Kigugumizi (Stuttering): Chanzo na Tiba kwa watu wazima na watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigugumizi (Stuttering): Chanzo na Tiba kwa watu wazima na watoto

Discussion in 'JF Doctor' started by Pape, Nov 15, 2009.

 1. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Habari wanaJF,

  Kuna mdogo wangu ana tatizo la kigugumizi cha kuongea kiasi kwamba hawezi kuzungumza bila kujipigapiga au kuruka!!Ningependa kujua chanzo cha tatizo hili na pia tiba yake kama ipo!!

  Naomba kuwasilisha!!

  mkada said,
  Habari wana JF,

  Nina mtoto wangu first born ana miaka minne sasa,alianza kuwa na kigugumizi toka akiwa ameanza kujifunza kuongea,akiwa na miaka mitatu niliona kama kinazidi,nikaamua kuwaona wataalam na madaktari wa magonjwa ya watoto,na majibu niliyopata ni kwamba kwa kuwa bado ni mtoto nisubiri kidogo kitaisha tu kikizidi nirudi tena kuna dawa, sasa ni mwaka wa nne na naona kama kinazidi.

  Mwezi huu nikaamua kwenda kwa Dr therapist mwingine na jibu aliloniambia ni kuwa stutterers (watu wenye kigugumizi) ni watu wenye akili sana kiasi kwamba akili yako inafanya kazi haraka kuliko midomo, kwamba midomo haiwezi ni ku copy na akili.Hapo Dr ndo akanichanganya kabsa,coz kwa maelezo yake mimi nahisi ni tatizo hilo,lakini yeye anasisitiza kuwa tena stutterers wana high IQ than average.

  Kuhusu dawa kanishauri nisitumie dawa yoyote zaidi ya therapy, kutokumuudhi, watoto wenzie kutokumcheka, mazingira mazuri ya kuongea au kutokumkalipia, kwani alisema kwa sasa hakuna dawa zinazotibu, na dawa maarufu iliyo za anti-convulsants, anti-depressants, antipsychotic and antihypertensive medications, and dopamine antagonists ni ziko kwenye majaribio tu.

  Am kind of confused please kama kuna watu wana hii experience nitashukuru sana mchango wao ili niwe na amani na mtoto wangu, manake siku hizi kuongea ni mpaka apige mguu chini yaani mpaka namwonea huruma mtoto wangu.

  -------- Michango--------
  lahabi said,
  Usiwe na shaka sana ndugu hali hiyo inawezakwisha automatically, nami ni muathirka wa hili. Nakumbuka nikiwa mdogo binamu yangu wa kike alikuwa ni mzuri kwa umbo pia alikuwa na kigugumizi na aliongea kwa mkato mkato. Mie kwa akili za utoto nikavutiwa sana na hali ile. Nikaiga kila alivyokuwa anaongea, baadae nami nikawa na kigugumizi kikubwa(cha kujitakia kabisa).

  ATHARI:
  1. Hujenga hali ya kutojiamini kwa muathirika hii inatokana na kunyimwa nafasi ya kujieleza ya kutosha kutokana na kutumia muda mwingi katika kutamka maneno.
  2. Huwa na asira za mara kwa mara kwa kuhisi kuwa anapuuzwa.
  3. Anapokuwa kwenye excitiment yeyote/planning for response(anapotumia muda mwingi kujiandaa kuelezea kitu cha baadae huwa taabu kwelikweli nk)

  NOTE: Binafsi hivi sasa naichukia sana hali hii.

  MAMBO YA KUFANYA:
  1. Mzazi/Mlezi mpe nafasi ya kutosha kijana wako ya kujieleza japo atatumia muda mrefu(hii hutufanya tuhisi tunathaminiwa)
  2. Usimkate kilimi anapoongea.
  3. Kama inawezekana anapoongea usimpuuze mkazie macho hadi atapomaliza kuongea.
  4. Kama itatokea akashindwa kutaja baadhi ya maneno kwa wale wenye kigugumizi kikali na kupiga ngumi ukutani/mguu chini msaidie katika kutamka maneno husika.
  5. Mpe muda mrefu sana wa kuongea au kuimba mf: kwaya kanisani/kaswida msikitini nk kuliko kukaa kimya.
  Siku zote mshauri kuongea taratibu kwa kupumzika, anapokuwa na hasira/furaha ya ghafla asiongee hadi hasira/furaha ishuke.
  6. Asichekwe anapoongea kwani hali hii humfanya kukaa kimya muda mrefu hatimae hali huwa mbaya zaidi.

