukiingiza waa unatia doa wagombea wetu, hilo moja nimeona lilikwenda ndivyo sivyo, mimi nilishindwa hata kuwapongeza, sijawapongeza mpaka leo, unapongeza vipi kisicho halali?
View: https://www.facebook.com/hpolepole/videos/1035169325065298