ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,114
- 49,840
Mama anaendelea kufanya Mageuzi ya Kilimo Kwa ku engage private sector Ili kujifanya Tanzania kuwa ghala la chakula Afrika.
Huyu Mwarabu wa Bwawa la Nyerere asizingue kama kule afanye kweli
==============
Tume ya Umwagiliaji imesaini Hati ya Makubaliano na Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji wa bonde la Bugwema katika Ziwa Victoria.
Baada ya kushuhudia utiaji saini, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) amebainisha kuwa mradi huo una jumla ya hekta elfu 30, ambapo kwa awamu ya kwanza utaanza na hekta elfu 10.
Mhe. Waziri Bashe amefafanua kuwa mradi wa Bugwema ni moja kati ya miradi iliyotangazwa Bungeni kuwa itatekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, yaani Public Private Partnership (PPP).