Hi. ukisema hivo unakosea mkuu, kwahiyo wenye gpa ndogo wafanyaje? wafe njaa? mi nadhani suala sio gpa, nchi zinazojali watu wao watu hawafiki hata vyuo wanaishia seconday na wana ajira nzuri, serikali yetu haina msimamo. kuna watu wengi sana ambao sio watanzania wanafanya kazi kwenye kampuni tena kampuni binafsi nyingi na wengi wakuja sio raia, unafkiri kwenye nchi zao watakupa ajira ww kwanza kabla ya mtu wao? hapana, nchi zote zinazojali zinahakikisha wazawa wanapewa ajira kabla ya expatriate. sisemi watu wa nje wasiajiriwe nchi hapana, ila sio kwa kiwango kikubwa km hapa nchi kwetu. vijana wanahangaika mtaani masikini wengine wakuja kaja na cheti cha uongo, experience ya uongo, ana kiji experience kdg akijua kazi kdg tu bac ataandika ana experience ya miaka 7 na anaajiriwa, wa kwetu humu humu wanahangaika. Ifike kipindi serikali iwe adilifu, huruma na kujali watu wao. serikali ingeweka sharia na zifuatwe vijana wapate ajira, hata kama ni mishahara kidogo lakini ni fresher basi sio mbaya sn japo laki 4 tu watu wajikimu hata hela ya kula, huko mtaani ni njaa tupu, labda haijakufika bado ndugu, sisi wote ni watanzania, umoja na upendo ndo utakaotupeleka mbele daima.