Jinsi ya kuchora/kujaza nyusi zako kwa kutumia brow powder au brow gel

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Kabla hujaanza kujihusisha na mambo ya makeup ni vitu vingi sana unakuwa hujui na nadhani kuwa bado wapo wale wasiojua utaratibu wa makeup vizuri, kama vile makeup products au makeup tools..na hivyo kuna wengine bado wanatumia wanja wa kawaida kujazia/kuchorea nyusi zao, hiyo pia ni sawa lakini brow powder ndio better zaidi.

Jinsi ya kujaziliza/kuchora nyusi zako.
Uwe na wanja wa powder au wa jel, eyebrow brush na concealer ( hii ya mwisho sio lazima maana mimi siitumii natumia foundation na wanja wangu unakaa vizuri tuu).

Anza kwa kuzichana nyusi zako kwa kutumia brush au kitana kidogo sana ili nyusi zikae kwenye mpangilio mzuri, then chukua brow brush yako na uchukulie wanja wako wa powder kisha uanze kupaka.
Kama haupo vizuri katika kupaka unaweza kutumia eyebrow shaper na uchore shape inayokufaa

Halafu chukua foundation yako ili usawazishe ile iliyotokeza/kunyoosha ule brow powder. Tumia concealer brush kupaka mstari mwembamba ulionyooka ukifuatisha uliyochora au kujaziliza nyusi zako. Fanya hivi kwa juu na chini kisha sawazisha vizuri.

Hapa chini ni njinsi ambavyo unaweza kuchora mistari ya namna unavyotaka wanja wako uwe. Mimi kwenye kuchora hiyo mistari huwa natumia wanja wa kawaida huu wa penseli halafu katikati humo ndo naweka wanja wangu wa poda au jel.

wanja.jpg


Hapa kuna wanja wa poda na wanja wa jel
Mimi natumia zote mbili kutegemea na sehemu ninayoenda na event husika. Wanja wa jel unakaa sana kuliko wa poda. Huo wa jel hata ukitokwa jasho wenyewe hautoki mpaka utakaponawa uso na sabuni

brow-5.jpg



Hii ndio eyebrow shaper. zinakuwa 3 ndani ya pakti yake na zinakuwa za shape tofauti. Kwahiyo wewe mwenyewe utachagua shape unayoipenda kutumia.
3-piece-different-bag-make-up-font-b-eyebrow-b-font-stencil-makeup-styling-tools-tools.jpg
 
Hari zenu ndugu zangu mmi leo nimeona niandike uzii huu kwakuwa wengi wetu hatujui kujipaka wanja karibuni tujifunze pamoja kila mtu kwa uzoefu wake tuanze hapa ni Vitu gani hasa vinahitajika?
 
  • Thanks
Reactions: etu
Mim napendelea wanja wa brown(wanja wa kawaida ule wa penseli)
Unapaka size unatotaka unapaka concelar (japo concelar kma huna make up og unaonekana kituko).ukimaliza kupaka sawazisha na brush kutumia foundation or concelar mpka upate size unayotaka na nyusi zinyooke.
Ni vzr ukapaka foundation kama concelar kusawazisha wanja
So unatakiwa kuwa na wanja,kibrush kidogo cha kusawazisha na foundation au concelar
 
Mim napendelea wanja wa brown(wanja wa kawaida ule wa penseli)
Unapaka size unatotaka unapaka concelar (japo concelar kma huna make up og unaonekana kituko).ukimaliza kupaka sawazisha na brush kutumia foundation or concelar mpka upate size unayotaka na nyusi zinyooke.
Ni vzr ukapaka foundation kama concelar kusawazisha wanja
So unatakiwa kuwa na wanja,kibrush kidogo cha kusawazisha na foundation au concelar
Weka picha tuone
 
Back
Top Bottom