Godbless Lema, Pokea Hongera na Pole

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,307
6,514
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, kwanza salamu kwako. Pokea pole kutoka kwangu, lakini pia zikufikie hongera zangu nyingi zenye ujazo wa kutosha.

Nakupa pole kwa sababu kwa takriban miezi mitatu ulitenganishwa na familia yako unayoipenda. Mkeo alikukosa bila shaka, wanao waliikosa huduma yako. Wapigakura wako pia hukuweza kuwahudumia. Imekuwa heri mpo pamoja tena. Mungu ni mkuu.

Pokea pongezi, maana miezi yako mitatu mahabusu imekuwa na elimu kubwa kwa maisha ya Watanzania. Mapambano yako na mawakili wako katika kukupigania dhamana katika kipindi chote hicho, juu yake kuna shule kubwa.

Ni shule kuhusu nyakati tulizopo, kipindi tunachopita na upepo unavyovuma. Shule kuwahusu binadamu na namna ambavyo wanaweza kutendeana. Shule kuhusu binadamu na mikono yao, amri zao, uthubutu na kusudi zao pale wajionapo wameshika rungu.

Hongera sana Lema, endelea kupokea heko, maana umekuwa kielelezo dhahiri. Mbunge kunyimwa dhamana kwa miezi mitatu, mbunge kupigania dhamana miezi mitatu! Raia wa kawaida pangupakavu itakuwaje pale wenye nguvu wasipotaka?

Lema umetumika kutuonesha nchi ilivyo. Ukitetewa na mawakili wasomi na maarufu lakini uliikosa dhamana kwa miezi mitatu, je, raia wa kawaida, kabwela wa daraja langu asiyeweza kumudu japo wakili?

Kumbe sasa tuelewe kuwa wapo wenye kunyimwa dhamana kwa sababu kuna watu fulani hawataki wawe huru. Vipi wasio na uwezo wa kukata rufaa juu ya rufaa? Vipi wanyoosha mikono na wepesi kutamka “namwachia Mungu?”

DHAMANA NI NINI?

Dhamana ni hati ya ahadi yenye kusainiwa na mlalamikiwa au mdhamini wa mlalamikiwa, kwamba kiasi fulani cha fedha au mali, italipwa na mwenye kusaini hati hiyo ya ahadi endapo mlalamikiwa hatatokea mahakamani baada ya kuwa huru chini ya dhamana.

Inawekwa ahadi hiyo kama angalizo kuwa mshtakiwa anaweza kutoroka akiwa na kesi mahakamani. Dhamana hunyimwa kama kesi ni nzito au pale inapoonekana usalama wa mshtakiwa au yeyote utakuwa hatarini kama mlalamikiwa atapewa dhamana.

Kwa ufafanuzi huo sasa tujadili; Lema ni kiongozi, inawezekanaje kuhofia kuwa anaweza kutoroka? Kesi ipi ambayo ameshtakiwa ionekane ina uzito wa kumnyima dhamana?

Kwa nini mara ya kwanza baada ya dhamana kutolewa ndipo mapambano ya rufaa juu ya rufaa yalianza mpaka kumchelewesha Lema kupata dhamana kwa miezi mitatu?

Sera ya Serikali ni kesi kuendeshwa haraka ili hukumu zitolewe mapema. Huo ndiyo mkazo wa Rais John Magufuli.

Kesi ya Lema imeonesha kuwa kumbe wachelewesha kesi siyo Mahakama, bali Serikali kwa maana ya Jamhuri.

Kesi ipo mahakamani, badala ya kujikita kwenye kesi ya msingi ili iwahi kumalizika, mawakili wa Serikali wao wakajielekeza kwenye mapambano ya dhamana. Mahakama inatoa dhamana wao wanakata rufaa.

Miezi mitatu ambayo imetumika katika mapambano ya dhamana, ingetumika vizuri pengine kesi yenyewe ingekuwa imekwisha kisha hukumu kutolewa.

Kwa mapambano ya dhamana kesi ya Lema jinsi yalivyokuwa na namna yalivyopoteza muda, ni wazi Rais Magufuli anatakiwa kuwakemea mawakili wa Serikali kwa kuchelewesha kesi na siyo Mahakama.