  TAHADHARI:
  Kigugumizi ni chepesi kweli kweli kuigika, kama utaona watoto wadogo wanajaribu kumuiga mtu yeyote wa karibu mwenye kigugumizi waeleze kwa upole na mara kwa mara madhara yake.

  NINA HUSHUHUDA KWA HILI: Jirani yangu mmoja alikuwa na kigugumizi kikali na wadogo zake wawili wakatokea kumuiga kaka yao, hivi sasa wote watatu wameathirika kwa hilo. Ahsante.

  -----
  No. 2
  Jinsi ya Kukabiliana na Kigugumizi

  "Ninaposhikwa na kigugumizi, mimi huwa na wasiwasi, na hilo hunifanya niwe na kigugumizi hata zaidi. Ni kana kwamba nimo ndani ya shimo refu na siwezi kutoka. Wakati mmoja nilienda kumwona mwanasaikolojia fulani. Aliniambia kwamba ninahitaji kuwa na rafiki wa kike-nifanye ngono ili nijiheshimu zaidi! Bila shaka sikurudi tena kwake. Ninataka tu watu wanikubali jinsi nilivyo."-Rafael, mwenye umri wa miaka 32.

  HEBU wazia hali ingekuwaje ikiwa kununua tu tiketi ya basi kungekufanya utokwe na jasho, na unapozungumza mara nyingi unashindwa kukamilisha maneno fulani na unajirudia-rudia. Watu milioni 60 hivi ulimwenguni pote, yaani mtu 1 kati ya watu 100, wanakabili hali hiyo kwa sababu wana kigugumizi. Mara nyingi, wao hudhihakiwa na kubaguliwa. Hata huenda wakaonwa kuwa wajinga kwa sababu wao hubadili maneno magumu na kutumia rahisi ambayo wanaweza kutamka.

  Ni nini husababisha kigugumizi? Je, tatizo hilo linaweza kutibiwa? Mtu mwenye kigugumizi anaweza kufanya nini ili kuboresha ufasaha wake?* Watu wengine wanaweza kusaidia jinsi gani?

  Je, Tunajua Kisababishi?

  Watu fulani walioishi nyakati za kale waliamini kwamba kigugumizi kilisababishwa na roho waovu ambao walihitaji kuondolewa. Wakati wa Enzi za Kati, watu walidhani kwamba ulimi ndio uliosababisha kigugumizi. Kwa hiyo, walitumia "dawa" gani? Vyuma vyenye moto na vikolezo! Katika karne zilizofuata, madaktari wapasuaji walikata mishipa na misuli ya ulimi na hata kuondoa tezi za kooni ili kutibu kigugumizi. Lakini njia hizo zote hazikufua dafu.

  Utafiti wa kisasa unaonyesha kwamba huenda kigugumizi kikasababishwa na mambo kadhaa. Kisababishi kimoja kinaweza kuwa jinsi mtu anavyotenda anapokuwa chini ya mkazo. Huenda pia mtu akarithi tatizo hilo, kwa kuwa asilimia 60 hivi ya watu walio na kigugumizi wana watu wa ukoo walio na tatizo hilo. Isitoshe, eksirei za mfumo wa neva zinaonyesha kwamba ubongo wa mtu mwenye kigugumizi huchanganua lugha katika njia tofauti. "Huenda watu fulani wakaanza kuzungumza kabla ya ubongo wao kuwaambia jinsi maneno yanavyopaswa kutamkwa," anasema Dakt. Nathan Lavid katika kitabu chakeUnderstanding Stuttering.*

  Hivyo, kigugumizi si tatizo la kiakili hasa kama ilivyodhaniwa hapo awali. Kitabu No Miracle Cures kinasema hivi: "Kigugumizi si tatizo linalosababishwa na ukosefu wa ujasiri, na huwezi kumchochea mtu aache kugugumiza." Hata hivyo, watu wenye kigugumizi wanaweza kuwa na matatizo ya kihisia kwa sababu ya hali hiyo. Kwa mfano, huenda wakaogopa hali fulani kama vile, kuzungumza hadharani au kwenye simu.

