Plan B

mkanyikivega

JF-Expert Member
Jan 16, 2016
215
224
Wanaume wa Dar mkiitwa kwa RC Makonda kuhusu kuterekeza watoto, tumia hizo points utashinda tu kesi..

Land alienation -matajiri walinunua ardhi tukakimbilia dar, baada ya kukosa ardhi ya kulima.

Forced Labour -tulifanyishwa kazi ngumu kiasi kwamba tukakosa wanawake wa permanent, tukazaa na tukahamishwa eneo lingine la kazi.

Low wages -mshahara ilikuwa midogo hii ilisababisha kutotimiza majukumu yetu ya kuwalea watoto wetu.

Poor technology-hii imesababisha kukosa mawasiliano kwa wakati kiasi kwamba tukitaka kuwasiliana na watoto hadi tupande juu ya Miti.

Poor infrastructure - ilisababisha tupate tenda ya kujenga barabara, na kila tulipopita tuliacha Mtoto.

Lack of education- hii kwa upande wa kina Dada imewasabashia kutokujua kalenda zao vizuri, hii imesababisha mimba kutunga bila wao kujua.

Unemployment-kutokana na kuwa sina kazi ya kueleweka hii imesababisha kutotimiza majukumu yangu.

Taxation-kodi ya bidhaa imekuwa kubwa hii imepelekea kufunga biashara zetu ambazo tulikuwa tunapata chochote.

Yaani hizi points huwa hazikataagi swali ..
 
Back
Top Bottom