PM Pinda is Too Weak For Negotiation?

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Hivi karibuni suala la mgogoro wa kimpaka kati ya Malawi na Tanzania limeibuka Bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda inasemekana ataongoza jopo kwenda Malawi ili kufanya mazungumzo.
Akijibu hoja hizo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alisema Serikali ya Tanzania inalipa uzito mkubwa suala hilo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ataongoza jopo litakalokutana na wenzao wa Malawi Februari kuanza mazungumzo.
(Tazama Gazeti la Mwananchi)
Mimi sina imani kabisa na Waziri Mkuu huyu Mizengo Pinda ambaye huwa anaonesha udhaifu mkubwa hasa pale anapobanwa kuhusu hoja aliyoitoa mwenyewe. Kwa mfano kuhusu suala la mauaji ya albino huyu bwana alilia pale Bungeni! Suala la Zanzibar ni nchi au la alilianzisha mwenyewe lakini likamlipukia na kumrudi mwenyewe. Suala la Mahakama ya Kadhi, alidai kwamba kuleta mahakama hizi itakuwa ni kuleta fujo, lakini baada ya muda mchache akakimbia tena kwa mashekhe na kwenda kujisalimisha na kudai kwamba hakuna aliyezuia Mahakama hizi kuanzishwa!
Sasa hivi anataka kuanzisha mazungumzo na Malawi! Sijui ataibua nini huko maskini! This man is too weak for negotiation and I don't trust him! Afadhali hata ya Lowasa ambaye aliiambia Serikali ya Misri kwamba sisi tutaendelea kutumia maji ya Ziwa Victoria bila kujali Mkataba wa Mwaka 1929 kati ya Serikali ya Misri na Serikali ya Tanganyika ambao unataka ruhusa ya Serikali ya Misri kabla ya kutumia maji ya Ziwa Victoria na Mto Nile kwa ujumla. Sijui hapa Pinda wetu angesemaje?
Mimi naona huyu PM aachane na utatuzi wa migogoro kwa kuwa anaonekana ni mnyonge mno kutatua na watamkandamiza tu!
 
huyu ni mtoto wa Mkulima kama anavyojinadi mwenyewe na yeye ni mkulima...Huwezi kumlinganisha na Lowasa yeye amekaa ki-bizness zaidi.Si unajua wakulima siku zote hukandamizwa kwa kupangiwa bei duni ya mazao hawana sauti hawa wakulima alwayz.
 
Kaaazi kweli kweli! Huyu bwana atawaambia kwamba "ili kudumisha amani" basi sisi hatuna tone hata moja la maji ya Ziwa Nyasa! Ni afadhali tuwe na mgogoro ambao unatuwezesha kutumia sehemu ya Ziwa Nyasa kuliko kutokuwa na mgogoro ambao utatuwezesha kukosa Ziwa hilo!
 
The guy cannot even negotiate anything with himself, let alone others.
 
teh teh ...anaweza akalia huko malawi nyie ngojeni tu mtakuja kuniambia
 
Hivi karibuni suala la mgogoro wa kimpaka kati ya Malawi na Tanzania limeibuka Bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda inasemekana ataongoza jopo kwenda Malawi ili kufanya mazungumzo. (Tazama Gazeti la Mwananchi)
Mimi sina imani kabisa na Waziri Mkuu huyu Mizengo Pinda ambaye huwa anaonesha udhaifu mkubwa hasa pale anapobanwa kuhusu hoja aliyoitoa mwenyewe. Kwa mfano kuhusu suala la mauaji ya albino huyu bwana alilia pale Bungeni! Suala la Zanzibar ni nchi au la alilianzisha mwenyewe lakini likamlipukia na kumrudi mwenyewe. Suala la Mahakama ya Kadhi, alidai kwamba kuleta mahakama hizi itakuwa ni kuleta fujo, lakini baada ya muda mchache akakimbia tena kwa mashekhe na kwenda kujisalimisha na kudai kwamba hakuna aliyezuia Mahakama hizi kuanzishwa!
Sasa hivi anataka kuanzisha mazungumzo na Malawi! Sijui ataibua nini huko maskini! This man is too weak for negotiation and I don't trust him! Afadhali hata ya Lowasa ambaye aliiambia Serikali ya Misri kwamba sisi tutaendelea kutumia maji ya Ziwa Victoria bila kujali Mkataba wa Mwaka 1929 kati ya Serikali ya Misri na Serikali ya Tanganyika ambao unataka ruhusa ya Serikali ya Misri kabla ya kutumia maji ya Ziwa Victoria na Mto Nile kwa ujumla. Sijui hapa Pinda wetu angesemaje?
Mimi naona huyu PM aachane na utatuzi wa migogoro kwa kuwa anaonekana ni mnyonge mno kutatua na watamkandamiza tu!
Pinda ni mchapa kazi na yuko makini katika maamuzi yake huyo lowasa ni richmund
 
