Pinda hatarini kung'olewa

Pinda hatarini kung'olewa

Maskini mawaziri waislamu.Watu wa mfumo walianza kumuandama Omar Nundu akaenda,akaja Mustafa Mkullo akaenda.
Huyu Kawambwa hata sikutarajia kutokana na kuwa kwake mtetezi wa NECTA.Ukiona hivyo kuna kijambo kidogo cha mfumokristo ambacho ama hajatekeleza au ameachia sehemu fulani wafaidi watanzania wote.
Sijui akiondoka Kawambwa baraza la Kikwete litabaki na waislamu wangapi?.Wacha yamkute Kawambwa atajua kuwa watu wa mfumo hawafanyiziki wema.Akitaka kuwa mzuri basi awe mkweli na amkumbuke Mola wake zaidi.

Tunahitaji kukokotoa akili yako wewe unaambiwa hii nchi tangu mwaka 1961 haijawahi kuwa na mitaala ( Curriculum) ndio maana kila waziri na raisi anayekuja anafanya chochote atakacho na elimu yetu iwe kwa nia yake au kwa shinikizo kutoka nje ya nchi lakini elimu ni uhai wa taifa lazima lijulikane vizuri hata kikatiba sasa mwenzutu unatuletea vitu vya ajabu kweli
 
wanatakiwa wajiuzulu wote, kuanzia waziri wa elimu na katibu wake na ma afsa elimu wote kuanzia mikoani na wa wilaya zote pia wakuu wa shule wapewe onyo kali otherwise tutaendelea kutwanga maji kwenye kinu ya hadi burundi na rwanda wanaboresha elimu yao huku sisi tunafanya siasa ndio maana tunaitwa maiti tunaoishi.
Inauma sana.
 
waziri mkuu ni sawa na "toothless bulldog" waziri na mkuu wa mkoa wote wateuliwa na raisi.
 
....

Nina wasiwasi kuwa Pinda atachangayikiwa na msongo wa mawazo!

Ninakumbuka sana maneno yake wakati akielezea suala kuteuliwa kuwa waziri mkuu...alisema alikuwa hataki "mzigo huu"... kwa hiyo nadhani anafanya makusudi atimuliwe.
 
Ni baada ya Waziri wa Elimu kulidanganya Bunge kuwa wizara yake ina mitaala ya kufundishia. Waziri wa Elimu Mhe. Kawambwa alipotakiwa kuwasilisha mitaala hiyo mezani kwa Naibu Spika na mtoa hoja Mhe Mbatia -Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. Kawambwa alibaki kutoa macho!!!

Wabunge wa upinzani wameazimia kutoa hoja ili waziri Kawambwa ajiuzuru na asipojiuzuru watamtaka aliyemteua amfukuze kazi vinginevyo Wabunge wa upinzani watatoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Mhe. Pinda!

Maskini Pinda huku wana Mtwara wanamtaka amuhamishe Mkuu wa Mkoa wao Simbakalia na huku wabunge wanataka kuazimia kutokuwa na imani naye!!

Nina wasiwasi kuwa Pinda atachangayikiwa na msongo wa mawazo!

Sijui atalia tena! Pinda ni bigwa wa kulia. Ndo maana uso wake umejaa mitaro (makunyanzi) ya machozi
 
Mtoto wa Mkulima ni chuma cha pua, hakiyeyuki kwa moto wa nyasi!, na kama ni kisiki, hicho ni kisiki cha mpingo!, hakingoleki kwa jembe, panga wala shoka!, labda kwa ...
Pasco.

Mkuu nadhani umekosea! Mtoto wa mkulima ni laini kama mlenda! Isipokuwa system inamlazimisha abakie madarakani!

Kumbuka maoni yake katika tume ya katiba; alipendekeza rais apunguziwe madaraka! Maoni kama haya si rahisi sana yatolewe na mtu aliye katika nafasi kama yake!

Hebu linganisha na maoni ya Ombeni Sefue - Katibu mkuu kiongozi katika tume ya katiba!
 
Tanzania tuna mtindo wa kuiga mambo yasiyoya msingi. Mh. Pinda alikwenda Mtwara kutuliza ghasia, namshukuru sana kwa kufanikiwa hilo maana asingefanya hivyo leo tungekuwa katika ramani ya dunia tukiwa tunaogelea katika maji machafu. Kuwepo Pinda pale Mtwara ilikuwepo Serikali nashangaa wengine wanasema JK amechelewa. Maana ya kuwa Pinda kuwa mtendaji wa Serikali ni nini??? Ndiyo hiyo Bw. Tuwe fair kutoa maoni tusibeze kila linalofanyika. waliopatwa na maafa huko Mtwara wanamshukuru sana Pinda, the problem wengi tunaangalia TV tungevaa viatu vya waathirika!!!! Tusingependa kugaragaza AMANI KATIKA MAVUMBI. Tudumishe AMANI!!!!!

Pinda halaumiwi kwa kuwa system yetu ndivyo ilivyo! Lakini kwa nini imechukuwa muda mrefu kufikia hapo Pinda alipowafikisha watu wa Mtwara?! Jibu ni kuwa wote waliotakiwa kutoa ufafanuzi muafaka ama hawana uwezo au hawakujua msimamo wa wakuu wao! Na kwa kuwa hapa kwetu rais ni kila kitu na kwa kuwa alikuwa nje ya nchi hakuna kitu ambacho kingekuwa na jibu sahihi!

Kumbuka sakata la Jairo!
 
Maskini mawaziri waislamu.Watu wa mfumo walianza kumuandama Omar Nundu akaenda,akaja Mustafa Mkullo akaenda.
Huyu Kawambwa hata sikutarajia kutokana na kuwa kwake mtetezi wa NECTA.Ukiona hivyo kuna kijambo kidogo cha mfumokristo ambacho ama hajatekeleza au ameachia sehemu fulani wafaidi watanzania wote.
Sijui akiondoka Kawambwa baraza la Kikwete litabaki na waislamu wangapi?.Wacha yamkute Kawambwa atajua kuwa watu wa mfumo hawafanyiziki wema.Akitaka kuwa mzuri basi awe mkweli na amkumbuke Mola wake zaidi.


Kafie mbali we mdini mkubwa! Akifanya madudu aachiwe tu, kisa muislam!!

Kwenda zako!
 
kwanini mitaala ya kufundishia iwe siri,je walimu wanatumia kitu gani kuwafundishiwa vijana wetu? na je kunahaja ya kuwa na usiri ktk jambo muhimu linalohusu maisha na maendeleo ya watanzania?
wekeni siri mikata ya kuchimba rasilimali za Taifa,lakini msiweke usiri ktk mitaala ya kufundishia maana elimu ndio uridhi pekee tunaotegemea kuwapa vijana wetu na sio uridhi wa dhahabu wala gesi,ni ELIMU
 
Last edited by a moderator:
ina maana wizara haina copy 300 za mitaala zilizotayari?jee hao waalimu wapya maelfu watakaoajiriwa watafundishaje?nchi hii kwa usanii ni balaa
 
Ni baada ya Waziri wa Elimu kulidanganya Bunge kuwa wizara yake ina mitaala ya kufundishia. Waziri wa Elimu Mhe. Kawambwa alipotakiwa kuwasilisha mitaala hiyo mezani kwa Naibu Spika na mtoa hoja Mhe Mbatia -Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. Kawambwa alibaki kutoa macho!!!

Wabunge wa upinzani wameazimia kutoa hoja ili waziri Kawambwa ajiuzuru na asipojiuzuru watamtaka aliyemteua amfukuze kazi vinginevyo Wabunge wa upinzani watatoa hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Mhe. Pinda!

Maskini Pinda huku wana Mtwara wanamtaka amuhamishe Mkuu wa Mkoa wao Simbakalia na huku wabunge wanataka kuazimia kutokuwa na imani naye!!

Nina wasiwasi kuwa Pinda atachangayikiwa na msongo wa mawazo!

Wabunge wote wa upinzani hata nusu ya wabunge wa CCM haifiki sasa Pinda anaondolewa kwa utaratibu upi? Wastage of time kwa jambo ambalo haliwezekani
 
Back
Top Bottom