Pinda awasifu Ngeleja, Malima

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Pinda awasifu Ngeleja, Malima
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Dodoma; Tarehe: 29th July 2009 @ 07:04


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewasifu mawaziri wanaoongoza Wizara ya Nishati na Madini, William Ngeleja na Adam Malima, kwa uhodari wao wa kuchapa kazi, licha ya kuwa vijana waliokabidhiwa wizara nyeti na ngumu. Pinda alitoa sifa hizo juzi alipohudhuria kwa mara ya kwanza tangu awe Waziri Mkuu, hafla zinazoandaliwa na wizara baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Wizara zao.

Alihudhuria hafla ya Wizara ya Nishati na Madini. Aliwaambia mawaziri mbalimbali, naibu mawaziri na wageni waalikwa, kwamba aliamua kuhudhuria hafla hiyo, kwa sababu kuu mbili, ikiwamo kazi nzuri iliyofanywa na mawaziri hao vijana wakati wa kujibu hoja za wabunge juzi jioni wakati wa kupitisha makadirio yao.

“Nimekuja hapa ikiwa ni mara yangu ya kwanza kufanya hivi… najua mawaziri wengine watanifuata, lakini nimekuja hapa kwa sababu kuu mbili. Moja ni kwa kazi nzuri iliyooneshwa na vijana hawa wawili jioni pale bungeni.

“Rais Jakaya Kikwete aliwakabidhi wizara hii akijua kuwa ni nyeti na ngumu, lakini sote tunakubaliana kuwa vijana hawa wamefanya kazi nzuri sana. Tena katika kipindi cha mwaka na kidogo. “Kwa hiyo, baada ya kazi ile ya pale jioni… nikamwambia Ngeleja nadhani nina sababu ya kuja katika sherehe zenu. Nikaona nije niwape motisha vijana hawa, kwa kazi ngumu na nzito waliyofanya.

Wamejibu maswali ya wabunge vizuri sana. Wanachapa kazi nzuri,” alisema Waziri Mkuu na kushangiliwa na watu waliohudhuria hafla hiyo.

Ngeleja, ambaye ni Mbunge wa Sengerema mkoani Mwanza na Malima anayetoka Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani, umri wao ni kati ya miaka 40 na 45, na walikabidhiwa kuongoza wizara hiyo katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete Februari mwaka jana, lakini wamejipambanua kuwa miongoni mwa mawaziri wanaochapa kazi vizuri, ingawa wamekabidhiwa sekta zinazogusa maisha ya Watanzania wengi.

Karibu wabunge wote waliochangia kwa kuzungumza na 30 waliopata fursa ya kuuliza maswali ya ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi juzi, waliwamwagia sifa mawaziri hao wawili kwa kazi yao nzuri.

Waziri Mkuu aliitaja sababu ya pili iliyomfanya ajumuike na waalikwa katika hafla hiyo kuwa ni kumuunga mkono Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shelukindo, ambaye alisema alimfundisha kazi akiwa Ikulu. “Jambo lingine ambalo nilikuwa sijawahi kulisema, ni hili la Mzee Shelukindo.

Huyu alinifundisha kazi mimi Ikulu. Namshukuru sana kwa mwongozo wake. Nikaona nije nimuunge mkono, kwa sababu naamini anawaongoza vizuri vijana hawa wawili na ndiyo maana kazi yao nzuri inaonekana. Kwa hiyo, nakushukuru sana Mzee Shelukindo,” alisema Pinda aliyefanya kazi Ikulu kwa zaidi ya miaka 12.

Shelukindo, ambaye ni Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga kwa tiketi ya CCM, aliwaeleza waalikwa katika sherehe hizo kwamba alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara mbalimbali kwa miaka 18, ikiwamo Ikulu ambako alikuwa Naibu Katibu Mkuu na Katibu Mkuu chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Alhaji Ali Hassan Mwinyi katika Awamu ya Pili.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema mbali ya Ngeleja na Malima kufanya kazi kwa kipindi kifupi na kazi nzuri inayoonekana, aliwataka waendelee kuongeza bidii na kwamba serikali itaendelea kuwapa msukumo katika kuboresha kazi zao, na akaahidi kwamba moja ya maeneo atakayowasaidia ni suala la umeme vijijini, lililozungumzwa na wabunge wengi katika michango yao kwa wizara hiyo.

Kwa upande wake, Shelukindo alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutambua kazi anayoifanya kwa kuwasaidia mawaziri hao na kwamba ataendelea pamoja na kamati yake kuwashauri kwa nia ya kuendelea kujenga taifa na kuboresha sekta ya nishati na madini.