Pinda ni mchapa kazi na yuko makini katika maamuzi yake huyo lowasa ni richmund

Statement yako iko too general! Lowasa alikuwa hatetereki kwenye maamuzi yake na sio kigeugeu kama Mizengo Pinda! Tatizo la Pinda ni kutokuwa na ujasiri! Kiongozi mwingine ambaye alikuwa hatetereki na maamuzi yake ni Nyerere! Wakati wa Vita na Idi Amini Dada Kamuzu Banda aliivamia Tanzania kwa kuleta manowari na ndege za kijeshi na kudai kuwa sehemu yote ya Kyela mpaka milima ya Livingstone ni sehemu ya Malawi! Lakini manowari zile na ndege zilitunguliwa na JWTZ! Hakumwonea mtu aibu, alianzisha uhusiano mzuri sana na Zambia, Zimbabwe na Msumbiji kiasi kwamba Malawi ilijikuta isolated!
 
Nadhani hata ile kauli yake ya kutangaza mali ina utata. Amefanya kazi ikulu for more than 20 years, amekuwa mbunge na Naibu waziri katika kipindi cha mkapa, amekuwa waziri katika kipindi cha JK na pia akawa waziri mkuu.
Sasa anasema hana nyumba ana chumba cha nyumba ya baba yake wakati alikuwa akiishi Dar, aliishi huko maneo kupita ukonga na ana nyumba na mifugo sasa hiyo si nyumba? Je hao mifugo hana pika inayohudumia? Mimi hainiingii akilini kama PM ndiyo anaweza kujivunia kuwa kuwa mtumishi wa umma for those years anashindwa kusave kujenga au kununua gari wakati analipwa allowance nyingi tu na safari za nje nyingi tu zenye per diem za kutosha tu.. Nadhani hapa kuna kasoro katika declaration yake au basi ni mvujaji kwa sababu alikuwa na nafasi ya kufanya saving sana tu kwa maendeleo.... it is a declaration to be looked with a third eye!!!!!
 
Uko sawa kabisa mkuu kwa hii ishu jamaa atashindwa, he is too weak!
 
Uko sawa kabisa mkuu kwa hii ishu jamaa atashindwa, he is too weak!

Huyu PM angepeleka Negotiating Team nyingine inayoongozwa na mtu wa kuaminika! Akienda kuchokoza mambo halafu akashindwa kujitetea atawapa nguvu sana hawa wenzetu!
 
i agree with you this man siku zote nimekuwa simuamini,anaonyesha udhaifu mkubwa sana wa kiuongozi na nadhani he is one of the weakest PMs tuliokuwa nao,PM is a second man in this country lakini yupoyupo,

not suprisingly hawapikiki chungu kimoja na .....................
 
Sioni hoja yoyote ya msingi katika mjadala huu, badala yake naona ni chuki binafsi tu zinaelekezwa kwa PM wetu. Hoja kwamba aliwahi kutoa machozi Bungeni kuhusu mauaji ya Maalbino linahusiana vipi na negotiation katika suala la mpaka wa Malawi na Tz? Hata hizo hoja nyingine hazithibitishi kwamba PM wetu ni weak. Wengi wetu tumezoea kuongozwa na viongozi wenye mbwembwe na maneno mengi ya kutaka sifa, huku wakiliibia taifa kwa njia za ujanja ujanja. Tunataka viongozi waadilifu na Pinda ni mmoja wapo.
 
