Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,832
- 21,661
Ni baada ya Waziri wa Elimu kulidanganya Bunge kuwa wizara yake ina mitaala ya kufundishia. Waziri wa Elimu Mhe. Kawambwa alipotakiwa kuwasilisha mitaala hiyo mezani kwa Naibu Spika na mtoa hoja Mhe Mbatia -Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. Kawambwa alibaki kutoa macho!!!
Wabunge wa upinzani wameazimia kutoa hoja ili waziri Kawambwa ajiuzuru na asipojiuzuru watamtaka aliyemteua amfukuze kazi vinginevyo Wabunge wa upinzani watatoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Mhe. Pinda!
Maskini Pinda huku wana Mtwara wanamtaka amuhamishe Mkuu wa Mkoa wao Simbakalia na huku wabunge wanataka kuazimia kutokuwa na imani naye!!
Nina wasiwasi kuwa Pinda atachangayikiwa na msongo wa mawazo!