Poleni sana Watanzania Wenzangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Poleni sana Watanzania Wenzangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsangulaKG, Jul 21, 2011.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Kwanza mtanisamehe kama nitakusea Kiswahili kidogo lakini nimejitahidi sana kuhakikisha kuwa si isahau Lugha Ya Nchi Yangu
  Naandika Waraka huu nikiwa natulia kidogo kushika Tama, kama mtanzania aishiye nje ya nchi yake kikazi.

  Nawapa pole sana kwa taarifa za mara kwa mara ninazozipata hasa kubwa kabisa ni hili la Mgao MKUBWA wa umeme ambao nadhani kwa sasa unaongoza Duniani. Suala Kubwa ninalojiuliza hivi viongozi wetu, kama rais akitembelea nchi nyingine kama Africa kusini au marekani huwa anafumba Macho?

  Hawezi kuona mifumo ya wengine kuanzia kwenye miundo mbinu na nishati akaiga japo Kidogo?
  Kwa nini Wamarekani wafurahie Maji ya bomba yasiyo na wadudu ya moto na ya baridi wakati bongo ni mgao wa maji?

  Je wao walijifunza wapi au ni udiriki wao na viongozi imara?
  Hapa nilipo sijawahai kuona umeme umekatika labda kwa kuwa wanatumia mfumo wa volti ndogo lakini kama hiyo ni suluhu kwa nini basi nasi huko nyumbani wasibadili?

  Marais hao wanaoingia Madarakani hawaoni aibu?

  Kwa kuwa nili mchagua Kikwete lakini sasa naanza kujiuliza siku niliyopiga kura nilikuwa nimelewa? Nadhani nilikuwa nimepiata kidondoni but nasikitika saaaana kuwa nami nilimchagua!

  Kuna wakati nadha ni akitoka ikulu akaona Maghorofa ya Posta anasahau na kusema haya ndo Maendeleo..akiwasahau wanakijiji wa Pale Charambe!

  Poleni saana Ndugu zangu Muda si Mrefu nitarudi tu ....japo moyo unasita kweli kweli
   
 2. g

  geophysics JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole yako haitusaidiii hata kidogo....kwanza wewe ndo umetuweka katika matatizo haya kwa kumchagua mtu asiyejali wananchi (JK) harafu ukakimbilia huko unakotulingishia Marekani. Pili wewe una uwezo wa kutumikia nchi yako lakini badala yake umeamua kuwasaidia walioendelea na mahali ambapo maji na umeme haukatiki.... sasa pole ya nini? Tatu unasema moyo unasita....... Acha kutukejeli.......
   
 3. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Nililitegemea Hilo lakini labda nawe umekosea ulipoaandika Upo Kigali na Hiyo najua iko Rwanda...we're in the same boat Brother!
   
 4. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kama una kazi nzuri fweza inaingia na life ni poa na huna cha kukuleta we jikalie huko huko mkuu. Unless una valid reason ya kugeuza. Maisha popote tu.
   
 5. g

  geophysics JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Karibu Dar es Salaam-Mwenge kwa wachonga vinyago (chumba 84) nitakupa zawadi ya vinyago au artworks yoyote najua Wamarekani wanavipenda vinyago hasa wa New Hampshire na Connecticut.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu huyo jamaa anajiita mtulutumbi na maana ya mtulutumbi ni mchawi!! Kwenye avatar yake kuna bundi ambalo huhusishwa na uchawi!!
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Weee mtulutumbi unataka kututukana? Hicho kijiji cha charambe kiko wapi? Manake mimi naishi mbagala Charambe sasa usije kuniambia kwamba ndicho kijiji unachokisema?
   
 8. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kabila gani????
   
 9. M

  Madoido Senior Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole mwenyewe, huna maana rudi bongo ujenge nchi yako, wakati huu wa shida ndio tutawatambua wazalendo ni nani na nani
   
 10. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako unadhani kujenga nchi ni kupiga makelele na kuandmana tuuu...unaweza kuwa nje ya nchi ukajifunza na ukaja na mawazo mazuri, huoni Rais wa Liberia alikuwa wapi na anafanya nini..wakati mwingine ufikirie japo kidogo
   
 11. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Pumba tupu Una Busara sana ni bora Ubadili jina ndugu yangu
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mujita, kwi!kwi!kwi!
   
 13. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,768
  Trophy Points: 280
  Inaelekea umeondoka huku zamani sana............... CHARAMBE NI KIJIJINI.!!!Au kuna Charambe nyingine zaidi ya ile ya Mbagala..???
   
 14. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  wewe endelea kubeba boksi usituzingue na pole za kinafiki!
   
 15. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Wewe mkuu kabila gani kwani,uko nchi gani mkuu?
   
 16. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Pole mwenyewe uliyekimbia matatizo ya nchi yako!
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Asante sana tumeshapoa
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  yaani unajifanya umesahau kiswahili kabisaaaaaaaaaa. huna hata aibu....mwaka jana umekuja na ukapiga kura halafu leo unasema eti samahani kama ntakuwa nimekosea kiswahili....huko uliko huna hata miaka 20........usitupe pole sisi wewe lilila ndugu na jamaa zako.....

  ulimbukeni tu unakusumbua......
   
 19. g

  geophysics JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Hapana mkuu mtulutumbi hawezi kuwa mchawi....maana wachawi wakifika amerika uchawi wao huwa unayeyuka... Pia angekuwa mchawi asingetuonea huruma sisi watanzania wenzake.... Huyu ni msomi tena msomi kweli we cheza naye...ninachoweza kumhisi ni kuwa ni mzuri wa kusoma alama za nyakati... Kaona tanzania ya sasa ilivyo kama yai visa (fragile and when bust will stink) kaamua kuchanja mbuga na anasikilizia kwa nje hadi pakae sawa arudi.
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu sijasema yeye ni mchawi ila jina analojiita maana yake ni mchawi na bundi pia anahusishwa na uchawi!!! Mkuu hakuna wasomi ambao ni wachawi?
   
Loading...