Polepole alipuka tena, awajibu Bulembo na Nape

Kiturilo

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
706
Reaction score
2,859
"Kwenye CCM binadamu wote ni sawa haijalishi uanachama wako uliupata wakati wa African Association (AA) au TAA au ASP au TANU au Babako alikuwa kada au Babako au Mamako alikuwa Kiongozi kwenye chama au hata kama huna rekodi kama za wanaojiita wenyewe au ulikuwepo Mwaka 1977 tarehe 5 Februari, mbele ya CCM sisi wote ni sawa." Mhe. Mbunge, Humphrey Polepole katika Ukurasa wake wa Facebook.
 
"Kwenye CCM binadamu wote ni sawa haijalishi uanachama wako uliupata wakati wa African Association (AA) au TAA au ASP au TANU au Babako alikuwa kada au Babako au Mamako alikuwa Kiongozi kwenye chama au hata kama huna rekodi kama za wanaojiita wenyewe au ulikuwepo Mwaka 1977 tarehe 5 Februari, mbele ya CCM sisi wote ni sawa." Mhe. Mbunge, Humphrey Polepole katika Ukurasa wake wa Facebook. #GADITVUPDATES

WAZO KUU LA PRESS YA POLEPOLE;

Nilichokiona kama ujumbe mkuu katika Mkutano wa Polepole na Waandishi wa Habari ni hili;

Nimeanza kukutana na mkono wa Serikali, nimepewa mashtaka ya kujibu kwa TCRA kwa tuhuma za Kuvunja Kanuni za Maudhui za Kimtandao (Online Content Regulations) kwahiyo Jumatatu tarehe 13.12.2021 nimeitwa kujitetea mbele ya Mamlaka hiyo ya Mawasiliano (TCRA); naombeni huruma (sympathy) ya Watanzania kwani nahisi naonewa.

POLEPOLE amezunguka sana kuelezea "historia" ya Shule yake ya Uongozi, lakini kumbe target yake ilikuwa ni kuelezea jinsi gani ameanza kukutwa na MADHIRA ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao, ambazo zilitungwa na Awamu ya 5 Serikali ya Magufuli wakati yeye mwenyewe akiwa Mshauri wa karibu wa Magufuli, kwa lengo la kuwahushughulikia Wakosoaji wa Serikali yao kwa kutumia mitandao.

Wengi walikosoa sheria hizo mbaya, lakini zilitumika kuwazimisha wakosoaji binafsi na hata Online TV, Polepole hakutumia dhamana yake kuwasemea Watu waliopata madhara hayo.

Leo yeye anailalamikia sheria aliyoshiriki kuitunga na akafurahia kuitumia kuwadhibiti wakosoaji na Wachambuzi wa siasa enzi za Magufuli.

Anatutangazia kwamba ameitwa TCRA, ili tumsaidie nini?

Wabunge kadhaa waliwatahadharisha sana WanaCCM kwamba Sheria zinazotungwa zinaweza kutumika kuwahushughulikia wao wenyewe baada ya kupoteza madaraka yao.

POLEPOLE yamemkuta na ni mfano mzuri.

Pole lakini jikaze.
 
Huyu Polepole ni mbaya sana kwani alikuwa anafurahia sana kipindi cha awamu ya tano wapinzani walivyokuwa wakishughulikiwa si mtu wa kumuonea huruma let him face the music huko ndani ya CCM
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom