Kwenye Walimu wa kujitolea kuna ukakasi ila Rais nimekuelewa

Cobra70

Senior Member
Jan 2, 2020
167
363
Wanabodi nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi iendelee..

Kwanza nampongeza mh. raisi kwa maono marefu katika katika eneo la utumishi wa umma hasa kwenye kada ya elimu pamoja na ualimu wenyewe. Raisi ameona mbali sana katika ualimu. Katika kongamano la wanawake initiative foundation raisi ameongea ukweli uliodhahiri kuhusu ualimu.

Nina maswali mengi nmekuwa nikijiuliza je kuna tofauti gani kati ya
Wanafunzi wa zamani na wa Sasa? Na je Kuna tofauti gani kati ya walimu wa zamani na wa kisasa? Ila majibu ni mepesi sana ne hayaitaji elimu ya chuo kikuu wala PHD.

Wanafunzi wa sasa uwezo wao wa kufikiri na kutenda ni mdogo ukilinganisha na wa zamani. Je ni kwanini? Walimu wa Sasa hawana wito kama wa zamani, Je kwanini?

1. Walimu wengi ni walimu jina ila hawana wito. Wengi hawakuwaza kuwa waalimu ila vigezo vya ufahulu wao umewafanya kuwa waalimu wakaona hakuna namna ili mradi kinywa kiingie mdomoni. Walimu wa zamani walifanya kazi kwa wito na kuwalea watoto kimaadili ila kwa Sasa ni bora liende mwalimu akimwadhibu mwanafunzi kwa kutofanya home work au kwa utovu wa nidhamu mzazi anakuja juu eti haki za binadamu hivyo mwalimu wa kisasa anajisemea kichwani kwani Tsh ngapi! Kila mtu apambane na maisha yake hivyo watoto wanakua vilaza na wenye tabia mbaya. Ualimu ni kujitoa ili uweze kuwa mwalimu bora kukubali kupigwa mawe mengi kuliko kumkatia tamaa mtoto.

2. Hakuna mafanikio katika elimu bila msaada wa wazazi. Ila wazazi wa sasa wanajifanya kuwa busy na maisha kuliko kujua kesho ya watoto wao. Wazazi wengi wameshindwa kwenye eneo muhimu sana la malezi ya watoto wao. Wazazi wengi wameshindwa kuwapangia ratiba watoto wao na kuwadhibiti juu ya marafiki, makundi na magenge mabovu. Yaani unakuta Wanafunzi wanadhurura usiku, wamekaa centre usiku, wanacheza mabonanza, mechi za mpira zote ziwe za mchana au usiku zote ni zao. Wanafunzi wengi wanamiliki smart phones wanachokiangalia humo ni kumuomba Mungu na muda anaotumia kwenye simu kuchati na boyfriend au girlfriend wake ni Majanga. Wengi wao ngono wameanza mapema wanatembea na watu wakubwa inafikia kipindi walimu wanapowakoromea wanawachukulia poa sana kama wapenzi wao. Imefikia kipindi yaani wanafunzi kupitia notes ya nini wamefundishwa darasani au kujisomea vitabu ili kuongeza wigo wa maarifa kwao imekuwa dhambi mana watu wenye jukumu la kuwasimamia hawajielewi yaani wamepigwa ganzi.

3. Utandawazi! Matumizi mabovu ya simu janja na vyombo vya kupashana habari na burudani vimewaaharibu sana vijana wetu. Muda mwingi wanafunzi wanaanglia miziki ya wasanii wa kiume waliosuka nywele, suruali za kubana, wamevaa eleni na mala nyingine wamevaa magauni je hapo utamtoa mtu? Ukiuliza albam zote utatajiwa hadi inayokaribia kutoka muulize sasa idadi ya topic alizozisoma Zero. Kwenye simu full kuangalia pono na wadangaji wa mitandaoni pamoja na kuchati na wapenzi wao je hapo kuna shule? Muda mwingi watoto wanawaza fashion cjui model, min kuliko shule.

4. Mikopo kwa walimu hisiyo na tija pamoja na michezo ya upatu. Taasisi nyingi za mikopo na vikundi vya upatu zinapata faida kubwa kupitia walimu kwani walimu walio wengi ni wabovu wa hesabu ya maisha. Walimu wengi wamekuwa wakichukua mikopo mingi yenye muda mrefu yenye riba kubwa kwa ajili ya ujenzi mala nyingi hujenga majumba makubwa kuliko kipato chao na kuishia kwenye maboma wakijitahidi sana huishia kuezeka. Msharahara wanaobakia nao na majukumu waliyonayo hayaendani pia na lengo la ujenzi wao kuishia njiani huealetea msono wa mawazo na kuathiri utendaji wa kazi zao. Pia wamekuwa na matamanio ya utajiri wa haraka bila kuvuja jasho na kudondokea kwenye mikono ya matapeli yaani biashara za mitandaoni, betting n.k. Wengine wanakopa hela kwenye taasisi za kifedha wanapeleka kwenye michezo ya upatu wakipigwa wanachanganyikiwa na kupata msongo wa mawazo namna ya kuishi muda wote wa deni bila ya kufanya chochote cha maana hivyo hali ya utendaji kazi inashuka, kujihusisha na bodaboda, utoro na sababu chungu nzima hazikatiki.