Naye Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa wizara hiyo, Mohamed Habib Mnyaa ambaye ni Mbunge wa Mkanyageni (CUF), alisema michango inayotolewa na upinzani haina nia ya kubomoa, bali kusaidia kuboresha masuala mbalimbali katika sekta husika.

Waziri Mkuu pia alikiri katika hafla hiyo kuwa ipo michango mizuri ya Mnyaa na kambi yake ambayo itafanyiwa kazi na serikali. Waziri Ngeleja aliwashukuru wabunge kwa niaba ya wizara yake na kuahidi kwamba wataendelea kushirikiana katika kuboresha sekta ya nishati na madini kwa maslahi ya Watanzania wote.
 
Madini yetu dhahabu, Almasi, Tanzanite na (si ajabu hata uranium itapoanza kuchimba) bado hayatunufaishi Watanzania. Wanaofaidika ni wazungu na makpuni yao pamoja na shareholders wao ambao wengi watakuwa ni wageni. Lakini hili la madini yetu kutoinufaisha nchi Pinda halioni, la Kiwira kurudishwa Serikali katika mazingira yaliyojaa utata kalifumbia macho, la Watanzania wenzetu wanaoishi karibu na migodi kufa na kuathirika kwa afya zao kutokana na kemikali zenye sumu zinazotumika na makampuni ya uchimbaji wa madini hili nalo kalifumbia macho. Mapendekezo ya kuibadili mikataba ya uchimbaji madini ili kuhakikisha Watanzania tunafaidika na madini yetu hayajulikani hata yameishia wapi pamoja na ahadi kwamba yangejadiliwa bungeni kabla ya kuyapitisha rasmi.

Huyu Pinda naye sasa anadhihirisha usanii wake wa hali ya juu kwa kusifia vile ambavyo havistahili kusifiwa
 
Kwa hiyo kazi nzuri inayotambuliwa ni kujibu hoja za bungeni? Utendaji kazi katika wizara na mwendesho mzima wa wizara si kipimo kinachokubalika?
 
Naibu waziri wa wizara hii ADAM Malima ana uwezo mkubwa kumshinda Ngeleja kwenye kujibu hoja na kuchapa kazi.kadri siku zinavyokwenda ukweli utadhihiri.
 
Naibu waziri wa wizara hii ADAM Malima ana uwezo mkubwa kumshinda Ngeleja kwenye kujibu hoja na kuchapa kazi.kadri siku zinavyokwenda ukweli utadhihiri.


masuala ya udini yanakuvuruga. Unaulete kila pahala brother unaharibu hali ya hewa
 
kazi ni kujbu hoja suala ni kutekeleza mapendekezo ya kamati ya Bomani,.. mbona hapo sioni jipya walilofanya hadi PM amimine sifa...
 
Kwa hiyo kazi nzuri inayotambuliwa ni kujibu hoja za bungeni? Utendaji kazi katika wizara na mwendesho mzima wa wizara si kipimo kinachokubalika?
Kosa kubwa ni kuchukulia uwezo wa mtu kuongea kama kigezo cha kuwa mchapakazi. Hili limetugharimu sana maana tunao mabingwa wa kupiga story karibu kila sehemu na utendaji wao ni dhaifu. Uzuri naona watu wameanza kuamka.Baadae tunaweza kupimwa katika yote mawili, kusema na kutenda. Hadithi nyingi bila matendo zimeshatuchosha
 
Kweli Pinda hapo kateleza kabisa yaani ukijua kuwajibu wabunge kwa kuwabembeleza na mashara kidogo ndio kuchapa kazi anatustaajibisha kabisa angetutolea takwimu basi kwamba hawa vijana wameongeza ajira ngapi kwa vijana wenzao kwa kuwapangia vitalu vya uchimbaji na kuwatafutia soko, la uhakika hawa vijana wanashuhudia vijana wenzao wanakufa njaa,wanatoa janja janja tu katika miradi ya kuwa inua vijana wazalendo yeye anawamiminia sifa,unaambiwa watu wa namtumbo wanalalamika kwamba watafiti wa uranium waliingia kinyemela hawajui kabisa walipewa ruhusa na nani yeye anasifu tu hii ni kali jamani huyu mkaka vipi sasa aangalie sana maswala ya kitaifa sio ya mzaha na kupakana mafuta kwa chupa ya mgongo
 
Back
Top Bottom