Please msaada tena

miss nora

Member
Mar 25, 2011
13
7
Jamanni nimerudi tena na matatizo yangu,,hili janaume linataka roho yangu sasa, coz anafika mbali mpaka wageni na ndugu zangu sasa anawatongoza..me nimefika mwisho, nishaurini tena,, nafikiria kuachana nae lakini nitaanzia wapi maisha na ukiangalia nasimamia biashara zetu . lakini sasa natafuta jinsi ya kuishi nae katika hii situation. Umalaya wke nimeushuhudia sana na hata nikimkamata na sms or emails, hajali anazikana na ushahidi ukiwa wazi anasema sielew usemacho, naweza kumfanyia uhuni wa mwaka lakini nikifikiria tulipotoka namuhurumia coz tumefight sana mpaka hapa tulipo nitakuwa pia nimemwaribia future zake.
Hapa jirani na nyumbani kuna kaka mmoja ambae kwa jinsi alivyonieleza familia yake ipo mkoa mwingine. Yeye yupo huku kikazi ana kama mwaka mmoja,kiukweli huyu kaka anaonyesha kunijali sana japo hajanitamkia chochote ila anaonyesha kunijali coz mara nyingi ananialika lunch sometimes outing na zawadi. lakini hajanitamkia lolote na wala mimi sijamweleza matatizo niliyonayo kwenye ndoa yangu.
Wanawake wenzangu nishaurini nijiingize katika mahusiano na huyu kaka tupeane kampany ili maisha yangu ya ndoa yaendelee niwe na mtu wakumfikiria niachane na kumfatilia huyu baba au nifanyeje ili nihandle --- hii life style?? Coz mume ndo hivyo kawa fataki, siwezi kumbadilisha hata kidogo.leo asubuhi kanishusha bara barani nikatembea kwa mguu mpaka kazini kisa naongea na simu na mama yangu mdogo hataki niongee na ndugu zangu wala niwe na marafiki.

Roho ya Umalaya inakuandama wewe!! Ingia kwenye maombi fasta. ili uponye ndoa yako......... we endelea kumuentertain huyo kijana wako jamaa akijua imekula kwako mzima best. kuwa makini

Heeeee huyo mume au balaa,hataki uongee na watu umekuwa kisiwa wewe duh, kwa kweli mambo ni ya shingo mie nakushauri uongee na watu wazima wamuonye, coz unaweza kuwa na huyo jirani pia ukapata mabalaa tu, hiyo sio njia nzuri ya ku handle matatizo yako ya ndoa, ukishindwa kabisa na bado anaendelea na uhuni uliokithiri mwambie umeshindwa, kaanze maisha mapya

ña mwanamke inakula kwako mbaya sana ukifumwa, bora aondoke akiona hatari ya ukimwi inakuja,coz huyo baba si mstaarabu,hadi ndugu anatongoza jamani! maombi yanahitajika tena ya kufunga kabisa
Roho ya Umalaya inakuandama wewe!! Ingia kwenye maombi fasta. ili uponye ndoa yako......... we endelea kumuentertain huyo kijana wako jamaa akijua imekula kwako mzima best. kuwa makini

Do what's best for you,huyo mume wako,hawezi kuacha mpaka aamue yeye mwenyewe,ila sio kwa kuambiwa na watu.dunia ya leo mambo ya kuishi kwa ajili ya kitu au watu,siyo kabisa.Angalia uzuri na ubaya halafu amua unavyo amua.kwa mwanamke akifanya,ataitwa malaya,kwa m.me ni dumbe la mbegu,ukimwi ukiingia ndani atalaumiwa nani?kisa mavumilivu?

Pole sana kwa matatizo ulikua nayo lakini mbona hujaelekea kama ukotayari kuamua au niseme umeshayazowea unayaona yakawaida?
Mume kama hajieshumu mara leo kamfungulia zipu huyu kesho yule na wewe unajua sio mara moja wala mara2,vithibitisho unavyo sasa unasubiri nini ukimwi? au ukisema utaanzia wapi maisha unamanisha ukotayari kufa sababu huna pakuanzia? shosti ebu fikiria tena kama unapenda maisha yako
anza kujipanga, unaweza kumfanyia uhuni wa mwaka lakini utamuaharibia future,kwani kuchukua chako au mkigawana mali kuna ubaya? kupoteza muda na huyo kaka wala hakukufanyi ukasahau madhila anayokufanyai mumeo,utakua nae mchana usiku ukonamumeo faida iko wapi?
fikiria maisha yako na afya yako na kama uko na watoto ndio kabisa wala usijaribu kufanya huo uzinzi sababu kutakua hakuna tofauti baina ya wewe na mumeo.

dahhh i kali....imenizidi kimo....pole lakin...NJE USIDONYOE TAFADHALI..itakula kwako

ubaya aumalizwi kwa ubaya...zungumza na watu wazima wampe A-Z yake.