5. Sera mbovu za elimu, Big result now ndio nn? Matokeo makubwa uwezo mdogo! Performance kubwa kwa mtoto pactically Zero. Hapa ni kutengeneza taifa lenye vyeti vizuri kitaaluma ila uweze mdogo. Unafuta somo la kilimo na stadi za kazi shule za msingi ili iweje! Kupitia haya masomo mtoto aliweza kumaliza la saba na kuweza kujiajiri bila kusubiri ajira. Ifikie mahali mpe mtu anachostahili hata kama watu 5000 wafahulu Tanzania nzima ni vizuri sana, ila ikitokea mambo ya standardization yatakuwa ya nn hayo! Mana na huo ni wizi kama wezi wengine kwa kupata kitu ambacho hustaili. Kwa mambo ya Big results now tutapeleka watoto sekondari ambao kusoma na kuandika ni tabu na kupelekea lawama kwa walimu wa shule ya msingi na sekondari na kuzalisha bomu lisilo la lazima kwa wengi kuwa na ufahulu wa div 4 na 0 na hata pia kuzalisha wataalam ambao hawakidhi vigezo. Mwanafunzi ambaye uwezo wake ni mdogo akariri darasa ila tukiendelea na bora liende huko mbele ni Majanga.

6. Udahili wa ualimu! NACTE na TCU idahili walimu kwa wale wenye ufahulu wa juu tu. Kwa walimu wa sekondari walau wawe na ufahulu wa div. 1 na 2 na wa shule za msingi uwe div.3 hii itatusaidia kupata walimu mahili na si bora walimu. Hii itafikiwa pale kada hii itakapoheshimika kwa kuboresha mazingira bora ya kuishi ya walimu na kufundishia, posho, semina na mishahara minono hivyo kada hii itavutia vijana wengi kuisomea na kutusaidia kupata walimu mahili.

7. Ufinyu wa walimu, mwalimu mmoja kufundishia wastani wa watoto 1000 na wote uwasahihishe na kuwapa mazoezi ya kutosha, mala maandalio ya muda mfupi ya vipindi vya kila siku kwa kila darasa, mala majukumu lukuki ya vitengo vya shule hapo kupata matokeo mazuri itakuwa ndoto zaidi ya big results now.

8. Kukosa walimu wa kujitolea ili kuziba pengo kwa masomo yenye uhitaji kwa shule husika. Hapa kiukweli kuna harufu ya siasa kuliko uhalisia ulivyo. Walimu hawa ni watu wanamahitaji kama binadamu wengine ila kwa baadhi ya wakuu wa shule wamekuwa na roho ngumu utafikiri hawakuzaliwa. Yaani mwalimu anajitolea bure hata kumkarimu kwa chai na chakula cha mchana inakuwa nongwa wanadai hawana mafungu hayo hii inawakatisha tamaa na kutafuta shughuli nyingine kutokana kwanza kufanya kazi akiwa na njaa, hakuna posho na pia wengine kutegemewa na familia zilizowasomesha. Hili suala la kuajiri walimu wa kujitolea lingemalizwa na vikao vya kamati ya wazazi wa eneo husika kwa kuangalia mapungufu ya uhitaji wa walimu na hivyo kuingia mikataba nao ila dhana waliojengewa ya elimu bure imewafanya kuwa walemavu wa akili.

NOTE: Walimu wa kujitolea mashuleni ni asilimia Zero point kulingana na mazingira mabovu ya kuwakarimu ila watakaoonekana kwenye mfumo wa ajira kupitia mfumo wa kujitolea ni asilimia zaidi ya hapo ambao wengi wao ni ndugu, watoto wa rafiki na rushwa za wakuu wa shule.
 
Mkuu usiwe kama Bwana mgumu Yesu alietolewa mfano kwenye biblia
"...unataka kuvuna mahali usipopanda........."

Serikali yetu haijawekeza kwa walimu. Serikali hawatambui walimu kama kada zingine kama wanajeshi au askari au hata fani nyingine

Sasa kama miongozo yenyewe ya Elimu haitambu walimu wenye Masters au hata PhD kwa kuweka mishahara na posho maalumu kwa walimu hao unategemea nini??

Bado inatakiwa serikali ijue kuwa factor Output is direct proportional to factor Input.

Yaan unawekeza nini kwa mwalimu ili yaweze kutoa Output unayoitaka

Mathalani hata semina au workshop's au makongamano su hata warsha tu za masomo kwa walimu ni changamoto
 
8. Uwingi wa shule kupitiliza na mashindano ya kufaulisha kwa 100%..........huko msingi wanapita wote; wasiojua na wanaojua kusoma

9. Elimu bure imefanya wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla kuipuuza kabisa elimu........wanajiendea tu ilimradi lakini akilini hawawazi shule kabisaaaaa
 
Kama walimu wasasa ni vilaza na kwakuwa wanatokea jamii moja na wazazi wengine,basi wazazi wasasa nao ni vilaza hivyo hata watoto nao ni vilaza(hawafundishiki)
 
Walimu wa zamani walifanya kazi kwa wito na kuwalea watoto kimaadili i
Haonl watoto wa zamani (wazee wa Sasa) wenye maadili mbona hawaonekani kwenye jamii?

Si ndiyo hawa akina;-
..babu seya wabakaji?
..chenge, magiduli, Biswalo, n.k wezi wa mali ya umma?
..papa ndama, papa msofe wauza ngada?
 
Back
Top Bottom