Pole sana ndugu yangu mh. Godbless Lema, nina ujumbe wako nakupatia leo

Daima hakuna mtawala yeyote duniani hupendezwa kuambiwa maneno yasiyompendeza na kumfurahisha.

Watawala wana tabia zinazofanana nayo ni kupenda kuogopwa na kuambiwa yanayowapendeza tu, na huamini zaidi yale wanayoambiwa na wapambe wao hata kama si sahihi, kwa vile tu wapambe wao huwatia moyo kuwa "mambo yako sawa tu".

Najua una huzuni, hasira na fikra mpya kila wakati, "wewe ni mchochezi", ndio nami nakubali kuwa wewe ni mchochezi, unachochea ktk kuleta fikra mpya za umuhimu wa kuwa na KIONGOZI na sio MTAWALA.

Pole sana ndugu! kazi ya siasa na ukombozi inahitaji gharama ya moyo na nafsi za watu. hongera kwa kujichagua.
Umesahau mwambie bado kifungo cha kutumikia gerezani kinamsubiri ajiandae pia atatumikia katika gereza la KILIMO MALYA HUKO KWIMBA.
 
ALISHASEMA DHAMBI KUBWA NI UOGA. SIDHANI KAMA ANAJUTA KATU. ANAAMINI ANACHOKIFANYA NI SAHIHI NA KWELI YUKO SAHIHI. 50 MILLION TANZANIANS ARE AFRAID OF TELLING THE KING THAT HE IS NUDE! HE HAS DARED TO!
Kwani kumtabiria mtu kifo ni kuongea ukweli huyu si yule mchungaji aliyetuambia kumzomea mwizi kama Lowasa tutapata thawabu na baadaye akakaa na mwizi itakuaje tumuamini sasa
 
Kwani kumtabiria mtu kifo ni kuongea ukweli huyu si yule mchungaji aliyetuambia kumzomea mwizi kama Lowasa tutapata thawabu na baadaye akakaa na mwizi itakuaje tumuamini sasa
WE are talking of Lema , not Lowasa! These are two different scenarios
 
Kosa kutukana ukiwa mzima. Umesahau alichokisema? Unafikiri aliyokuwa anayasema alikuwa usingizini? Na ile sms yeye na mkewe waliituma wakiwa usingizini? usitake kucheza na maneno na mimi, hutoniweza.
Kwa Faiza tena...labda ni mgeni hakujui
 
Usisahau na kumtukana mkuu wa mkoa.

Nilisema humu hili litam cost Lema, hamkunielewa.

haalafu Mkuu wa mkoa amabae ni mwakilishi wa Rais anaongea, yeye anajidai kimbele mbele mbele ya waalikwa wengine kwenye hadhara.

Nilijuwa lile ni kosa kubwa sana kwa kumfanyia hivyo mwakilishi wa Rais kwenye mkoa. Na nilijuwa litamgharimu sana na nililisema humu.

Na hata siku mawakili walivyojidai kumtafutia dhamana eti kwa rufaa ya mahakama kuu, nikasema tena, bora wamsiombe rufaa wamuache hapo hapo, hataachiwa.

Kinyangarakata kama kile hakiwezi kushindana na dola. Hawakuweza akina Kambona mpaka wakaikimbia nchi ataweza huyu mjinga?
Mmmhhh maneno makali.
 
Anachofanyiwa Lema ni reflection ya serikali inayonyanyasa raia wema kwa kutumia nguvu ya dole.
Lema hana kesi inayohitaji nguvu kubwa kiasi hicho,tusijifanye wendawazimu.
 
Kama ushujaa ni kuwatabiria vifo wale wanaotenda usiyoyataka ndio ushujaa.
Sidhani kama jamii ikijengwa ktk mfumo huo inaweza kuimarika.

Watu kama ninyi ndio mnamfanya asijutie matendo yake mabaya.
Waliomtabiria Lowassa kifo nani aliwachukulia hatua?? Wengine walimdhihaki Mungu kwa kukejeli kuwa hawezi hata kuzungusha mikono kwa ishara ya mabadiliko

Mungu yupo na atatenda
 
Yawezekana sijui kesi yake kwa usahii lakini kitendo cha kumtabiria kifo na kutangaza hadharani kiongozi anayeongoza nchi hakikubaliki.
Mahali popote,

Biblia imetuasa kuheshimu wenye mamlaka na kuwaombea.

Yaliyo nje ya hapo yatoka kwa yule mwovu.
Kama Biblia inasema nimuheshimu mteule wa Jecha. Nipo tayari kuiacha na kwenda motoni.

Usihusishe Biblia na mambo ya kijinga

Back to topic, Lema hakutabiri kifo. Huu ni uongo wa kipuuzi tu. Okay ni sheria ipi inamuhukumu hapo?
 
Hii watajua wanasheria mimi fani hiyo
sina,

Lakini ikiwa hata mimi nitaota ndoto eti jirani yangu nisiyempenda wala kukubaliana naye,
Eti asipobadilika atakufa na mwingine akaota na mwingine akaota Tanzania nzima ikajaa ndoto zenye chuki na visasi
Na kuzihubiri hadharani sidhani kama hiki kinachoitwa Tanzania kitaendelea kuwepo.

Lema ni mwanasiasa mzuri tena anayekubalika arusha na Tanzania yote lakini kwa wastaarabu wanaona kama anavuka mipaka ya kiuti na kijamii,

Bahati mbaya sijui nani wa kumshauri arekebishe aina ya siasa anazozifanya kwa sasa ikiwa viongozi wake wakuu wanamuunga mkono.

Ngoja tusubiri na kuona.
Kama hizo ndoto huzipendi au unaona hazifai washauri wakuu watunge sheria ya kuhukumu wanaoota. Very simple lakini kwa sasa hakuna sheria ya kumhukumu zaidi ya uonevu unaoendelea
 
Hivi Lile swala la kuanzisha hospital mpya ya akina mama Na watoto ambayo chimbuko lake ni wazo zuri la Mheshimiwa Lema limeishia wapi? Hiyo hospital tunaihitaji sana jamani, kwanini wanamvuruga Ili ashindwe kufanya mambo yenye kuleta tija kwetu sisi wananchi! Yaani ......
Lipieni kadi za kielectroniki ili tupate bilioni 13.9 kwa mwaka tutaijenga tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom