Pole Dr. Slaa, Pole CHADEMA

Pole Dr. Slaa, Pole CHADEMA

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
31,195
Reaction score
18,224
TUmeona mlivyopambana bungeni na jinsi mlivyopigwa vita left right and center...

Tumeona mlivyojitolea kusaidia waathirika wa Gongo la Mboto na jinsi media yetu na serikali zinavyojitahidi kuwabania

Hizo ndio changamoto zenu na naomba sana msivunjike moyo

A challenge to you; wekeni ahadi yoyote ile muone CCM na serikali watakavyohamanika kuitimiza ili waonekane wamefanya kitu... do that for bombs victims
 
Ni kweli Pokola, tatizo kubwa lililopo sasa ni kila unit imekua defensive na wanashindwa kukaa chini na kukubali kwamba janga halina chama wala itikadi ya kisiasa

I hope wananchi watapata bahati ya kuelewa na kutofautisha siasa na haki za kila siku za huduma za jamii na majanga
 
Tujuze mkuu CDM wamewasaidia vipi wahanga?media imewabania hebu tupe news wale tusiokuwepo Dar.
 
Ah ccm kumbe ndo walivyofanya, jaman hata magazeti sijaona maswala ya cdm yakisomeka. Msikate tamaa tupo pamoja.
 
Hata wafanye vipi, Ipo siku tutajua mwelekeo wetu, Siwezi sema sisi ni wajinga ila we shall have to redefine and find our destiny! kudadadek Raia tunaungua humu tz
 
namtumia PM Kitila aje atujuze zaidi kwani mimi si msemaji wa CDM wala CCM.... ila kwa community yetu tumeweza kutoa damu, nguo na pesa kupitia shirika lisilo la kiserikali

Jumanne tunakwenda Majole kuangalia kama tunaweza add any value...
 
CDM wameshiriki, siyo lazima vyombo vya habari viandike.
 
Tumeona mlivyojitolea kusaidia waathirika wa Gongo la Mboto na jinsi media yetu na serikali zinavyojitahidi kuwabania

Hizo ndio changamoto zenu na naomba sana msivunjike moyo

Kama vyombo vya habari vimewabania mbona na wewe pia unaungana navyo kuibania Chadema?? ebu eleza jinsi ilivyowasaidia Wahanga hao ili nasi tufahamu.
 
Kama vyombo vya habari vimewabania mbona na wewe pia unaungana navyo kuibania Chadema?? ebu eleza jinsi ilivyowasaidia Wahanga hao ili nasi tufahamu.
soma post number saba
 
Kwanza mie nahisi kichefuchefu na huyu farisayo wanayemuita spika wa bunge,mambo yake ya kuilinda sisiemu mbele ya maslahi ya taifa, tumuombee mjaa na majanga. Amen
 
soma post number saba

Umeeleza taarifa ya NGO moja kutoa misaada lakini bado haujaeleza Chadema imefanya nini kuwasaidia hao Wahanga mpaka isitangazwe ata na gazeti la Tanzania Daima.

namtumia PM Kitila aje atujuze zaidi kwani mimi si msemaji wa CDM wala CCM.... ila kwa community yetu tumeweza kutoa damu, nguo na pesa kupitia shirika lisilo la kiserikali

Jumanne tunakwenda Majole kuangalia kama tunaweza add any value...
 
Kwanza mie nahisi kichefuchefu na huyu farisayo wanayemuita spika wa bunge,mambo yake ya kuilinda sisiemu mbele ya maslahi ya taifa, tumuombee mjaa na majanga. Amen

nimependa ulivyomuita huyo mama MFARISAYO. Hakika ni mfarisayo na mpinzani wa maendeleo Tz, yeye anajiona anajua kila kiti wkt hamna kitu...
 
Umeeleza taarifa ya NGO moja kutoa misaada lakini bado haujaeleza Chadema imefanya nini kuwasaidia hao Wahanga mpaka isitangazwe ata na gazeti la Tanzania Daima.

ndg yangu Butola hujaelewa kitu gani mbona jamaa kaeleza vizuri tu au unataka malaika ndio waje kukuelimisha?
 
ndg yangu Butola hujaelewa kitu gani mbona jamaa kaeleza vizuri tu au unataka malaika ndio waje kukuelimisha?

Hivi ameeleza nini hapo kitakachotufanya sie tumpe pole Dr. Slaa na Chadema kwa kubaniwa na vyombo vya habari kwa jitihada zao kubwa walizozifanya kuwasaidia Wahanga wa Gongo la Mboto?

Kama umeeleweka kwa maneno haya "aliyoyaeleza hapa" basi tuna tatizo kubwa kuliko tunavyoweza kudhania.
 
Mkuu kusaidia wahanga si swala la publicity. Ili mradi wame fanya wajibu wao kama chama cha siasa kwa jamii yao haija lishi kama wame make headlines or not. Mimi naamini nafsi walizo zigusa kwa misaada waliotoa ni publicty tosha kwani watu walio guswa hawa wezi kusahau na wakisha vuka majaribu haya wata hadithia wenzao. Maybe it's a good thing hawaja tolewa kwenye media ili wajenge grass root support.
 
@Mwanafalsafa nimekusoma vyema sana... lakini kumbuka denial ya info inavyosababisha watu kufanya uninformed decisions

@Butola; uko sahihi kabisa kwa upande wako... nimesema uliyoyasoma na kuonyesha jinsi walivyobaniwa, ila nimezungumzia ya NGO kwani hayo ninaweza kuyasema wani mimi nimdau wa moja kwa moja... Hayo ya CDM mkuu wanabaniwa na ninatumaini kwamba wataleta updates humuhumu

Kama ningekua ni msemaji wa chadema, basi ningesema waliyofanya,

tusubiri wataelezea zaidi, ila wakishindwa hadi kesho, mie ntaweka
 
Mkuu ungesubiri basi mpaka pale utakapoweza kutupatie habari kamili ndio uanzishe thread vinginevyo hakuna maana kuanzisha thread isiyo na taarifa kamili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom