Pinda na Makinda wampa changamoto Kikwete. Je watajiwajibisha au kuwajibishwa?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Waziri mkuu Mizengo Pinda na Spika wa bunge Anna Makinda waliuambia umma kuwa rais Jakaya Kikwete ameidhinisha kuongezwa kwa posho ya wabunge. Siku moja baadaye ikulu imekanusha.Je kwa kumsingizia rais, kudanganya umma, na kupinga na rais watanusurika kuwajibishwa? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
 
Kwa uongo na visingizio dhidi ya rais, vilivyofanywa na waziri mkuu Mizengwe Pinda na Anna Makinda kwa kudanganya kuwa rais aliidhinisha nyongeza za wabunge, wahusika wataweza kuendelea kuwa ofisini na rais awanyamazie?
 
Kwa hii nchi hii,wataendelea tena kwa mbwembwe.Hii nchi bwana,ukitazama inavoendeshwa,na ukikumbuka ilivokuwa kipindi cha waasisi wake,unaweza kulia.
 
Kama kweli rais hajaidhinisha malipo ya marupurupu ya wabunge na posho za makalio, hawa akina Pinda na Makinda walipata wapi hayo waliyosema? Je hapa nani anawadanganya watanzania?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kama kweli rais hajaidhinisha malipo ya marupurupu ya wabunge na posho za makalio, hawa akina Pinda na Makinda walipata wapi hayo waliyosema? Je hapa nani anawadanganya watanzania?

Mkuu Mpayukaji, wote hao lao moja kupokezana kijiti cha kucheza na akili za wadanganyika.
 
Ni kwa mara nyingine tena tunashuhudia vituko vya Serikali ya majaribio inayoongozwa na Waheshimika wa Ccm chini ya Jk.
Katika nchi za watu makini ubabaishaji wa aina hii huwa haupewi nafasi hata kidogo.
Ninacho kiona hapa ni Ushauri wa Makinda kwa Kikwete Wabunge waongezewe posho ili aidha yeye apate kile anachokiona kwake kama sifa ya kuongezea Posho za wabunge chini ya uongozi wake. Pili ni kama rushwa ya kuwafanya nao waonekane ni sehemu ya ufisadi unaondelezwa na Serikali.Watanzania wote kwa ujumla wenu hili ni somo tosha ambalo linaonyesha ni jinsi gani sasa kila mtu anavyojitahidi kujineemesha bila kujali maslahi ya wengi.
 
Ukweli ni kwamba Jk keshabariki posho za masaburi.Ila kwa vile unamjua raisi wako asivyo na msimamo anapima nguvu ya upepo na nadhani hakuna kiongozi kigeugeu kama yeye duniani.Je umeshau aliposema hawajui Dowans, na aliposema hakuna mwanafunzi wa chuo kikuu atafukuzwa kwa kukosa ada? Umesahau alivyomtuma Vuvuzela nape awatukane wakuvuliwa magamba kisha kamgeuka.Na ilani ya CCM na OIC je? si aliwageuka waisilamu wenzake.

Btw, wote hao yaani Jinga Kubwa, Bi kiroboto na huyo mtoto wa tajiri ambaye hajitambui wala hatambui madaraka yake ni yapi [mzee wa kumwaga chozi]; ni vipofu wanao-ongozana na mwisho wa siku wote watatumbukia katika shimo.
 
Mi naona mafisadi wameamua kuchonganisha kati ya wananchi na serikali dhaifu ya jk.
 
Naye David Kafulila, Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufumua mfumo mzima wa posho na kwamba madai ya nyongeza ya posho na mishahara, hayawezi kushughulikiwa vipande vipande.
"Leo utawalipa wabunge, kesho madaktari, walimu nao wakigoma, nao uwalipe kwa wakati wao. Hii haiwezekani," alisema.
Alisema mfumo wa malipo kwa sasa ni mbaya kwani wakati daktari anayefanya kazi nzito ya kutibu wagonjwa analipwa sh milioni moja, ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) analipwa sh milioni sita kwa kukusanya kodi.

Waziri mkuu Mizengo Pinda na Spika wa bunge Anna Makinda waliuambia umma kuwa rais Jakaya Kikwete ameidhinisha kuongezwa kwa posho ya wabunge. Siku moja baadaye ikulu imekanusha.Je kwa kumsingizia rais, kudanganya umma, na kupinga na rais watanusurika kuwajibishwa? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

Ni usanii tu,hawajibishwi m2 hapo,we huwajui viongozi wetu?
 
Kama kweli rais hajaidhinisha malipo ya marupurupu ya wabunge na posho za makalio, hawa akina Pinda na Makinda walipata wapi hayo waliyosema? Je hapa nani anawadanganya watanzania?
Acha matusi mkuu. Kwa kauli zilizokwisha tolewa na viongozi hao, hakuna udangayifu wowote, bali wamekuwa wakitolea ufafanuzi upotoshwaji juu ya suala zima za posho za Wabunge. Hata kama wangekuwa wamepitisha nani mwenye kosa hapo wabunge waliopendekeza posho hizo au Rais, Waziri Mkuu au Spika. Tujaribu kutafakari sana kabla ya kulaumu. Nakumbuka wabunge wengi tu walikubaliana kupandishiwa posho wakiwemo wa upinzani. HAPA NANI ANAWADANGANYA WATANZANIA? Rais, Waziri Mkuu na Spika au WAbunge. Mimi naona ni Wabunge. Tujaribuni kwenda na facts badala ya hisia binafsi.
 
yawezekana pinda na makinda ndio wamesema ukweli ila ktkana na upepo wa madaktari imebidi serikali idanganye
 
Hawa wote uliowataja ni genge la wezi na majambazi wanaoiibia nchi!
Wana mbinu nyingi, hii pia ni moja kati ya mbinu zao nyingi za kuwachanganya wananchi ili wapate kulendeleza ujambazi wao dhidi ya taifa!
Hakuna alie na nafuu hapo, sema tu JK ndiyo kinara wa uchafu huu na mara nyingi yeye ndiye anae bunu usanii huu!
 
Naye David Kafulila, Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufumua mfumo mzima wa posho na kwamba madai ya nyongeza ya posho na mishahara, hayawezi kushughulikiwa vipande vipande.
"Leo utawalipa wabunge, kesho madaktari, walimu nao wakigoma, nao uwalipe kwa wakati wao. Hii haiwezekani," alisema.
Alisema mfumo wa malipo kwa sasa ni mbaya kwani wakati daktari anayefanya kazi nzito ya kutibu wagonjwa analipwa sh milioni moja, ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) analipwa sh milioni sita kwa kukusanya kodi.

Afadhali umeliona hilo kwa sababu wengi tunakimbilia kuwalaumu viongozi wetu wakati kumbe tatizo linaeleweka. Tatizo ni mfumo na mfumo haujawekwa na JK, MAKINDA au PINDA. Mfumo upo kisheria na ndicho tunachotakiwa kuongelea na hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa kupata katiba mpya. Kafurila alikuwa sawa na ndiyo sababu kama mbunge makini hawezi kukimbilia kulaumu viongozi huku akijua tatizo ni mfumo. Kusema Rais, Waziri Mkuu au Spika anawadanganya wananchi ni kuonesha jinsi gani una upeo mdogo wa kuchambua mambo.
 
Looking at the pattern in this government mbona anayedanganya anaeleweka! Maana kuna mtu huwa anakataa kufahamu hata yanayofahamika.
 
Kama kweli rais hajaidhinisha malipo ya marupurupu ya wabunge na posho za makalio, hawa akina Pinda na Makinda walipata wapi hayo waliyosema? Je hapa nani anawadanganya watanzania?

Mpayukaji umeniamsha. Kumbe si posho ya vikao ni posho ya makalio. Nimekapenda hako kaupayukaji kako.

Mihimili inakinzana kila kukicha. Bunge na executive. Spika anasema zimepand huku presidaa anasema hazijapanda. Lakini pia ndani ya executive wanakinzana: tunasoma magazetini kwamba PM amesema zimebarikiwa lakini ofisi ya Rais inasema laaah hakuna kitu kama hicho!! Nadhani sasa ni wakati muafaka wa kuingiza muhimili wa Mahakama ili utuambie nani ni muongo!
 
Since when we have got the accountability word in our vocabulary? Kama kweli wabunge wanalipwa posho hizo, itakuwa aibu kubwa kwa ikulu maana watakuwa wanafanya kazi ya kujidanganya nafsi zao. Watanzania wanapenda kujua ukweli na sio longolongo ambazo sasa zinaonekana ndo mhimili wa ustawi wa siasa zetu.
 
Naye David Kafulila, Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufumua mfumo mzima wa posho na kwamba madai ya nyongeza ya posho na mishahara, hayawezi kushughulikiwa vipande vipande.
“Leo utawalipa wabunge, kesho madaktari, walimu nao wakigoma, nao uwalipe kwa wakati wao. Hii haiwezekani,” alisema.
Alisema mfumo wa malipo kwa sasa ni mbaya kwani wakati daktari anayefanya kazi nzito ya kutibu wagonjwa analipwa sh milioni moja, ofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) analipwa sh milioni sita kwa kukusanya kodi.

it's something which is irelevant kabisa hata ukiangalia kwa wabunge ambao wengine elimu zao ni ndogo na kazi yao nikupayuka majukwaani na kupitisha bajiti za kupewa hongo na kulala bungeni tu bado wanalipwa zaidi ya madaktari na walimu ambao wanafanyia kazi ktk mazingira magumu
 
Back
Top Bottom