Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Hivi karibuni suala la mgogoro wa kimpaka kati ya Malawi na Tanzania limeibuka Bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda inasemekana ataongoza jopo kwenda Malawi ili kufanya mazungumzo.
Mimi sina imani kabisa na Waziri Mkuu huyu Mizengo Pinda ambaye huwa anaonesha udhaifu mkubwa hasa pale anapobanwa kuhusu hoja aliyoitoa mwenyewe. Kwa mfano kuhusu suala la mauaji ya albino huyu bwana alilia pale Bungeni! Suala la Zanzibar ni nchi au la alilianzisha mwenyewe lakini likamlipukia na kumrudi mwenyewe. Suala la Mahakama ya Kadhi, alidai kwamba kuleta mahakama hizi itakuwa ni kuleta fujo, lakini baada ya muda mchache akakimbia tena kwa mashekhe na kwenda kujisalimisha na kudai kwamba hakuna aliyezuia Mahakama hizi kuanzishwa!
Sasa hivi anataka kuanzisha mazungumzo na Malawi! Sijui ataibua nini huko maskini! This man is too weak for negotiation and I don't trust him! Afadhali hata ya Lowasa ambaye aliiambia Serikali ya Misri kwamba sisi tutaendelea kutumia maji ya Ziwa Victoria bila kujali Mkataba wa Mwaka 1929 kati ya Serikali ya Misri na Serikali ya Tanganyika ambao unataka ruhusa ya Serikali ya Misri kabla ya kutumia maji ya Ziwa Victoria na Mto Nile kwa ujumla. Sijui hapa Pinda wetu angesemaje?
Mimi naona huyu PM aachane na utatuzi wa migogoro kwa kuwa anaonekana ni mnyonge mno kutatua na watamkandamiza tu!
(Tazama Gazeti la Mwananchi)Akijibu hoja hizo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alisema Serikali ya Tanzania inalipa uzito mkubwa suala hilo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ataongoza jopo litakalokutana na wenzao wa Malawi Februari kuanza mazungumzo.