Jamhuri imemfungulia kesi Lema. Inaamini kuwa mashitaka dhidi ya Lema ni yenye nguvu. Na kama lengo ni kumfunga Lema, njia rahisi ilikuwa kujielekeza kwenye kesi ya msingi, Jamhuri iithibitishie Mahakama kuwa Lema anapaswa kupewa adhabu kali, Mahakama ione, iridhike kisha imfunge.

Mapambano ya dhamana hayana tafsiri ya kucheleweshwa kwa kesi peke yake, bali pia kuna kukomoana, kuoneshana umwamba au pengine kukosa imani na kesi ya msingi. Hivyo adhabu pekee ikawa kulazimisha akose dhamana kwa miezi mitatu.

SIKUPI POLE LEMA

Bila shaka ulikuwa ukiumia kipindi chote cha kusotea dhamana. Hilo mimi sikupi pole, badala yake nakupa pongezi. Msoto wako umekuwa rutuba inayostawisha mbegu ya ufahamu mpaka kwenye vichwa vya walio wengi.

Siwezi kukupa pole Lema, wewe siyo James Richardson wa Arcadia, Florida, Marekani, aliyefungwa jela kwa kifungo cha mateso na maumivu makubwa mwaka 1967.

Richardson alipoteza watoto wake saba kwa mkupuo. Watoto wake walinyweshwa sumu na kufariki dunia. Akiwa na maumivu makali ya kufiwa na wanaye saba kwa wakati mmoja, Richardson akapewa kesi ya kuwaua wanaye.

Mashitaka yaliandaliwa na Richardson akafikishwa mahakamani kwa kuwaua wanaye saba ili ajipatie fedha nyingi kupitia malipo ya bima. Askari walifika mahakamani na kusema Richardson alikiri mbele yao kuwaua wanaye.

Richardson alilia mahakamani, akasema hakuwahi kukiri popote kuua wanaye. Yaya wa watoto wa Richardson, Bessie Reece, alifika mahakamani kutoa ushahidi kuthibitisha Richardson ndiye aliwawekea sumu wanaye.

Mtaalamu wa Mahakama aliyepima ushahidi wa Reece, alitaka mwanamke huyo (yaya) asiaminiwe kwa sababu yupo nje kwa msamaha baada ya kumuua mume wake. Hata hivyo, mtaalamu huyo hakusikilizwa.

Kesi hiyo ikiendelea, Richardson alibambikiwa kesi nyingine. Watu walipiga kelele kuwa Richardson alikuwa akionewa kwa sababu ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika. Hakuna aliyejali, hukumu ikatoka, Richardson alihukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Hukumu hiyo ilibatilishwa na Mahakama ya Rufaa Marekani, kwamba ilikuwa inakwenda kinyume na Katiba, kwa hiyo iliamuliwa Richardson afungwe jela maisha. Richardson akaishi jela kwa unyonge, akiumia kupoteza wanaye na kusingiziwa kesi ya mauaji juu yake.

Richardson aliishi jela miaka 21, ndipo Reece wakati anaugua alipokiri kuwa ni yeye aliyewapa sumu watoto saba wa Richardson na kuwaua. Uchunguzi mpya ukafanyika na kugundulika ni kweli Richardson hakuua wanaye wala binadamu yeyote.

Baada ya Richardson kutoka jela, aliwafungulia kesi polisi kwa kumbambikia kesi iliyomfanya afungwe jela, ikabidi polisi wamlipe fidia ya dola 150,000 ambazo ni Sh335 milioni kwa sarafu ya sasa.

Hivyo, Richardson ndiye anapaswa kupewa pole kwa majanga yaliyompata. Kufiwa na wanaye kisha yeye kuitwa muuaji na haikuishia hapo akafungwa. Siyo wewe Lema ambaye msoto wako mahabusu miezi mitatu umefungua chemchemi mpya za ufahamu kuhusu mfumo wetu wa utoaji haki.

NAKUPONGEZA LEMA

Hapa nakwambia ukweli kuwa hapo kabla sikuwahi kushawishika kupenda aina ya siasa zako za harakati na amsha-amsha kila wakati. Sikuwahi kukusikitikia hata mara moja ulipokamatwa na kuwekwa mahabusu kwa sababu niliamini sheria inachukua mkondo wake.

