Pinda awaonya vigogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda awaonya vigogo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jan 14, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,468
  Trophy Points: 280
  Pinda awaonya vigogo
  Mwandishi Maalumu, Zanzibar
  Daily News; Wednesday,January 14, 2009 @20:20​

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema viongozi serikalini hawana budi ‘kujinyonga' kama kweli wanataka kumsaidia mkulima wa kawaida.Alitoa kauli hiyo jana mchana wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Cheju mara baada ya kukagua mradi wa kilimo cha mpunga katika Bonde la Cheju, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja.

  "Ninaposema kujinyonga nina maana tubadilike, tuache maneno maneno na tudhamirie yale tunayosema, la sivyo kilimo hakitaweza kuwa uti wa mgongo wa Taifa hili," alisema.

  Akifafanua, Waziri Mkuu alisisitiza kauli yake ya kuacha kununua magari ya serikali kama kweli viongozi wamedhamiria kuwasaidia wananchi. Alisema yeye anaposafiri na magari matatu ni sawa na kushika Sh milioni 300 na kwamba anaamini kama zingetumika kununua matrekta, yangepatikana mengi zaidi kuliko hayo magari matatu.

  "Ninasisitiza kwamba yote tuyafanyayo, changamoto iko kwetu sisi viongozi … bado hali ya kujipenda ni kubwa sana na wakati mwingine inatufanya tuzibe masikio … na ndiyo maana nikasema semina kwa sasa basi, ili tuonekama tutaokoa fedha hizo," alisema. Alisema: "Katika mwaka huu wa fedha, fedha zilizotengwa na wizara mbalimbali kwa ajili ya semina peke yake zimefikia Sh bilioni 33.

  Nilijiuliza nikikataza semina na fedha hiyo tukanunulia matrekta madogo, tutapata mangapi? Kwangu mimi kilimo cha jembe la mkono ni tatizo na bila kulibadili hatutaweza kusonga mbele." Akijibu risala ya wanakijiji hao, alisema serikali kwa sasa inakabiliwa na mtihani mkubwa wa jinsi gani itamsaidia mkulima azalishe kwa wingi zaidi kuliko alivyokuwa akifanya hapo nyuma.


  "Gharama ya kisima kimoja ni Sh milioni 12, kama Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja ataacha kununua gari, katika bajeti ijayo mtaweza kukamilisha visima vitano ambavyo mmesema mnavihitaji ili kusaidia kilimo cha umwagiliaji maji katika bonde hili … ninajua hili linawezekana lakini ni lazima viongozi tusimame kidete," alifafanua. Katika risala yao, wakazi wa Cheju waliomba serikali iwasaidie kutengeneza barabara ya kuingia katika bonde hilo ambayo gharama ya kuweka kifusi ni Sh milioni 34.

  Pia walisema visima vitatu kati ya vitano havifanyi kazi sababu ya kukosa umeme ambavyo gharama yake ni Sh. milioni 65.WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema viongozi serikalini hawana budi ‘kujinyonga' kama kweli wanataka kumsaidia mkulima wa kawaida.

  Alitoa kauli hiyo jana mchana wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Cheju mara baada ya kukagua mradi wa kilimo cha mpunga katika Bonde la Cheju, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja. "Ninaposema kujinyonga nina maana tubadilike, tuache maneno maneno na tudhamirie yale tunayosema,la sivyo kilimo hakitaweza kuwa uti wa mgongo wa Taifa hili," alisema.

  Akifafanua, Waziri Mkuu alisisitiza kauli yake ya kuacha kununua magari ya serikali kama kweli viongozi wamedhamiria kuwasaidia wananchi. Alisema yeye anaposafiri na magari matatu ni sawa na kushika Sh milioni 300 na kwamba anaamini kama zingetumika kununua matrekta, yangepatikana mengi zaidi kuliko hayo magari matatu.

  "Ninasisitiza kwamba yote tuyafanyayo, changamoto iko kwetu sisi viongozi … bado hali ya kujipenda ni kubwa sana na wakati mwingine inatufanya tuzibe masikio … na ndiyo maana nikasema semina kwa sasa basi.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mheshimiwa hapo anatapika mapovu.
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...napenda style yake ya kueleza issue kwa kutumia hard numbers!
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hii ya magari mbona kama hasikilizwi? Je wahusika wa ununuzi wakiamua kununua tu atawafanya nini ? angeweka wazi ieleweke isije ikawa ni mapovu tu.
   