  Msaada kwa Walio na Kigugumizi

  Jambo la kushangaza ni kwamba watu wenye kigugumizi wanaweza kuimba, kunong'ona, kujizungumzia au kuzungumza na wanyama wao vipenzi, kuzungumza wakati uleule na wengine, au kuwaiga wengine bila tatizo lolote. Isitoshe, asilimia 80 ya watoto wenye kigugumizi huacha kuwa na tatizo hilo bila kutibiwa. Namna gani hiyo asilimia 20 inayosalia?

  Leo kuna matibabu ya kuwafunza watu kuzungumza kwa ufasaha zaidi. Mbinu fulani zinahusisha kulegeza taya, midomo, na ulimi na kupumua kutoka kwenye kiwambo. Pia wagonjwa wanaweza kufundishwa kuvuta pumzi kwa kiasi kidogo kutoka kwenye kiwambo na kisha kupumua polepole wanapozungumza. Pia, wanaweza kutiwa moyo kuvuta vokali na konsonanti fulani wanapozungumza. Mgonjwa huanza kuzungumza haraka kadiri ufasaha wake unavyoboreka.

  Mtu anaweza kujifunza ustadi huo kwa saa chache tu. Lakini kutumia mbinu hizo kwa mafanikio chini ya hali zenye mkazo sana huenda kukahusisha kufanya mazoezi kwa saa nyingi sana.

  Mazoezi hayo yanapaswa kuanza mtu akiwa na umri gani? Je, inafaa kungoja hadi mtoto aache tatizo hilo bila msaada wowote? Takwimu zinaonyesha kwamba watoto wasiozidi asilimia 20 hupona bila msaada hata ikiwa wamekuwa na kigugumizi kwa miaka mitano. "Kufikia umri wa miaka sita," kinasema kitabu No Miracle Cures, "yaelekea mtoto hawezi kupona tatizo hilo bila msaada."

  Hivyo, "watoto walio na kigugumizi wanapaswa kupelekwa kwa mtaalamu wa usemi na lugha haraka iwezekanavyo," kitabu hicho kinaongezea. Kati ya asilimia 20 ya watoto ambao huendelea kuwa na kigugumizi hata wanapokuwa watu wazima, inakadiriwa kwamba asilimia 60 hadi 80 kati yao hupona wanapopata msaada wa kuwasaidia kuzungumza kwa ufasaha.*

  Ona Mambo Kihalisi

  Mtaalamu wa usemi Robert Quesal, ambaye pia ana kigugumizi, anasema kwamba chini ya hali zozote zile, mtu mwenye kigugumizi hapaswi kujiwekea mradi wa kuzungumza kwa ufasaha kabisa. Rafael, ambaye alitajwa mwanzoni mwa habari hii, hajafaulu kushinda tatizo hilo kabisa, ingawa ameboresha ufasaha wake.

  Anasema hivi: "Ninakuwa na kigugumizi zaidi ninaposoma au kuzungumza mbele za watu au ninapokuwa na mtu wa jinsi tofauti ambaye ni mrembo. Nilikuwa mtu mwenye wasiwasi sana kwa sababu watu walinidhihaki. Hata hivyo, siku hizi, nimekubali hali yangu na sijifikirii sana. Sasa neno fulani likinifanya nishikwe na kigugumizi, nyakati nyingine mimi hucheka, kisha ninajaribu kutulia na kuendelea kuzungumza."

  Maneno hayo ya Rafael yanapatana na maelezo ya Shirika la Kuzuia na Kutibu Kigugumizi la Marekani kwamba "kushinda tatizo la kigugumizi mara nyingi huhusisha kushinda woga wa kuwa na kigugumizi badala ya kujitahidi sana kuacha kugugumiza."

  Watu wengi hawajaruhusu tatizo hilo liwazuie kuwa na maisha yenye kusudi. Hata baadhi yao wamekuwa watu mashuhuri kama vile, mwanafizikia Sir Isaac Newton, mwanasiasa Mwingereza Winston Churchill, na mwigizaji Mmarekani James Stewart.