.....NJE USIIIPELEKE IYO KITU MUNGU APEND..UENDA mme wako ana mapepo tu/kitu kinamsumbua..urimbuken ivi now ana ela zaman alikuwa hana so ndo anachacharika nw aonekane kidume...tak t easy ..

.we mkristu?nenda kansani waambie viongozi wako watakupa njia sahihi ya kumuendo mmeo..

.dah lakini hii ngumu kumeza...pole shost LAKIN NJE USTOKE...uyo shetan tu anakuvuta kwa kumtumia jiran apo ili uone ahaaa uyu ananipenda..full zawad fullcare..wakat huo kamfunga mmeo askupende wala asikujali naumalaya A ...sasa wewe ukikubali kumuuunga mkono shetan kwa kujiingiza kwenye kitanz chake itakula kwako ...shetan yupo kwenye harakat za kuharibu ndoa yako...kuwa makini...pga got dada....ahh swaga iz apetite ya kuolewa inasepa kabsa cz leo anajifanya malaika kesho akawiii kugeuka shetwan...

Jamanni nimerudi tena na matatizo yangu,,hili janaume linataka roho yangu sasa, coz anafika mbali mpaka wageni na ndugu zangu sasa anawatongoza..me nimefika mwisho, nishaurini tena,, nafikiria kuachana nae lakini nitaanzia wapi maisha na ukiangalia nasimamia biashara zetu . lakini sasa natafuta jinsi ya kuishi nae katika hii situation. Umalaya wke nimeushuhudia sana na hata nikimkamata na sms or emails, hajali anazikana na ushahidi ukiwa wazi anasema sielew usemacho, naweza kumfanyia uhuni wa mwaka lakini nikifikiria tulipotoka namuhurumia coz tumefight sana mpaka hapa tulipo nitakuwa pia nimemwaribia future zake.
Hapa jirani na nyumbani kuna kaka mmoja ambae kwa jinsi alivyonieleza familia yake ipo mkoa mwingine. Yeye yupo huku kikazi ana kama mwaka mmoja,kiukweli huyu kaka anaonyesha kunijali sana japo hajanitamkia chochote ila anaonyesha kunijali coz mara nyingi ananialika lunch sometimes outing na zawadi. lakini hajanitamkia lolote na wala mimi sijamweleza matatizo niliyonayo kwenye ndoa yangu.
Wanawake wenzangu nishaurini nijiingize katika mahusiano na huyu kaka tupeane kampany ili maisha yangu ya ndoa yaendelee niwe na mtu wakumfikiria niachane na kumfatilia huyu baba au nifanyeje ili nihandle --- hii life style?? Coz mume ndo hivyo kawa fataki, siwezi kumbadilisha hata kidogo.leo asubuhi kanishusha bara barani nikatembea kwa mguu mpaka kazini kisa naongea na simu na mama yangu mdogo hataki niongee na ndugu zangu wala niwe na marafiki.

Anakujali tu kwasababu anakualika lunch na kukupa zawadi,.....anakutega huyo,...fungua kichwa,.....anyway driving desire is as your desire is,...mimi simo kwenye hili

Pray n Pray n Pray...
Ukizini akakufuma atakuacha na kila kitu unachodhani mmefight naye utavipoteza...
Tulia, keep yourself busy, endelea kusali

Sijui ni kwa nini ummeomba msaada kwa wanawake pekee!
Mimi najipendekeza......yaelekea kinachokufanya uendellee ktulia kwa huyu mwanaume si upendo .Kinachokuweka hapo ni vitu material,au roho ya utegemezi iliyovuka mipaka .Pole sana ni hatari kuishi na mtu kama humpendi kwa kiwango hicho!Ushauri wangu ufuate moyo wako !

jamani,mume ana mwanake,sali muombe mungu,unaomba weeee,baadae mume yule mwanamke wa mwanzo amemuacha,amepata mwengine,muombe mungu,unaomba.mume siku hizi kawa mlevi,muombe mungu unaomba ataacha,unaomba.mume amezaa na mfanyakazi mwenzake,unaambiwa muombe mungu,unaendelea kuomba.

Mume huyo huyo,kamtongoza house girl,unataka ushauri,unaambiwa mfukuze house girl,na wewe endelea kuomba,unaendelea kuomba,dada wa kazi unamtimua.mume amezaa na bar maid,bar maid anakuletea mtoto nyumbani kulea huyo mtoto hataki,unampokea mtokea mtoto unamlea kama wako,unaomba ushauri,unaambiwa wewe endelea kuomba,unaomba weee.mwisho wa yote mume anakuletea ukimwi ndani,unaanza kuumwa,bila ya kwenda kupima unajishuku kuwa unao tu,juu ya vitendo vya mume wako,unapima ni positive,mawazo yanakufanya huishi muda unachukuliwa na ndugu unauguzwa.