Mimi napenda siasa za hoja. Siasa za mchuano wa fikra. Wewe unajenga hoja zako katika namna unayoamini na mwingine anajenga zake. Navutiwa na siasa za kutofautiana bila shari. Siasa za kuachiana nafasi, kuvumiliana na kustahiana.

Tukio la kunyimwa dhamana miezi mitatu, limenipa fikra mpya. Kwa mara ya kwanza nikaguswa na kujisikisia vibaya kwa namna ulivyotendewa. Ndiyo maana nilikwambia msoto wako wa dhamana ni rutuba iliyostawisha mbegu mpya ya ufahamu kuhusu mfumo wetu wa haki.

Kama mimi nimeguswa, naamini na wengi pia wameguswa. Wengi waliokuwa wakikuona kuwa mwanasiasa mpenda fujo, awamu hii walielekeza huzuni zao juu yako. Kumbe sasa, miezi yako mitatu ya msoto wa dhamana imekuwa ya mapinduzi makubwa ya fikra za walio wengi.

Miezi mitatu imekuwa hivi, sijui wangekuweka miezi sita ingekuwaje? Siombei ungeendelea kuwepo mahabusu, maana maombi hayo ni ukatili mkubwa kwa familia yako iliyokukosa kwa muda mrefu.

Sithubutu kuomba hivyo, maana ingekuwa maumivu kwa wapigakura wa jimbo lako, waliokosa huduma yako kwa kitambo kirefu. Isipokuwa nimewaza kwa kukopa ubongo wa malaika ambao Mungu amewaamuru wawe nami nyakati zote.

Nakupongeza Lema, maana kipindi kile nilikuwa nakuona mwanasiasa mpenda fujo, ila miezi hiyo mitatu uliyosoteshwa mahabusu, imenibadili kifikra. Nilipokuwa nikifuatilia habari zako za rufaa za dhamana, nikasema Lema ni Ali Salem Tamek.

Ona Lema nilivyokupandisha daraja. Nakufananisha na Tamek ambaye ni mwanaharakati hai, mpigania dola huru ya Sahrawi. Tamek alishaamua kuyatoa maisha yake sadaka kwa ajili ya kuhakikisha ndugu zake, yaani watu wa Sahrawi wanajitawala kama taifa huru.

Sahrawi inakaliwa kimabavu na Morocco. Kila Mahakama za Morocco zinapomfunga jela Tamek, akitoka ndiyo anakuwa na moto mkali zaidi. Tamek kukamatwa na kufungwa jela siyo mshangao. Tamek anapokaa uraiani muda mrefu bila kukamatwa ndiyo watu hushangaa.

Kwa msingi huo unatakiwa ujipongeze kuwa miezi yako mitatu rumande haikuwa ya bure, malipo yake ni makubwa. Ni malipo ambayo huwezi kuyaona kwenye salio benki wala chakula mezani, malipo yake ni kwamba umeweza kuingia kwenye mioyo ya watu wengi zaidi. Ni malipo yenye thamani inayopita kiwango chochote cha pesa.

Kwa hali hii naweza vipi kukupa pole wakati msoto wako jela umekuwa mtaji mkubwa kwa maisha yako, siasa na harakati zako? Chama chako kilicheza mpira mgumu kuhakikisha unatoka, hata hivyo nacho kimevuna matunda ya msoto wako. Thamani yake sasa si sawa na miezi mitatu iliyopita.

UTAWATESA WASIPOKUJULIA

Hapa Lema wala sitaki kukupamba kinafiki. Siamini hata kidogo kuwa wewe ndiye hasa unatakiwa kuwa mbunge maarufu zaidi, nikipima michango yako ndani na nje ya Bunge.

Kama ingekuwa unapimwa kwa hoja zako za ndani ya Bunge au hata nje, ungebaki kuwa mbunge wa kawaida, japo sisemi wewe huna athari bungeni. Athari unayo, tena kubwa, ila wapo ambao wanakuzidi bungeni lakini unawameza nje ya Bunge.