  Wengine wamejifunza ustadi ambao hauhusishi kuzungumza, kama vile kucheza ala fulani, kuchora, au kujifunza lugha ya ishara. Watu wanaozungumza bila kugugumiza wanapaswa kuthamini jitihada nyingi za wale walio na kigugumizi. Hivyo, na tuwatie moyo na kuwategemeza kadiri tunavyoweza.

  Zaidi ya asilimia 80 ya watu walio na kigugumizi ni wanaume.

  Ingawa maoni mbalimbali kuhusu visababishi na matibabu yanayofaa ya kigugumizi yanafanana, hayapatani nyakati zote. Gazeti Amkeni! halipendekezi maoni au matibabu yoyote hususa.

  Katika visa fulani, huenda wataalamu wakapendekeza kifaa fulani cha kuzuia kigugumizi ambacho hufanya sikio lichelewe kusikia.

  UNAWEZA KUMSAIDIA JINSI GANI MTU ALIYE NA KIGUGUMIZI?

  ● Msaidie atulie, na kustarehe. Maisha ya leo yenye hekaheka nyingi na mkazo mara nyingi hufanya tatizo hilo liwe baya zaidi.

  ● Badala ya kumwambia mtu mwenye kigugumizi azungumze polepole, mwekee mfano kwa kuzungumza polepole. Msikilize kwa subira. Usimkatize. Usimalizie sentensi anazosema. Tua kabla ya kujibu.

  ● Epuka kumchambua na kumrekebisha. Onyesha kwamba unapendezwa na anachosema kwa maneno yako, kwa kumtazama, na kwa ishara zako za uso na mwili. Usikazie fikira jinsi anavyozungumza.

  ● Hupaswi kuogopa kuzungumzia tatizo lake. Kutabasamu kwa njia ya kirafiki na kuzungumzia tatizo lake, kutamsaidia mtu mwenye kigugumizi kujihisi huru. Huenda ukasema: "Nyakati nyingine si rahisi kusema tunachotaka kusema."

  ● Zaidi ya yote, mhakikishie kwamba unamkubali jinsi alivyo.

  "POLE KWA POLE NILIACHA KUWA NA KIGUGUMIZI"

  Víctor, ambaye amekuwa na kigugumizi kwa miaka mingi wakati familia yao ilipopatwa na mkazo mwingi, alishinda tatizo hilo bila matibabu yoyote. Akiwa Shahidi wa Yehova, alijiandikisha kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi, ambayo hufanywa kila juma katika kila kutaniko. Ingawa shule hiyo haijakusudiwa kutoa matibabu ya usemi, imewasaidia wanafunzi kuboresha uwezo wa kuzungumza na kupata ujasiri.

  Kitabu Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi hutumiwa katika shule hiyo. Chini ya kichwa, "Kukabiliana na Kigugumizi," kitabu hicho kinasema: "Ni muhimu kuendelea kujaribu. . . . Kama una mgawo wa kutoa hotuba, tayarisha vizuri. Fikiria sana jinsi utakavyoitoa. . . . Ukikwama unapoongea, jaribu kwa kadiri unavyoweza kudumisha utulivu wa sauti yako na hali yako. Legeza misuli ya utaya wako. Tumia sentensi fupi-fupi. Epuka kutumia maneno kama ‘mmh' na ‘eeh.'"

  Je, shule hiyo ilimsaidia Víctor? Anasema hivi: "Kukazia fikira kile ambacho ningesema, na si jinsi ambavyo ningezungumza, kulinifanya nisahau kwamba nina tatizo. Pia, nilifanya mazoezi sana. Pole kwa pole, niliacha kuwa na kigugumizi."

  VIDEO
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Pole sana.
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kusikia dawa, lakini kuna device fulani unaivaa sikioni inawasaidia baadhi ya watu.

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=HuO3DbnQjxE[/ame]

  http://www.speecheasy.com/index.php
   
 4. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Chukua hatua ya imani mwombe Mungu maana kwake hakuna kisichowezekana
   
 5. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  better this way
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  amen
   
 7. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh! naona watu hapa wanafanya utani kwa sababu hawajui ni jinsi gani mtu mwenye kigugumizi anavyo jisikia pale anapo shindwa kutamka maneno kiusahihi....Me pia nina sumbuliwa na tatizo hili,kwenye ukoo wetu karibu wote tuna sumbuliwa na tatizo hili.
   
 8. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Pole mkuu,

  Hamna dawa, ukiwa unaongea ukizidiwa na kigugumizi piga mguu chini neno litatoka.
   
 9. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kweli hapa watu sasa mnatania, asante anyway! sikuombei mabaya mdau
   
 10. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Pokea dawa ya kigugumizi hapa chini:

  Fuatisha maneno haya kwa imani nawe utaponywa. yesu ni zaidi ya Madaktari wa ulimwengu huu:

  Ee Mungu Baba katika jina la Yesu Kristo, umesema katika Yohana 16:24 ya kwamba "hata sasa hamna kitu kwa sababu hamjaomba, basi ombeni lolote kwa jina langu ili furaha yenu iwe timilifu". Nimesumbuliwa kwa muda mrefu, na tatizo hili la kigugumizi, lakini leo ninataka niamini ya kwamba Yesu Kristo unaweza kuniponya kama ulivyoahidi katika Marko 10:27 na Yeremia 32:26-27 ya kwamba wewe ni Mungu wa wote wenye mwili je! kuna jambo gumu lolote usiloliweza?. Nataka kupata furaha leo niondokane na kigugumizi, na ulithibitishe neno lako kwamba unaweza kuniondolea tatizo hili. Kwa kuwa neno lako katika Mitahali 30:5 linasema kila neno lako limehakikishwa, na wewe ni ngao yao wakwaminio, ninataka ithibitike leo ya kwamba kila neno lako limehakikishwa na kwamba utaniponya. Katika jina la Yesu Kristo nimeomba haya yote, Amen".

  Ukiomba kwa imani, na usipopata uponyaji, unijulishe.

  best regards
   
 11. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Amen
   
 12. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  Sasa hapa ndugu yangu nimekutania nini? sijawahi kusikia dawa ya kigugumizi, labda ufanyiwe operesheni ukiwa mdogo au kama wewe ni muumini wa dini ya kikristu uwende kanisani ukaombewe. Ila watu huwa wanapiga miguu chini na maneno huwa yanatoka endapo umebanwa sana/chronic stuttering.
   
 13. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  its ok Nguli, peace!
   
 14. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Halow Jf Dr,
  jamani madactari na wote wenye fani ya utabibu, nina binti wa miaka 4, alianza kudevelop kigugumizi tangu akiwa na miaka 3 mpaka sasa, kuna wakati kinakuwa juu sana wakat mwingine kinashuka. Sasa ndugu zangu naomba msaada wenu niweze kumnusuru binti yangu na mateso ya kuongea. Lingine pia mimi nina kigugumizi, na nina wadogo zangu 2 pia wanacho, bab pia anacho lkn kwa mbali. Najua kinaweza kuwa cha urithi ila ningependa kujua kama kuna njia ya kumpunguzia bint yangu shida ya kuongea. Nawasilisha kwa msaada wa maoni na ushauri. Asanteni
   
 15. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Pole sana.
  Wakati ukingojea msaada wa wataalam hapa JF. Jaribu kupitia hii link:

  Have a problem stutter or stammer. The How to stop stuttering stammering centre can help

  Jamaa anaeleza kuwa amewasaidia watu kadhaa kuachana na kigugumizi.
   
 16. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole sana mtoa mada mwanao anakuwa na kigugumizi wakati gani?? mfano mimi nikiwa na hasira huwa kinanitokea yani nashindwa kuongea kabisaa naweza hata kuua mtu akiwa karibu yangu.
  Je mwanao anacho wakati wote au??
   
 17. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sorry to bother you, mimi huwa ni mpenzi wa kuangalia TV Emmanuel, jamaa alikuja ana kigugumizi mpaka kuongea kanisani ilikuwa ni shida. Alivyopewa annointing water kikaisha na akaeleza shida yake pale pale na kupona. Huwa kuna aina nyingi upepo mbaya unapita katika njia nyingi.
   
 18. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
 19. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Maria Rosa, asante, Mwanangu anacho wakati wote, kuna wakati kinashuka lakn hakiishi, ila anakuwa nacho wakati wote
   
 20. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Caro, nashukuru kwa ushuhuda, nahisi hvyo, wakati tukiendelea na maombi tunaangalia sayansi inasemaje, usijekuta ni kukosa kula karoti tu, naishia kukemea. Al in al, I should not underestimate the power of The Great God of Might!
   
Loading...