Kuna ngoma moja tu kutoka kwa god of hiphop himself EMINEM kitu kinaitwa Lose Yourself.
Hii ngoma naweza kukaa nikaisikiliza hata masaa mawili mfufulizo kwa vibe la biti yake na mashairi yanayohakisi uhalisia wa maisha ya kweli, maisha ambayo ni magumu na vikwazo kwa asilimia mia moja.
Hiki chuma kinapiga kabisa kwenye moyo kiasi kwamba kila nikisikiliza nakuwa napata vibe na nguvu ya ajabu kabisa huku nikienda mstari kwa mstari.
Yaani jinsi tu hii ngoma inavyoanza inakumotivate mara 1500 ya motivation speaker wote duniani.
Em anaanza na
"Look if you had one shot, or one opportunity,
to seize everything you ever wanted,
in one moment, would you capture it,
or just let it slip. Yoo.
Humu ndani kuna hiki kinanda hatari sana ambacho kinapita ndani kabisa ya ubongo kama umepigwa shoti ya kichwa.
Mzuka ushaanza kunipanda tena ngoja niishie hapa nikasikilize hii best hiphop song of all time.
Na kitu kimoja ukitaka uilewe vizuri hii masterpiece ni kuelewa kila mstari, kusema ukweli ni one of the best rap song ambayo haitokuja kutokea duniani, Tena.