Lema, wewe mtaji wako ni dola. Kadiri dola inavyotumia nguvu kukudhibiti ndivyo na wewe unavyopaa kwa umaarufu. Utaendelea kuitesa na utazidi kuitumia kama ngazi ya kupaa kwako kisiasa kama haitajishitukia na kujirekebisha.

Nguvu haijawahi kuwa nyenzo bora ya mapambano kama akili haipewi ushiriki wa kutosha. Mabavu bila kushirikisha ubongo matokeo yake ni kuua mende kwa shoka kwenye marumaru. Mwisho muuaji kugeuka kichekesho.

Yapo mambo ambayo kweli hayakuwa na maana yoyote wewe kuyatamka, lakini jinsi ambavyo nguvu kubwa imetumika kukushughulikia, ndiyo inayowafanya watu kusahau makosa yako na kuishia kukuhurumia, huku wakiwafikiria watumia nguvu kwa pupa bila kupata majibu.

Kama wangekuwa wanatumia kiasi cha nguvu sawasawa na kosa husika, pengine hali isingekuwa kama ilivyo sasa. Tatizo wanaamini mno mamlaka. Hawajui kuwa mamlaka yameelekezwa kufuata sheria. Tanzania ni nchi ya utawala wa sheria.

Kufikia sasa, jina lako halizungumzwi Tanzania tu, bali ulimwengu umeambiwa mengi kuhusu msoto wako wa dhamana. Utaona kuwa jina lako linakua zaidi. Maana yake nguvu za dola zimekuwa daraja la kupaisha jina lako mpaka anga nyingine.

TUMIA UJASIRI WAKO

Badala ya kuzungumza vitu ambavyo havina tija mpaka kusababisha kugombana na mamlaka za nchi, tumia vizuri ujasiri wako kwa kuyanena yale muhimu kwa nchi ambayo yanaogopwa kusemwa na wengine.

Hakikisha ujasiri wako hautumiki vibaya. Ujasiri ni kipawa ambacho si kila mtu anapewa. Ukiwa jasiri tambua kuwa wewe ni maalumu, kwa hiyo tumia kipawa chako kuzungumza yenye faida kubwa kwa taifa lako na jimbo lako.

Fanya kuwavuta zaidi watu kwako kwa kuingia kwenye mgogoro na dola kutokana na kuzungumza au kupigania mambo yenye msingi mkubwa kwa nchi na jimbo lako. Achana na tafsiri za njozi japo sioni kosa, shindana na unayedhani anakuminya kwa hoja bila lugha za kuudhi.

Nikuhakikishie, ukifanya hivyo fikra zako na jitihada zako hazitakwenda na maji. Hutakuwa kama Sabino Arana, ambaye fikra na mapambano yake ya kuhakikisha jamii ya Basque inakuwa taifa huru, ziliishia Gereza la Larringa, Bilbao, Hispania mwaka 1903.

Arana akiwa nembo ya jamii ya Basque, alipigana mno kuhakikisha jamii yao inakuwa na utaifa wake, ikimega sehemu za Ufaransa na Hispania ili kuunda nchi yao mwishoni mwa Karne 19.

Arana alipofikwa na mauti mwanzoni mwa Karne 20, kutokana na maradhi aliyopata jela, kuanzia hapo ndoto za Wabasque kupigania taifa lao zikapotea. Maono, fikra na mikakati aliondoka nayo Arana.

Nakuhakikishia kuwa ukiwa na maono bora Lema, hayatafia jela kama maono ya taifa la Basque yalivyofia gerezani na Arana. Hata sasa Wabasque maeneo yao huita nchi lakini walishasalimu amri.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Bp

Bla bla blaaa sitaki kusikia
 
Well spoken Maloto, Lema's pain was not in vain, wengi tumefunguka akili
 
Hongera kwa Ujasiri wako Kamanda Lema Ila hawaelewi kuwa Nguvu haijawahi kuwa nyenzo bora ya mapambano kama akili haipewi ushiriki wa kutosha. Mabavu bila kushirikisha ubongo matokeo yake ni kuua mende kwa shoka kwenye marumaru. Mwisho muuaji kugeuka kichekesho.
 
Back
Top Bottom