 5. O

  Ogah JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mh Pinda....we need actions bana............. na sio maneno mingi!.....ukisema umesimamisha semina zinazo-cost billioni 33.....tunataka kusikia pia hospitali zetu mgao wake ni upi na pembejeo za wakulima mgao wake ni upi, na mashule/vyuo yetu mgao wake ni upi nk nk......we need actions actions actions....at least tueleze kiasi unacho-save utakitumia wapi na kwa sababu zipi......
   
 6. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #6
  Jan 15, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0


  Hivi kila kiongozi afisa mwandamizi wa serikali lazima awe na gari la serikali wakati akienda ofisini wakati wengi wao wanakaa tu ofisini hadi jioni wanaporudi tena nyumbani?

  Njia nyingine ya kubana matumizi ingekuwa ni kununua mabasi ya maofisa wa serikali wakaa mezani ambao hukaa mezani toka asubuhi hadi linatua jua.Badala ya kila ofisa wa serikali kuwa na gari la kifahari la kumpeleka na kumrudisha kazini mini bus au mabasi yangenunuliwa ya kuwabeba maofisa wote wa serikali wanaokaa eneo moja bila kujali wako wizara gani kuwapeleka maofisini kwao kama maofisi yao yako jirani.

  Mfano tuchukulie Masaki kuna maofisa wa serikali 30 wanaokaa eneo hilo wa wizara tofauti za serikali ambazo ziko katikati ya jiji la Dar es salaam badala ya kila wizara kununua magari ya kifahari 30 yenye madereva 30 ingenunua basi moja lenye dereva mmoja wa kuwabeba na kuwarudisha kazini badala ya kila ofisa kubebwa na lake.Na savings zinazofanyika zipelekwe kwenye kilimo huko au kokote kwenye kipau mbele.

  Serikali ifanye sensa wapi maafisa wengi wakaa mezani ofisini wanaishi iwajue Kimara wako wangapi,Masaki wangapi,Mikocheni wangapi,n.k halafu ione uwezekano wa kuwapa basi tu la kuwabeba wote na kuwarudisha kazini badala ya kila mmoja kuwasili katikati ya jiji na TOYOTA PRADO new model.

  Mtu ukienda ofisi za serikali utashangaa magari yalivyopangwa nje ya hizo ofisi utafikiri uko kwenye uwanja wa mnada wa kampuni ya magari ya kijapani.Hizo pesa zilizopaki kama magari ni “PARKED DEVELOPMENT CAPITAL” ambayo ingebadilisha maisha ya wananchi kama ingeingia katika uzalishaji badala ya kuiacha ime-park kwenye parking area ya ofisi ya wizara.

  Pinda shukrani kwa kuwa serious.Nadhani maofisa wa serikali wakikuelewa tutafika.Lakini kama mawazo yao na macho yao bado yako ndani kwenye magari yenye giza ndani yenye vioo tinted vya kutoonwa wala kuyaona matatizo ya wananchi hatutafika popote.​
   
 7. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mimi nauliza hivi ni lini Mh. Pinda atatoa instructions badala ya maombi???? Ndani ya instructions ni rahisi kutengeneza action plans na kuset delivarables ambozo zitakuwa checked against. lakini sasa kila siku anashauri na kulalamika tu mpaka lini??? mara akutane na makatibu wakuu wa wizara analalamika na kutoa ushauri tu. Naye Mr. Kikwete utamsikia hivyo hivyo. Siamini kama kwa staili hiyo tutafika mbali.
   
 8. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mimi nauliza hivi ni lini Mh. Pinda atatoa instructions badala ya maombi???? Ndani ya instructions ni rahisi kutengeneza action plans na kuset delivarables ambazo zitakuwa checked against. lakini sasa kila siku anashauri na kulalamika tu mpaka lini??? mara akutane na makatibu wakuu wa wizara analalamika na kutoa ushauri tu. Naye Mr. Kikwete utamsikia hivyo hivyo. Siamini kama kwa staili hiyo tutafika mbali.
   
 9. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pinda apindua ukulima? Sio uti wa mgongo?:confused:

  'Najinyonga'. Nitabadilika na maneno maneno,nitabandika maneno maneno ama sivyo Kula Breki!!! itaPinda!:D


  Nafikiri mkuu amenena tuone hizo action. :p
   
 10. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Hao Vigogo wanaonyeka au ni siasa za majukwaani tu.

  Akishasema ina maana kuna ufuatiliaji au ni basi tu bora liende.

  Watanzania kwa maneno ni asilimia 80 matendo 20 labda
   
Loading...