ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
Hay wana jf
Happy Valentine1
Natumai muwazima wa afya tele na mnaendelea vyema na shughuli, kazi,
masomo, biashara na mengineyo ilimradi tu mpate vya kuweka mdomoni;
Siku ya leo nimeonelea niwakumbuke kwa kuwapa furaha ya upendo wa kweli (agape)
watoto wote wa mtaani, yatima, na wajane na bila kuwasahau
ninyi marafiki zangu wa muhimu sana hapa jf
Awali ya yote napenda kuwaambia siku hii maalum huazimishwa kwa
maneno matamu yenye bashasha ya kutakiana heri na fanaka
katika shughuli zetu mmbalimbali, vilevile ni siku ambayo
waweza kuonesha upendo wako kwa wale ambao huko nao na hata
wale ambao hauko nao, yaani ndugu, marafiki, majirani na jamaa.
Cha kushangaza katika dunia yetu hii ya leo watu wameiweka siku hii
kuwa ni siku ya kufanya maasi, uovu, na dhambi zilizopitiliza, wengine wamefanya siku hii
kuwa siku ya kuharibifu wa utu wao, kwa kuendekeza kufanya dhambi ya ngono,
na maasi mengineyo.
Wengi wa wanadamu hawamhofu Mungu wao kwa yale wanayoyafanya,
hawaoni ipo siku ambayo watakuja hesabu yale maovu waliyoyafanya hapa duniani.
Ndugu rafiki mpendwa napenda kukwambia kuwa chochote ufanyacho hapa
duniani hujue kuwa utakuja kukivuna hapo baadaye
kama ulipanda choroko ujue kuwa utavuna choroko, kama ulipanda mema utavuna mema
na kama ulipanda mabaya nayo kwayo utavuna mabaya.
Rafiki jichunguze
UMEPANDA NINI SASA? NA UNATARAJIA KUVUNA NINI SASA?
kama unafanya maovu na kuona uko sawa hauko sawa kabisa.
Ni heri ukamgeukia Mungu wako eo na kuziungama dhambi zako na
kwani yeye ni mwingi wa rehema atakusamehe. Hebu soma Warumi 10:9-11
Nawapenda
na nawatakia sikukuu njema yenye amani, utulivu,
baraka, na furaha tele kwenu marafiki wote wa jf
Pokeeni zawadi hizi za upendo toka kwangu
nazo ni hizi hapa chini