Hiki ni kisa cha kweli,ni dada yangu baba mmoja mama mmoja,ambae tumeshamzika,na aliniusia vitu ambavyo kwa upande wangu mimi kuomba nitaomba ila sitokuwa weak kukaa kusubiri mwisho wa yote unaishia mbaya,saa nyengine ni vizuri kujua mapungufu yetu katika relationship,jaribu ku solve hayo matatizo,ila kama haya utatuzi na umeshajaribu vya kujaribu,ni bora ku move on

Mambo mengine yapo wazi mno, sitaki kuamini kwamba hii nayo inahitaji maombi.

Give that a--hole the reason to be envious, for phuck sake!

Nakubaliana na ushauri wa kuomba. Pamoja na hayo, weka vikao na wakubwa zake ...Wazazi, Viongozi wa kiroho.... Mpe ABC zake... Hataki/Habadiliki Lianzishe. Hayo ya huyo tena mwenye familia yake linaonekana ni pepo la ngono alilonalo mumeo huenda linaambukiza na sasa linataka kutua kwako.

Sijui ni kwa nini ummeomba msaada kwa wanawake pekee!

Mimi najipendekeza......yaelekea kinachokufanya uendellee ktulia kwa huyu mwanaume si upendo .Kinachokuweka hapo ni vitu material,au roho ya utegemezi iliyovuka mipaka .Pole sana ni hatari kuishi na mtu kama humpendi kwa kiwango hicho!Ushauri wangu ufuate moyo wako !

umemwambia neno la maana, afuate matakwa ya moyo wake, kwani hatimaye ni yeye ndiye atawajibika iwe kwa zuri ama baya, kuhusu ushauri akumbuke kuwa mshauri ajapotoa wa mzuri asipolenga matamanio ya ashauriwaye basi ni heri kulishauri jiwe maayu!

Jamani eeenh kila kiapo cha KWENYE SHIDA NA RAHA, sasa hapo upo kwenye SHIDA, usikimbie vumilia, sababu uliapa hata kwenye shida wewe utamvumilia tuu!! sasa shida za huyo jamaa ni hilo la kula kila anachokiona mbele yake! huyo kaka anaekujali unajuaje km ni mzima? angalia utaruka mkojo ukakanyage mavi, KM ni mmeo kaa nae chini muelimishe, usiishie kumsema tu na kumtukana!!

endelea kukaa na huyo mwanaume mpaka atembee na ndg zako,atembee na majirani, atembee na mabarmaid halafu akuletee ukimwi. Maana unashindwa kufanya maamuzi magumu ya maisha yako.

Sijui ni kwa nini ummeomba msaada kwa wanawake pekee!

Mimi najipendekeza......yaelekea kinachokufanya uendellee ktulia kwa huyu mwanaume si upendo .Kinachokuweka hapo ni vitu material,au roho ya utegemezi iliyovuka mipaka .Pole sana ni hatari kuishi na mtu kama humpendi kwa kiwango hicho!Ushauri wangu ufuate moyo wako !

ABSOLUTELY? UTEGEMEZI NDO UNAOMWEKA KWA HUYO MUMEWE

Maskini kama nakuona vile...... Pole sana lakini una acha penye nafuu na kutaka kuionja adha ya dunia, (hujawahi kukaa chumbani ukabubujikwa na machozi yasiyokifani eeeeh?) hakika utajuta sababu ni kwamba wanawake wote wanaoachika ki bifu hawadumu huko waendako, nikimaanisha kwamba huyo mwanamme anataka kujua ulivyo umbwa na siyo kuku hifadhi rohoni daima.

Pia imejengeka kwa baadhi ya mawazo ya wanaume kwamba endapo amekupata baada ya ww kuachika huwa anakuchunguza zaidi kujua kwa nn uliachika, hivyo hata kama ukafanya kosa la kawaida tu yeye anaanza ku relatisha kama ndo tabia zilizomshinda mme mwenzake juu yako. Hapa tunashauri tu unaweza kuudelete huu ushauri wangu na ku utupa dampo then ukaendelea na maamuzi yako.

Hapa jirani na nyumbani kuna kaka mmoja ambae kwa jinsi alivyonieleza familia yake ipo mkoa mwingine. Yeye yupo huku kikazi ana kama mwaka mmoja,kiukweli huyu kaka anaonyesha kunijali sana japo hajanitamkia chochote ila anaonyesha kunijali coz mara nyingi ananialika lunch sometimes outing na zawadi. lakini hajanitamkia lolote na wala mimi sijamweleza matatizo niliyonayo kwenye ndoa yangu.

Nahisi justification ya usaliti
Ila pole sana dada , lakini kosa halisahihishwi kwa kosa

Miss Nora katika post yako what caught my eye ni wewe kufikiria kutoka nje...
Amini usiamini ukifanya hivo - itakuja julikana na wee ndo utaonekana malaya
kuliko hata huyo mme... be careful katika his sector ya kutoka nje mwanamke
mara nyingi turns out to be the looser...

Similar Discussions

Back
Top Bottom