Kaaazi kweli kweli! Huyu bwana atawaambia kwamba "ili kudumisha amani" basi sisi hatuna tone hata moja la maji ya Ziwa Nyasa! Ni afadhali tuwe na mgogoro ambao unatuwezesha kutumia sehemu ya Ziwa Nyasa kuliko kutokuwa na mgogoro ambao utatuwezesha kukosa Ziwa hilo!

Ziwa Nyasa?! maana ya Nyasa ni ziwa kwa ki-chichewa, malawi wameishaliita Ziwa Malawi - ya kwamba ni alama ya taifa lao. TZ mnaita Ziwa nyasa yaani ziwa ziwa.

Pinda anatakiwa kuwa strong kwa hili. mipaka lazima iwe kama ya maziwa mengine na kama ilivyo kwa ziwa nyasa upande wa msumbiji. That should be his stand.
 
Sioni hoja yoyote ya msingi katika mjadala huu, badala yake naona ni chuki binafsi tu zinaelekezwa kwa PM wetu. Hoja kwamba aliwahi kutoa machozi Bungeni kuhusu mauaji ya Maalbino linahusiana vipi na negotiation katika suala la mpaka wa Malawi na Tz? Hata hizo hoja nyingine hazithibitishi kwamba PM wetu ni weak. Wengi wetu tumezoea kuongozwa na viongozi wenye mbwembwe na maneno mengi ya kutaka sifa, huku wakiliibia taifa kwa njia za ujanja ujanja. Tunataka viongozi waadilifu na Pinda ni mmoja wapo.

Sasa akibanwa akalia au kubadili maamuzi, uadilifu wake unasaidia nini hapa? Hakuna chuki binafsi, tumetoa na data kuonesha kwa nini haaminiki kwenye negotioations! Hana bold spirit, he is timorous in his spirit! Nilitoa mfano wa JK Nyerere ambaye alisimama kidete kuutetea mpaka wetu na Malawi na Lowasa juu ya Maji ya Ziwa Victoria! Hayo ya ujanja ujanja na kuliibia taifa letu kama yapo mimi siyatetei na kuyakubali kwamba ni mazuri! Ninachozungumzia ni ujasiri, ambao Mtoto wa Mkulima Pinda hana!
 
pinda is just pinda!...its not easy to change things that have been built for years..butr ya right pindais working under someone's tension!...so sometimes he is not himself!....
 
pinda is just pinda!...its not easy to change things that have been built for years..butr ya right pindais working under someone's tension!...so sometimes he is not himself!....

Really?
 
Mhe. PM ni m deplomasia mno kuliko Papa!..pengine shida ipo kwenye "negotiation skills" Liliongelewa hilo kwenye Taarifa ya Dr. Mwakyembe kuhusu Richmond kuwa watumishi wengi wa umma, hopeful PM inclusive, hawana taaluma ya "majadiliano". Aidha, uzoefu waonyesha kuwa wengi ya watumishi waliofanya kazi Ikulu huwa ni kama wafuasi wa YESU Mnazareti, wao kila kitu ni "YES, YES.." hata kama panasitaili "BIG NO.." nidhamu yao ni kama ya gheshi, hakuna kubishana na Afande!
 
Hii kali!
 
Mkuu Buchanan sikubaliani na vigezo vyako ulivyotumia ili kuhitimisha hoja yako kuwa Pinda ni dhaifu katika kusimamia maamuzi/ukweli. Hata mafisadi wameshatufisadisha akili zetu na kuwaona kuwa ni watu wenye msimamo katika hoja zao za kuwafisadi watanzania. Ningekubaliana nawe kama ungefanya tathmini ya wajumbe wa jopo atakaloongozana nao. Hao ndio waliotakiwa kuwa na 'negitiation skills' kuliko Pinda. Yeye anakwenda kama Waziri Mkuu na atajadiliana na waMalawi kulingana na ushauri atakaopewa na wataalamu wa jopo lake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom