Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 525
- 1,816
Jinsi tunavyoiona leo teknolojia na uchumi wa China ukipaa na kuitishia Marekani, ndivyo ambavyo Japan ilikuwa na uchumi unaokua kwa kasi na kiteknolojia karibu kuifikia Marekani miaka ya 1980.
Marekani akaja na mkataba ulioitwa PLAZA ACCORD. Mkataba huu Marekani alisaini na mataifa ya Japan, Uingereza, Ufaransa na West Germany. Wakati huo haya ndiyo yalikuwa mataifa yenye uchumi mkubwa duniani na kiviwanda.
Wakati huo dollar ya Marekani ilikuwa na thamani kubwa sana kiasi kwamba export (mauzo ya nje) ya bidhaa za Marekani ilipungua sana duniani, kwa sababu watu wengi duniani walishindwa kuhimili bei za bidhaa za Marekani.
Yen ya Japan ilikuwa na thamani ndogo ukilinganisha na dollar hivyo ilisaidia sana kwenye export ya bidhaa zake. Wakati huo makampuni ya Japan kama TOYOTA, TOSHIBA n.k yalitawala soko la dunia huku makampuni ya Marekani yakiwa na export ndogo, hii ilikuwa hatari kwa uchumi wa Marekani.
Kwa sababu ya kushuka sana kwa mauzo ya nje ilipelekea trade deficit kwa uchumi wa Marekani. (Trade deficit ni pale taifa linapotumia pesa nyingi kuagiza bidhaa kutoka nje kuliko mapato wanayopata kwa kuuza bidhaa nje. Sikuzote hii huwa ni sign mbaya kwa uchumi wa nchi)
Tarehe 22 September 1985 katika hoteli ya New York City's Plaza Hotel, nchini Marekani mawaziri wa fedha wa nchi za Japan, Ufaransa, Uingereza, West Germany na mwenyeji Marekani wakakutana.
Marekani aliyashinikiza mataifa hayo manne yapandishe thamani ya sarafu zao dhidi ya dollar ya Marekani.
Mataifa hayo yakakubaliana na Marekani matokeo ni kwamba kwenye soko la dunia Marekani akaanza kuuza zaidi bidhaa zake kuliko mataifa mengine ya kiviwanda
Nchi hizo ziliathirika sana kiuchumi lakini hasahasa Japan kwa sababu exportation ya bidhaa zao katika soko la duniani zilipungua sana.
Nafikiri katika vitu ambavyo Wajapani hawatakuja kusahau ni kuingia mkataba huu wa kimangungo na Marekani na kuwashusha.
China imekataa kuwa kama Japan imekataa kutikiswa na Marekani anapigwa vikwazo lakini anakuja na mbinu mbadala. Kuna la kujifunza kutoka China tofauti na Japan.
Marekani ni kutunishiana naye misuli tu kibabe kama Urusi na China wanavyofanya sio watu wazuri.
Japan na EU wametepeta wamechagua kuwa chawa wa Marekani.