Pole sana Dada

Mbona hata wadada nao sio wakweli. Wanashindwa kujiamini. Mara nyingi unakuta binti ana wachumba zaidi ya wawili. Likisanuka wote wanamtema. Utasemaje wanaume ni waongo.
 
Ni kweli mkuu. Hawatulii. Wanakuwa na waume wengi kama kubahatisha na mwishowe bahati Nasibu inawaponza.
 
Maisha sio kuolewa tu.....

(Ukizingatia walioolewa wenyewe wanajuta kwa tabia za ajabu walizonazo wanaume.... (baadhi))
Ni kweli kuna walioolewa na mambo yao si mazuri. Hata hivyo kuna waliofanikiwa. Ni kwanini ujitabirie kundi la walioshindwa na iwe sababu ya kutoolewa?
 
Tuache kuwananga wanawake wakati tatizo 75% ni sisi wanaume
Kwa asilimia kubwa wanawake wanaachwa kwa kupenda makuu. Kama vile maisha ya juu. Wengi wanakubali wanaume kwa lengo la kupata chochote na wanakuwa hawana mapenzi ya kweli. Baadae wanaanza kulia wanaume hawaaminiki!
 
Ni kweli mkuu. Hawatulii. Wanakuwa na waume wengi kama kubahatisha na mwishowe bahati Nasibu inawaponza.
Na ndo maana baadae wanakuja kufikisha umri hadi miaka 40 anakuja kujishtukia kuwa kajipotezea muda kwa kumkimbia anayefaa na kuwakimbilia wachezeaji t .
 
 
Kwa lugha nyepesi tuseme wanawake wanaume wote ngoma droo hakuna aliezidi mwenzie,

Wenye nia nzuri hawakutani na wenye nia nzuri wenzao, hii formula sijui ikoje.
Hapa dada ndo umeongea point. Big up!
 
Pole sana dada, hata vimini havikupendezi kwasasa!, maana goti limekomaa utachekwa na vijana huko nje
 
Mbona hata wadada nao sio wakweli. Wanashindwa kujiamini. Mara nyingi unakuta binti ana wachumba zaidi ya wawili. Likisanuka wote wanamtema. Utasemaje wanaume ni waongo.
Ni kweli hapo unakula ametegesha atakaye kuwa mkweli basi ndiyo atafanikiwa kuoa.

Na huyo wa hivyo ukirudi nyuma utakuta alishaumizwa na mwanaume kisaikolojia na hapo haamini MTU tena kama anachosema ni kweli.
 
Pole sana dada wema sepetu í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…í ½í²…
 
daaah sio wote wasio olewa walichezea baati au walilinga ujanani, wengine wanaupenda usingo ndo maisha walio jiamulia, afu sio ndoa zote nzuri kuna wengine wanajuta hata kuolewa usikariri
Hiyo ni kauli tumezoea kuiskia siku zote toka kwa wakosaji.
 
Hahahahhaha duh sio kwa mashairi hayaa chaa...
 
Wanaume tuna bahati sana na mambo ya ndoa. Hata uwe na miaka 50 utaona mtoto wa kike anatafuta mume wa miaka 50. Lakini huoni mwanaume anatafuta mchumba wa miaka 50.
Labda mariyoo ndio huwa hawaangalii umri wa mwanamke wao wanahitaji mwenye pesa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…