Poleni sana vijana wangu wa TMAA

Hili halitaishia kwa watumishi waliokuwa TMAA pekee, litaenda pakubwa sana. Taasisi zinazolipa CEO na DG zaidi ya 12M zipo za kutosha.

Ila mzee mkubwa anafanya kazi kwa mihemko sana, hii ni hatari sana!!!
Mimi namkubali. Alichofanya ni sahihi
 
Wapigwe chini tu maana walimu na wauguzi kule vijijini hawana mishahara mikubwa lakini ni majembe kweli wanapiga kazi mno tena hawatoshi lakini hawaachi kazi huo ndio uzalendo wakweli ikikuuma acha kuna na biashara nyingi za kufanya mtu unalipwa mamilioni ya hela kwa mwezi unashindwaje kuishi wakati wenzio wa laki tatu na wanasomesha hadi ndugu zao shame
 
wewe unafanyia kazi serikali hiyo hiyo unalipwa kama ofisa wa serikali ya Ulaya wakati mwenzio analipwa kama anafanyia kazi serikali fulani ya Afrika.

Ndo maana hatukomai kuwa wajasiriamali. Ukipata ubosi ndo kila kitu. Au ukipata kazi TMAA au TRA umemaliza
 
Zinakusanya zilizozalishwa na wazalishaji
yaani maana yake kama tunaangalia kwa namna sawa,haitakiwi hawa walipwe mbuzi,wengine ng'ombe.

maana humo humo kuna watu wanafanya kazi nzito sana na wanalipwa mbuzi,yaani mambo ni shaghala baghala.
 
Umeongea point ya msingi sana kila kazi ina umuhimu wake huyo anaekusanya mamilioni asingeweza kukusanya bila kupita kwa mwalimu
 
Na huo ndio uzembe mwingine uliofanyika kwa nini taasisi za serikali zisiingizwe ktk scale za serikali(TGS) toka awali?
Kuna sehemu kama taifa tuliyumba na kuachia watu mianya madhara ndio tunayaona sasa.
 
Hapana mkuu,NASA ni moja ya tasisi ambayo staff wake wanalipwa vizuri,wizara/taasisi zinazolipa vizuri USA zinafahamika wala sio kitu cha kuficha,hata katika jeshi,jeshi la anga la marekani wanafahamika kwa kuwa na malipo mazuri.hata training academy zao zipo classic sana tofauti na wengine,hiyo ipo wazi hata ukienda youtube utakuwa documentary kibao na videos zipo.Point yangu ni kwamba,tuangalie namna ya kulipa watu wetu mishahara kuendana na uhalisia wa maisha ili kusiwe na haya malalamiko,ila sio kupunguzia watu mishahara kwa nguvu
 
Huyu mnyampara uwezo wake wa kufikiri uko < average afadhari angewastishia ongezeko la mishahara hao anaoona wana mishahara mikubwa wakati huo huo akiwapatia nyingez wale anaoona wana mishahara ya mbuzi kama member mmoja alivyisema hapo juu
 
Makusanyo yakiongezeka tena wajiongezee tena, yakiongezeka tena wajiongezee tena hawa wengine ambao sio wakusanyaji wabaki tu stagnant wakati wenzao wanapaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…